Je, nimekosea kuwapotezea baadhi ya ndugu zangu? Naomba ushauri tafadhali

Je, nimekosea kuwapotezea baadhi ya ndugu zangu? Naomba ushauri tafadhali

DALA

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2009
Posts
2,256
Reaction score
4,647
Nawasalimu nyote!

Moja kwa moja kwenye mada, historia yangu ina changamoto nyingi. Naamini kila mmoja ana changamoto yake. Kwa kifupi ni kwamba nimezaliwa kwenye familia ya wake wawili.

Mama yangu ni mke wa pili kwa Mzee. Aliolewa na Mzee baada ya mamkubwa kufariki miaka ya sabini. Nikiwa mdogo sana sikuona sikujua tofauti mpaka nilivyokuwa na umri wa kupambanua mambo. Mama yangu (sasa marehemu) alikuwa mpole sana na aliwapokea wototo wa mumewe bila shida.

Tatizo ni kwamba mama yangu alikuja kupatwa na ugonjwa mmoja mbaya sana, sitalitaja lakini ule ungonjwa ukawa ndiyo mwanzo wa matatizo yooote. Kwanza Mzee wangu anaonekana alimind Kwanini babu yangu alimuozesha mama yangu huku akijua binti yake anaumwa. Nilivyokuja kufanya utafiti, nilikuja kuambiwa kwamba mama yangu hakuwahi kuumwa kabla ya kuolewa na hata alipoolewa ilichukua miaka kadhaa ndo ugonjwa ukazuka.

Huu ugonjwa ulepelekea mama yangu kuwa kama mlemavu fulani hivi. Ikawa chanzo cha unyanyapaa usiyomithilika. Katika ukoo wetu baadhi hawakusema moja kwa moja kwa heshima ya Mzee lakini chini chini tuliishia kudharauliwa sana, mama yangu alidharauliwa sana. Kibaya zaidi ni kwamba mtoto wa kiume wa kwanza kwa mamkubwa alikuwa sehemu ya waliotudharau. Baadae alivyooa mke wake akawa ndo kabisaaaaaa. Kwake hata uji kunywa ilikuwa mbinde.

Kipindi hicho Mzee anapata vijisenti kidoog kidoog akafanikiwa kuwasomesha watoto wa Nyumba kubwa kwa alivyoweza. Kaka yangu mkubwa akapelekwa chuo cha ualimu baadae akaajiriwa na serikali, mtu wa kwanza kwenye ukoo kuajiriwa serikalini. Kichwa kikavimba. Mdogo wake pia wakiume akapelekwa naye chuo cha ualimu akapata ajira. Mdogo wao wa mwisho akapelekwa mpaka sekondari akaja kuolewa na mwanaume mwenye kipato cha wastani hivyo kiburi ikaongezeka.

Sisi kwa upande wetu, dada yangu mkubwa nakumbuka alikimbilia kuolewa akiwa mdogo sana kutokana na manyanyaso ya wana ukoo. Mimi nikaja kusoma sekondari kwa kujilipia. Kila wikendi nilikuwa narudi kijijini kukata miti ambayo Mzee alikuja kuingia dili na shule kununua kwa matumizi ya jikoni hivyo ikawa kama ada yangu.

Nakumbuka Mzee aliwahi kutoa kauli kwamba sisi watoto wa mke mdogo tunamsumbua na hatuna manufaa kama walivyo wale wa mamkubwa. Nilimind sana ila sikuwa na jinsi. Kwa watoto wa kiume upande wa mama, mimi ndiye mkubwa.

Nilivyomaliza sekondari sikufaulu vizuri na Mzee akawa hana mpango wa kunipeleka chuo. Bahati mbaya sijui niseme bahati nzuri. Wakati namaliza sekondari, dada yangu upande wa mamkubwa akawa anahitimu naye ualimu Ekenford Tanga. Alipokuwa anasoma Tanga, alijenga urafiki na familia moja ya kisambaa ambayo walimpa binti yao aje kumtembelea kwetu kujenga undugu.

Huyu binti nilikutana naye kwa wito wa dada yangu aliyenitaka nimuonyeshe mji wetu kidogo. Bahati mbaya tukapendana. Tatizo likawa naye amemaliza form four na alikuwa na mpango wa kuendelea na form five.

Nilichofanya ni kutafuta sababu ya kuja Dar ili niwe Karibu naye. Baadae akajiunga na high school Mpwapwa. Mtoto alikuwa mbichi, utepe niliukata mimi. Tatizo ni kwamba dada yangu alipogundua tupo serious hakupenda na mpaka leo sijajua ni kwanini na sikuwahi kumuuliza kwani alichofanya ni kuja Dar akakutana na familia ile, wakati huo mama wa huo binti na dada zake walikuja Dar, alinichafua sana.

Kilichofuata ni kwamba yule binti alipigwa biti sana na ndugu zake kiasi cha yeye kuchanganyikiwa. Wakati huo yeye bahati mbaya alikuwa shuleni hivyo hakuweza kunitetea dhidi ya uwongo ulokuwa unasemwa juu yangu.

Siku fanya lolote, nilichomuambia dada baada ya kupata zile taarifa ni “mwisho wa ubaya ni aibu” nikatulia.

Yule binti tulikuja kuachana kwani maji yalichafuka sana. Sasa baada ya pale shemeji yangu (mume wa dada) biashara ikabuma. Akafilisika kabisa mpaka kesho.

Katika kufilisika huko, ikabidi dada atafute kazi akahitaji kwenda kusomea kozi ya kufundisha shule maalumu. Nikaombwa kupitia dada yangu tumbo moja nimchukue binti yake aje anisaidie kukaa na mtoto badala ya kumuajiri mtu mwingine. Hii hoja ilikuwa ni kumsaidia dada yangu (mfini ni wangu) apate ada. Bila hiyana nilitoa ushirikiano na kumlipa hela kiasi ambacho asingepata kwa mwingine. Nilimpiga sound mke wangu (Mzungu) aelewe Kwanini tunamlipa dada kiasi kikubwa vile.

Cha ajabu baadae yule mpwa wangu akawa na tabia za kijinga tu ambazo hazieleweki hususani kwa namna ambavyo alikuwa ana relate na mimi ila nikapotezea. Baada ya yeye kuondoka na miaka ikapita nilishangaa kumbe kipindi yupo kwangu, mama yake alianza tena kuingilia ndoa yangu. Akatia fitina za kutosha. Haya nilikuja kujua siku moja tulikuwa na ugomvi wa nyumbani na mke wangu, kwa hasira akafunguka yote aliyokuwa akiambiwa na dada yangu kupitia mpwa wangu. Kumbuka hapo nimempa hela ndefu tu ya kulipia ada akanipa binti yake anisaidie kwa wakati ule.

Sasa mimi historia ya kunyanyapaliwa mama yangu na sisi watoto wake, bahati mbaya sana mambo yamebadilika mimi kusema kweli ndo nina kipato cha kueleweka, upande wa nyumba kubwa wanataka niwape tafu. Jambo hili sijaliafiki kwani hawakunipa hata pocket money wakati nasoma, hawakunilipia ada ila mafanikio yangu wanataka kuyafaidi.

Mzee ninamtunza kwa kidogo nachopata, niliwajengea nyumba ya uhakika ila kwa ndugu hawa nimekataa kabisa.

Sasa leo nimekuja hapa kupata ushauri, Mzee wangu amenitafuta kwamba dada (mfitini) amemuomba amsaidie kuniomba 5m ana shida kubwa. Hata kama ni kukopa. Nafsi inagoma kabisa. Yeye mwenyewe hawezi kuniomba moja kwa moja.

Nikiri kwamba alishaniomba msamaha mwaka 2018. Ila huu msamaha uliombwa kimkakati kwasababu uchumi wao ulishayumba ikawa jeuri haipo tena. So ilikuwa ni kama kutafuta njia ya kunirudisha kwenye anga zake.

Nisaidieni ushauri.
 
Kama una kipato cha kutosha cha kuweza kuwasaidia we Sadia tu. Hii Dunia tunapita we samehe naamini Mungu amekupitisha ktk changamoto zote hizo ndo maana Leo umekuwa hivyo.

Wadogo zangu tumbo moja nimewasomesha na hivi sasa namsesha mtoto wa dada yangu tumbo moja ila kule nimeshindwa kabisa kujitoa.
 
Golden chance never come twice. M/mungu hakukupa kwa bahati mbaya, kakupa wewe kisha kawaangusha wao kwa makusudi upate kulipa kisasi, sasa jifanye baba huruma halafu uje kuona cha mtema kuni.

Unamuona Diamond mjinga anavyo mdiss yule mzee wake eeh? Jifanye malaika utarudi kutuhadithia hapa! Mwanaume mzima unashindwa kuwa na misimamo, wanini ndugu kama hao, unawaweka weka karibu ili uvumbue nini kwa mfano?

Hata huyo baba ako ungempotezea tu, kwani shing ngapi? Wanakufanya jinga lao na watahakikisha wanakuharibia maisha kwa kukutumia wewe mwenyewe! Mwenye macho haambiwi 'ona', alieua kwa upanga nae afe kwa upanga. (Umenimwagisha mipovu km nakujua vile 🤣🤣)
 
Golden chance never come twice. M/mungu hakukupa kwa bahati mbaya, kakupa wewe kisha kawaangusha wao kwa makusudi upate kulipa kisasi, sasa jifanye baba huruma halafu uje kuona cha mtema kuni...
Nimekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom