Kama una kipato cha kutosha cha kuweza kuwasaidia we Sadia tu. Hii Dunia tunapita we samehe naamini Mungu amekupitisha ktk changamoto zote hizo ndo maana Leo umekuwa ivo.
Hakuna!! Asamehe hiyo vipi? Kwenye kukata hiyo migogo ili apate ada angeshuka mshipa wangemsaidia hata matibabu? Vipi km angepata tb au ulemavu wowote? Angeishia kuwa chokoraa au kibaka au teja kutokana na kutengwa na kudharauliwa ingekuwaje?
Mbona mnapenda kujazana unyonge bila sababu za msingi? Kwa kukushauri tu, mleta uzi, wanunulie smart 4n ndugu zako wote bila kumsahau baba ako, kisha anzisha group la whatsp, waunge wote, thereafter, anza kula bata huku unapiga picha na kuzitupia kwa group kila siku!
Hata ukiweza nenda viwanja vikubwa km mahoteli makubwa, piga picha ondoka, kawapostie, wakijileta tu unawapa kubwa, unawachana live bila chenga! Bila kusahau kutupia status za vijembe kwa baba ako, anza na hizi chache:
Uliookota nae kuni ndie utaota nae moto.
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Mama yangu ndio kila kitu kwenye maisha yangu.
Mtu mwenye kitu, asie na kitu kinyama cha mwitu.
Kikulacho ki nguoni mwako.
Mchawi ndugu, paka katumwa tu.