Je, nimekosea kuwapotezea baadhi ya ndugu zangu? Naomba ushauri tafadhali


Nanyenyekea mkuu. Hakika nakumbuka hata kwenda chuo ilibidi nipigane sana tu Dar mpaka nilipopata kazi ya uhakika nikajiunga KIU kwa vipindi vya jioni hapo nawasomesha pia wadogo zangu maana Mzee hapo Hana kitu.
 
Visasi havina maana sanasana ukikaa na kutafakari kuwa kuna vitu kama kifo hivi. Vipi shida aliyokuwa nayo dada yako ikampelekea kufa labda....haitakua fresh.
Binafsi sjawah kufikiria kujenga chuki hua naona kama furushi la misumari.
 
Nipo pamoja na wewe aise jamaa kazaaa kabisaaa. Kuwa mgumu ivyo ivyo ndugu hasa wakushare baba ni wanafiki haswaa
 
Tatizo nafsi inagoma kabisa.
Hiyo nafsi inayogoma ndo kitakachokumaliza,,, ni vizuri kuwa na HURUMA ila isipite kiwango..Saidia kile kilicho ndani ya UWEZO bila kujiumiza maana huyo hakuwa na wala hatokuwa na msaada na wewe..

Kiuhalisia hapo nikuwa huyo dada yako shida yake ni hiyo hela yako tu, na kwa historia ya familia yenu ni wazi huyo moyoni yuko na chuki kwako ila tu hali ya kifedha ndo inamfanya atulie.. Jiulize mfano ndo umempa hiyo hela leo halafu nawe hali yako ikawa dhoofu huko baadae, je atakuinua???...
Naongea haya from experience niliyonayo na familia zenye watoto wa matumbo tofauti ambazo kuwa na amani huwa ni ngumu sana haswa mnapotofautiana kipato...
 

Ni shida omera
 
Hili mbona jepesi sana,unapendwa sababu una kitu waza ungekuwa huna tena ingekuwaje?
PEOPLE WILL LOVE AND SUPPORT YOU WHEN IT'S BENEFICIAL.
Kukwepa lawama unaweza toa kidogo hata laki 5,ukasema kwasasa siko sawa ngoja nijipange Au kula bati mazima.Mzee mtunze hata kama sio kwa 100% sababu licha ya yote mzazi ni mzazi tu
 

Ushauri nimeupokea. Ahsante mkuu
 
Mzee nimemsamehe ila upande wa pili sitaki mazoea nao
Achana nao hao,hawakuthamini wanahitaji tu ela yako!siku ukiterereka kidogo ndo watakunyanyapaa zaidi ya mwanzo,
 
Visasi havina maana sanasana ukikaa na kutafakari kuwa kuna vitu kama kifo hivi. Vipi shida aliyokuwa nayo dada yako ikampelekea kufa labda....haitakua fresh.
Binafsi sjawah kufikiria kujenga chuki hua naona kama furushi la misumari.
MashaAllah tabarakaAllah... unaimani na yako Roho nyeupeee peer...
 
Mpe 50000 elfu,dawa ya jeuri ni kiburi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…