Mpendwa pole na hongera na hali ambayo hukuitarajia. Ngoja nikupe experience yangu. Mimi yalinikuta kama yako wakati first born wangu akiwa na miezi kumi na moja hivi. Nilijaribu kumwachisha mtoto ziwa mtoto akagoma kabisaaaa. Watu wakaniambia nikomae hivyohivyo, nikashindwa maana mtoto akagoma sasa kula chochote.
Nikaamua tu nimnyonyeshe hivyo hivyo. Mpaka mimba imekua kubwa nilikua namnyonyesha, ila kwa vile nilikua naamini kua maziwa yangu hayatakua na ubora kwa ajili ya ujauzito nikawa pia namfeed chakula kizuri, mayai ya kienyeji, supu za samaki na maharage, maboga, pudding za matunda, kifupi niliwekeza kwenye chakula chake.
Huwezi amini last time kumnyonyesha usiku, alfajir yake naingia leba. Watu walikua wananishangaa sana before, niko na mimba kubwaaa halaf nanyonyesha, nilikua nasemwa sana hata nikienda clinic wamama wengine wamejijengea hiyo imani eti namwaribu mtoto, ila walikua wanashangaa, katoto kamenawiri kana afya, kachangamfuu, basi wanakaa kuitana kunishangaa.