Je, nifuate computer science au film and multimedia and film technology??

Savagethug

New Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
3
Reaction score
0
Shikamooni,

Mimi ni form four graduate na Nina mpango wa kwenda college for further studies. Nina division 2 na nimebalance science subjects zangu zote pamoja na computer studies Kwa wastan wa "c".

Napenda sana mambo ya graphics sana sana motion graphics and animation.
Nilikuwa nataka nikasomee diploma ya multimedia and film technology kama major ila naogopa nitakosa chance ya kupata wide range of choices mbeleni.

Wazo liliopo kichwani ni kwamba either nisome computer Science alafu haya maswala ya multimedia na film technology nifanye kama hobby AU nichukue risk ya kuzama katika diploma ya multimedia and film technology nifate ndoto zangu. Ila Bado nipo njia panda sijui nifanyaje.

Ningeomba ushauri kutoka kwenu ili niwe safe baadae nisifanye kitu ambacho kitanifunga vibaya maishani especially financially.
 
Marhaba. . .
Hapo angalia unachokipenda zaidi, ambacho hata ukikosa ajira unaweza kujiajiri nacho. Nasisitiza soma unachokipenda zaidi na siyo kinachoonekana kina ajira
 
Angalau una ideal nn unataka ubase nacho. Muhimu kuangalia future ya hizo taaluma zaidi
 
Angalau una ideal nn unataka ubase nacho. Muhimu kuangalia future ya hizo taaluma zaidi
Eti uncle, Kwa expirience uliyo nayo, ipi kati ya hizo path Ina future nzuri?
 
Paragraph yako ya pili kutoka mwisho ndio ina jibu sahihi. Fanya hivyo mdogo wangu
 
Nna mashaka na Future ya hizo kozi unazozipenda kama Edzone alivyokueleza...

Maana siku hizi madogo wanaambiwa fanya unachokipenda ukirudi kitaa Msoto hata kujiajir kwa fani uliyosomea hauwez na haina wigo mpana wa kutoboa... Then unabak ningejilua hivi ningejua vile,

Hayo mambo ya wazungu fanya unachokipenda
Sasa hivi ni kozi gan inamwelekeo mzuri wa ajira na kujiajiri na ukimaliza hauwezi lala njaa hili ndo la msingi...

Sasa ww hizo kozi zako 2 unazozipenda nna mashaka nazo koz kuna watu wana bachelor ya hizo koz probably na wengine wana masters kabisa hususan hizo Computer science na hiyo film hata kusikia sijawah unless uwe na connection.

ila kuna watu wa certificate na diploma na maisha yanawaendea mzee bila msoto licha ya kuwa na elimu ndogo,

My point ni hii kama umefaulu vyema masomo ya science O-level especially Biology, Chemistry iwe included nenda Kozi za Afya za kibabe either Pharmacy, Medical Lab naamin possibility ya kutoboa ipo na haina msoto kivile kama ulisoma vyema na kumaliza vzur na possibly Radiology bado inawataalam wachache nchini ni mwendo kupiga vijiwe viwili mpaka vitatu per day.

Achana na mambo ya unachokipenda angalia Future ya maisha yako...
Msoto wa kitaa sio poa kijana...!

Akili kun Kichwa...!
 
Hivi siku hizi si kuna ma MD wapo kitaa na hawana ajira?
 
Usingoje chuo. Kama una bando ingia youtube anza kujifunza kutumia photoshop, illustrator nk nk!

Ushauri soma unacho penda ila hizo kozi ulizo taja zote ni rahisi kujiajiri ukiwa fiti na ukiwa na akili ya kujiajiri!

Popote utapo amua kwenda kasoma kazana uwe COMPITENT maama huwezi jiajiri usipo kuwa compitent.
 
Kama unajiona una uwezo mzuri hasa katika kufikiri tofauti na kubuni mambo na pia hujioni kabisa katika kundi la watu wanaopigania kuajiriwa, yaani ndoto zako ni kujiajiri na kufungua kampuni yako binafsi, soma computer science. Ila kama unategemea Ajira na kipaji cha kufikiri kiubunifu huoni kama unacho, endelea kupitia comments za wadau.
 
Ningekushauri ukasomee computer science ila jitahidi kukaza sana YouTube & udemy ili ukimaliza miaka 3 uwe guru kwelikweli
 
Kizazi chetu sio chakusikia akishahamua la kwake, ndo maana ukishaona anakwambia hivi mtafutia fursa kwenye kile anataka. Nina binti hapa ana One 5 PCB hataki kusikia kozi za afya, so wanayao kichwani
 
Kizazi chetu sio chakusikia akishahamua la kwake, ndo maana ukishaona anakwambia hivi mtafutia fursa kwenye kile anataka. Nina binti hapa ana One 5 PCB hataki kusikia kozi za afya, so wanayao kichwani
Dhaa kazi kwel ipo, mm huwa nnawaza hivi bora uwe na cheti ya hata kwa fani usiyoipenda lakin iwe na fursa,
then ukimaliza unaweza kufanya mambo yako unayoyapenda,

Msoto ukiwa mkali na mambo unayoyapenda at least una cheti chako kile unakifuta vumbi, unaingia kitaa life linasonga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…