AAh, kids, kids! jamani wazee wenzangu kina Chriss, FL1, MJ1, Nyamayao, Fidel nk. nk, kazi tunayo jamani, tena kubwa tu,, nafikiri itabidi tuanzishe library ya mahusiano tuwe tunadesa kwanza maana hawa vijana watatupa presha na haya mahusiano.
Nachokiona mimi, vijana hawaelezani ukweli wakati wanaanza mahusiano, hawana trust wao kwa wao, hawapendi kuwa responsible na wanachoona wao ni ngono vs pesa.
I am afraid Gudboy kama umeamua kuwa na mpenzi mwanafunzi kuwa responsible bila malalamiko kwamba anakuchuna, au kaeni chini muongee kwa uwazi nini hupendi na nini hapendi, unajua wanawake tuko tofauti, sie wengine habari ya kumtegemea mwanaume hatuwezagi kabisa, yani habari ya kuomba sijui vocha, sijui pesa ya matumizi kwa upande wangu siwezagi, sijui ni kwa kuwa sipendi kuwa matonya. lakini kuna wengine wanaoamini ukiwa mwanaume you have to provide, so it depends unampenda kiasi gani, na una priority gani nae. pima mwenyewe kama unaona anakuyeyusha anza.