Hakuna tatizo kwenye jeshi kuwa na siri na hakuna jeshi lisilo la siri.
Haimaanishi Rwanda kufundishwa na Israel + Russia kwamba ndo iwe vizuri. Unaweza fundishwa na South Korea ukawa mtabe kuliko wenzako wote. Sisi kufundishwa na nchi zenye vikwazo bado haina tatizo tena hizo zenye vikwazo ziko vizuri mno kijeshi maana huwa zina ukorofi mkubwa. Imagine Iran anaweza kushambulia vituo vya US unadhani angekuwa mzembe angetoa wapi jeuri.
Majeshi ya nchi kadhaa hasa Uganda na DRC yanakuwa na graduates hapa chuo cha Monduli hivyo nakuwa na imani na uwezo wetu.