Je, nifanye biashara na ndugu wa kuzaliwa nae?

Je, nifanye biashara na ndugu wa kuzaliwa nae?

LDA COMPANY

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
340
Reaction score
622
Kama kichwa kinavyojieleza, je nifanye biashara na ndugu wa kuzaliwa nae au kila mmoja afanye yake tusije gombana?

Kuna kipindi nilifanya na brother mmoja ila nilikuwa naona kama yeye ndo inabidi apambane kwa kuwa ni mkubwa mimi na relax mpaka sasa maisha yamenipiga mbaya.
 
kama kichwa kinavyojieleza je nifanye biashara na ndugu wa kuzaliwa nae au kila mmoja afanye yake tusije gombana.
Ushauri, jifunze kutenganisha family na biashara au kazi, mapenz na biashara, undugu na biashara.

1.Utashndwa kufanya baadhi ya vitu kwa aibu ya undugu ,kama maonyo, kutumana nk.

2. Kutake advantage, ndugu anaweza kuchukulia poa matendo yake hata kama mabaya ktk biashara akijua ndugu hato nichukulia hatua. Hili likiwemo hata ufujaji.

3.Ndugu wachach sana, wenye busara ya kujituma ktk uaminifu ktk kazi za ndugu zao.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kwa sisi waafrika (ngozi) nyeusi tu inakuwa shida kufanya kazi/biashara pamoja.

Otherwise fanya naye ila kabla ya kuanza mkae kikao na kupeana 'makavu' kuhusu yale mambo yetu!.
 
Kufanya biashara na mtu ni kazi sana, mara nyingi kuna mmoja anakua ananyonywa

Kama mnafanya biashara na mtu inabidi wote muwe na same level of commitment,

Kufanya biashara na ndugu ni ngum sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenzetu Waasia na Wazungu mfano familia ya Grazer (wamiliki wa MAN U) wanafanikiwa kufanya kazi kindugu na kufanikiwa sisi watanzania tunakwama wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza ujue kama anafaa sio kufanya nae tuu maladii mnafanya bishara.

Wekeni makubaliano, na kugawana majukumu kwa kuweka commitment.

Pia hutakiwi kufanya nae kama ndugu Bali kama mfanya kazi tuu yani mkiwa kwenye biashara undugu usiwepo. Hapa ndipo tuna Kuja kufell Sana mana Kuna maamuzi huwa tuna shindwa kuyaamua.

Wakati mwingine wanasema usijaribu kumuamini mtu kwenye bishara Ata wew mwenyew ikibid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri, jifunze kutenganisha family na biashara au kazi, mapenz na biashara, undugu na biashara.

1.Utashndwa kufanya baadhi ya vitu kwa aibu ya undugu ,kama maonyo, kutumana nk.

2. Kutake advantage, ndugu anaweza kuchukulia poa matendo yake hata kama mabaya ktk biashara akijua ndugu hato nichukulia hatua. Hili likiwemo hata ufujaji.

3.Ndugu wachach sana, wenye busara ya kujituma ktk uaminifu ktk kazi za ndugu zao.



Sent using Jamii Forums mobile app

Hii ni kweli binafsi nilijaribu na Ndugu karibu wote biashara fulani. Niliishia kutengwa na familia nzima. Acha kabisa Ndugu.
 
Usijaribu usithubutu ..! Mm yamenikuta! Jamaa kila mtaa ana mwanamke na anakutambulisha kbs...ss mwachie lak 3 hapo ..inaisha bila hesabu..kumsema anazira!...huu mwez uishe tu kwakwel
 
Kama ni biashara ya kujikimu inategemeana na busara, tamaduni, maamuzi na tabia kati ya ndugu husika.

= = =

Ila kuna mtaji mkubwa kidogo, fungueni kampuni.

Kila Mtu apewe hisa zake kulingana na mtaji aliowekeza na kila mmoja alipwe mshahara kulingana na kazi anayofanya.

Kama Kampuni kila mmoja awe na mkataba kisheria na ajirini/husisheni watalamu kama hasa mtu wa sheria na mhasibu.

Hapo Hata Kama Mkikosana, Mkawa Hamsalimiani, Hisa Zako Ni Salama na hutaki kuendelea unauza hisa zako na kusepa kwingine
 
Back
Top Bottom