Je, nimetenda dhambi?

Watu hawana problem na uwezekano wa creator of the universe.. tatizo ni kwamba kila mtu anakuja anasema ameongea nae peke yake na anatupa masheria aliyotunga kichwani tufate ..at the same time anatutishia moto tusipomsikiliza na majority of human beings wanaamini coz wameambiwa wakiwa watoto... tatizo ndo hili tu. So wakija na maswali Yao Kama sijui nanasi limekuwaje tamu nawajibu tu we both don't know
 
kabisa kuna vitu ni ngumu kuvipuuzia ukishavijua
 
Dini ziko nyingi kuleta distractions , kuna negative forces ambazo zina kiongozi mmoja ndo anahusika na haya yote. Ndo maana nikakuambia just pray, Atheism haitakupeleka popote, kwasababu Atheism haiwezi ishi bila kuwa na Theism ila Theism haitegemei kabisa Atheism kwasababu origin yake inatoka kwa Muumba ambaye ni mmoja . Aisee naweza jaza vitu vingi ila Pray.
 
Biblia nafikiri ina maelezo sahihi ya dhambi nini; si maanishi kuwa dini zingine hazijaeleza hiyo dhambi ni nini.
Bibilia inasema dhambi ni uasi- uasi ni nini - ni hali yo yoye ya mtu kutenda kutenda jambo ambalo analiona si swa kwake na kwa jamii. Pia kwa wale tunaoamini uwepo wa Mungu ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu. Ndio maana dhambi yo yoye unayofanya kwa mwenzako unamkosoea Mungu. Kwanini? Kwa sababu Mungu alituumba sisi si kwakusudi la kutenda dhambi bali kwa kumtukuza Yeye.
Ndio maana mtu wa kwanza alitenda dhambi ya uasi; maana hakutii agizo la Mungu alililompa asilifanye naye akafanya. Na vizazi vilivyozaliwa baada ya hapo haivikulelewa tena katika misigi ya kumheshimu Mungu. Uovu wa kila uliongezeka toka hapo.
Mungu amefanya njia ya kutusaidia kubadilika kuondokana na hali hii ya uasi ambayo imo mioyoni mwa watu. Ndio maana ni rahisi mtu ye yote kuelekea kutenda mabaya kuliko kutenda mema. Njia yenye ndiyo inamsaida mtu kuondokana na utawala wa dhambi au uasi ulioumbika ndani yake. Njia hiyo nitaieleza vizuri baadaye kwa mtu anayetaka.
 
Mimi nafikiri tukiweza kuainisha dhambi itatusaidia kuwa na usawaziko na kuenenda katika njia zinazompendeza Muumba wetu.
Universalize your principles

Ipo hivii; dhambi ni tendo lolote ambalo kwa makusudi unalifanya na linamuumiza jirani yako maana hapo unakuwa umeenda kinyume na kanuni na ya kimungu ya TUPENDANE.

Basi dhambi mbaya kabisa inakuwa ni kumuumiza yule ambaye ulipaswa kumsaidia kwa matendo yako. Na kama alikuamini zaidi yaani ndiyo mbaya mnooo, usiombe

Tofauti na hivyo hapo ni makosa tu ya hapa na pale
 
Dhambi ni jambo lolote baya ambalo ukilifanya humchukiza Mungu na pia linakupelekea kupata adhabu mbele ya Mungu.

Kinyume cha dhambi ni hasanati (jema/wema) na malipo ya jambo jema huitwa thawabu. Kila jambo moja jema huandikiwa thawabu Kumi na kila baya moja huandikwa kama dhambi moja.

Hii ni kwa Mujibu wa dini ya Kiislam.

Dhambi zimegawanyika katika makundi mawili ...kuna dhambi kubwa na dhambi ndogo.

Dhambi kubwa ni zile ambazo zimeainishwa moja kwa moja kupitia Quran na Sunnah za Mtume Muhammad pamoja na ijamaa ya wanazuoni wa kiislam, na mwenye kuzifanya hustahiki kupatiwa adhabu au laana hapa hapa duniani na kesho Akhera. Ili hali Dhambi ndogo ni zile ambazo hazijaelezwa moja kwa moja ipi ni adhabu zake hapa duniani au kesho Akhera.


Miongoni mwa madhambi makubwa ni kama haya yafuatayo yaliyoainishwa na Mtume Muhammad (sala na amani ziwe juu yake)

"Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na uchawi, na kuuwa nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu ispokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya mapambano, na kuwazulia machafu wanawake waumini wenye kujihifadhi wenye kujizuia na machafu". (Imepokewa na Bukhari na Muslim)​

 
Kutovunja Amri 10 za Mwenyezi Mungu haiwezi kuwa kipeo cha Mkristo kwa vile kushika Amri na Sheria haitoshi.

"Sheria na Amri zake nimezishika zote tangu utoto wangu".
Yesu akamkazia macho (yule kijana) ... akamwambia: "Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo... kisha njoo unifuate" (Mat. 19:20-21; Mk. 10:20-21).

Iko hivi, anayeshika Sheria tu akiangalia halali na haramu, hajatimiza Sheria, kwasababu "Utimilifu wa Sheria ni upendo". ( Warumi 13:10).
 
Mkuu Pantosha , kwa Wakristo na Waislamu, dhambi ni kumkataa Mwenyezi Mungu, na kukataa amri zake.
Lakini pia, Wakristo na Waislamu wana mambo fulani ambayo wanaachana kimtazamo kuhusu dhambi.

(A) Kwa Waislamu, Dhambi ni uasi mbele ya Mwenyezi Mungu.
Sifa kuu ni kumtii Mungu; kwahiyo Dhambi ni kukataa kutii.
Mwislamu haaimbiwi kupima matendo yake kwa kipimo cha Mapendo kama Mkristo.
Mwislamu haambiwi kuwa kufanya hivi ni vema kwasababu kunampendeza Mungu au kufanya vile ni vibaya kwasababu kunamchukiza Mungu.
Mwislamu anaangalia kama Sheria inamruhusu kutenda vile ama la.

Kwake matendo ni ya aina 5:
1. Matendo ya lazima:
kufunga, kuswali, kutoa zakat ... Akiyatenda anapewa tuzo; asipotenda anapata adhabu
2. Matendo ya hiari: yule ayatendaye anapata mastahili; asipotenda hakuna kosa wala adhabu
3. Matendo yasiyo mema wala mabaya: ukiyatenda hupati tuzo, wala adhabu; Sheria ipo kimya kuhusu hayo
4. Makuruhi: matendo ambayo hayakatazwi na sheria; lakini hayapendezi. Ukiyatenda hupati adhabu.
5. Matendo yanayokatazwa na sheria (haramu): kama hatia, dhambi, maasi. Ukiyatenda, adhabu inakuhusu sana.

Lakini ktk hali ya kawaida kuna aina 2 za Matendo:
1. Matendo halali: yale yaliyohalalishwa
2. Matendo Haramu: yale yaliyokatazwa yasitendwe ( Q 66:6)
Kwa Waislamu dhambi hukaa katika matendo.
Mungu huwapenda wafanyao mema (2:196)

(B) Kwa Wakristo, kuna tofauti kubwa; hawaangalii kama tendo fulani ni halali au haramu, bali kama linampendeza Mungu au kama linamchukiza; kwao hakuna matendo yasiyokuwa mema au mabaya, yakifanywa na moyo mwema, basi ni mema. Yakifanywa kwa nia mbaya , basi ni mabaya. Kwao, dhambi hukaa katika moyo.
Haramu/halal - soma hapo juu.
Kuoa wake wengi
Kwa Waislamu, ndoa haikukusudiwa kumletea mwanadamu taabu na dhiki; "Basi tutamrahisishia (mwanadamu) mambo kuwa mepesi (92:8).
Kwa Mkristo, ndoa ni namna ya kutimiza amri kuu ya Yesu ya kupenda mwenzake kama anavyojipenda mwenyewe.
Nao watakuwa mwili mmoja (Mt. 19:5-6)
Kula aina fulani ya nyama kutoka kwa wanyama fulani,

Mimi nafikiri tukiweza kuainisha dhambi itatusaidia kuwa na usawaziko na kuenenda katika njia zinazompendeza Muumba wetu.
 
Shukrani kwa kuboresha nukuu ya andiko langu.

Tuendelee kukumbushana kuhusu uwepo wa Pepo na maisha baada ya kiama
 
Nimekuelewa. Unachotaka ww ni sawa na kusema tufanye dini iwe moja, dunia nzima. Ni kitu ambacho hakiwezekani.
Kwanini ?

Dhambi inakua defined na dini husika. Mfano, uislam una katiba yake halkadhalika Ukristo.

Kila dini kati ya hizo umeve define baadh ya mambo kua ni dhambi, separately.

Unaposema tufanye dhambi ziwe universal maana ake unasema tuzi combin dhambi zinazodefiniwa na uislam na zile zinazodefiniw na wakrist ziwe kitu kimoja. Hiwezekani
 

Dhambi Kubwa zaidi ni Kumshirikisha Mwenyezi Mungu (Shirki)

“Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”
Biblia Takatifu - Kutoka 20:3-5

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa.​



Al Qur-aan 4:48
 
Kila dini inatishia hivi...asa utamwamini Mungu yupi na kumwacha yupi na usiseme Mungu ni mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…