Je nilipe kisasi?

Je nilipe kisasi?

Pure nomaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2011
Posts
1,158
Reaction score
1,385
Habari zenu wana JF
wakuu kuna manzi ambaye nilimtongoza zamani kidogo lakini yeye alinikataa kwa kunitolea maneno machafu mno.baada ya kusikia ana mimba na aliyempa kaikataa nikamtongoza tena na kunielewa bila shida nia yangu ikiwa ni kulipa kisasi.nna mpango wa kula "mzigo" na kuanza mbele,je ntekeleze azma yangu?au nisamehe tu?.ni hayo tu
 
Style yake ya kutoa maneno machafu ndo haikuwa nzuri..ila kukubaliwa na kukataliwa yote ni matokeo kwenye process nzima ya kutongoza. Accept that....Ila kisasi sikushauri!! Utajiumiza mwenyewe tu..
 
achana nae unaweza kumfikiria kumkomoa kumbe we ndo ukajikomoa,,,,, kimbia
 
Ukilipa kisasi unafikiri utakuwa shujaa ?watu wanamatatizo mengi mkuu usione raha kumfanyia mwenzio ubaya ,hata yeye anaweza kuwa na baya juu yako,ila ameamua kukuheshimu tu na kuthamini tu kama humpendi mwambie ukweli maisha yanasonga.
 
Kama ulimtongoza kitambo na you still feel that hate, then deep down bado wampenda. Hata hivo mapenzi ya kweli na dhati hayako hivo, daima one hutaka what is best for huyo ampendae aidha kakataliwa ama kakubaliwa. Unapomtongoza mtu sio lazima akukubali, maana roho bana hailazimishwi hata kidogo kupenda....... Haya baas kapata matatizo wataka kumuongeze kidonda emotionally na psychologically na on top of that ana mimba? Kua na huruma jamani.... Wanawake twapitia mengi, na whenever possible tujaribu epusha maumivu ya makusudi.
 
kisasi huwa hakiruhusiwi na sio kitu kizuri kabisa.

sasa hiyo ya kula mzigo, unaweza ukala utamu ukausikia kwa utosini, ukasahau yote, yale matusi ukaona ni wimbo mzuri alikuimbia ukashindwa kubanduka, fikiria kabla hujaumua, uwe tayari kulea mtoto kwa upendo kabisa.
 
Kama ulimtongoza kitambo na you still feel that hate, then deep down bado wampenda. Hata hivo mapenzi ya kweli na dhati hayako hivo, daima one hutaka what is best for huyo ampendae aidha kakataliwa ama kakubaliwa. Unapomtongoza mtu sio lazima akukubali, maana roho bana hailazimishwi hata kidogo kupenda....... Haya baas kapata matatizo wataka kumuongeze kidonda emotionally na psychologically na on top of that ana mimba? Kua na huruma jamani.... Wanawake twapitia mengi, na whenever possible tujaribu epusha maumivu ya makusudi.


HIvi kweli kama mtu bado anampenda mtu
atathubutu kusema huyu kijana alichosema hapo juu??
Binafsi naona ni bora ungemuuliza kama anampenda kuliko
kusema bado anampenda.. Maana maneno aliyoyatoa hayana upendo ndani yake kwa kweli..
 
We unataka kuchapa wakati anamzgo wa jamaa au kashajifungua,inaelekea una UKEKE kama wa jogoo
 
unajua kuna maradhi?

Tena maradhi mengine ni ya kihisia..Guilty consciousness! Just imagine dada yako ndio anafanyia hivyo...Utu na ubinadamu ni vitu vidogo lakini in real sense ni vikubwa sana..
 
Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Kisasi siyo tija!
 
Unapomtongoza mtu sio lazima akukubali, maana roho bana hailazimishwi hata kidogo kupenda....... Haya baas kapata matatizo wataka kumuongeze kidonda emotionally na psychologically na on top of that ana mimba? Kua na huruma jamani.... Wanawake twapitia mengi, na whenever possible tujaribu epusha maumivu ya makusudi.
hahahahah ndo maana kuna mada The Boss alidrop tofauti ya mvulana na mwanaume.sasa dada asha jitahidi na wewe ulete mada inayotofautisha msichana na mwanamke.kwa sababu moyo aulazimishw kupenda sasa ni mimba inamlazmisha huyo dada kwa muda uhu kumpenda jamaa AU? Muongozo tafadhali!
 
Mimi nafikiri hadi hpo Mungu ameshakulipia kisasi so wewe unatakiwa kutulia tu na kama utataka kulipa kisasi basi kwako litakuwa kosa na Mungu atamlipia huyo mwanamke kisasi juu yako. mie nafikiri hakuna haja ya kisasi. Fikiria ni wanawake wangapi ambao unahisi wanakupenda km wangepata nafasi ya kukuambia ungewakubalia wote? nafikiri ni wachache ambao ungekua nao.. sasa jiulize km hao ambao ungewakataa wangekua na roho ya kisasi wewe ungekua ktk hali gani?......... ni mtazamo wangu tu
Thanks
 
Back
Top Bottom