Nianze kwa ku kiri kuwa nimelelewa kwenye maadili ya kikristu lakini pia nimebahatika kuishi maeneo ambapo Waislam ni wengi. Tukiwa wadogo wazazi wetu walituruhusu tuhudhurie Madrasa. Watoto wengi hapo mtaani kwetu walitoka familia za Kiislam.
Katika harakati zangu za kijipanga kupambana na Dhambi ili niweze kuishi vizuri hapa duniani na hatimaye kuyarithi makao huko mbinguni, najiuliza dhambi ni nini? Je dhambi ina sifa zipi?
Mkuu
Pantosha , kwa Wakristo na Waislamu, dhambi ni kumkataa Mwenyezi Mungu, na kukataa amri zake.
Lakini pia, Wakristo na Waislamu wana mambo fulani ambayo wanaachana kimtazamo kuhusu dhambi.
(A) Kwa Waislamu, Dhambi ni uasi mbele ya Mwenyezi Mungu.
Sifa kuu ni
kumtii Mungu; kwahiyo Dhambi ni kukataa kutii.
Mwislamu haaimbiwi kupima
matendo yake kwa kipimo cha
Mapendo kama Mkristo.
Mwislamu haambiwi kuwa kufanya hivi ni vema kwasababu kunampendeza Mungu au kufanya vile ni vibaya kwasababu kunamchukiza Mungu.
Mwislamu anaangalia kama
Sheria inamruhusu kutenda vile ama la.
Kwake matendo ni ya aina 5:
1. Matendo ya lazima: kufunga, kuswali, kutoa zakat ... Akiyatenda anapewa tuzo; asipotenda anapata adhabu
2. Matendo ya hiari: yule ayatendaye anapata mastahili; asipotenda hakuna kosa wala adhabu
3. Matendo yasiyo mema wala mabaya: ukiyatenda hupati tuzo, wala adhabu; Sheria ipo kimya kuhusu hayo
4. Makuruhi: matendo ambayo hayakatazwi na sheria; lakini hayapendezi. Ukiyatenda hupati adhabu.
5. Matendo yanayokatazwa na sheria (haramu): kama hatia, dhambi, maasi. Ukiyatenda, adhabu inakuhusu sana.
Lakini ktk hali ya kawaida kuna aina 2 za Matendo:
1.
Matendo halali: yale yaliyohalalishwa
2.
Matendo Haramu: yale yaliyokatazwa yasitendwe ( Q 66:6)
Kwa Waislamu dhambi hukaa katika matendo.
Mungu huwapenda wafanyao mema (2:196)
(B) Kwa Wakristo, kuna tofauti kubwa; hawaangalii kama tendo fulani ni halali au haramu, bali kama linampendeza Mungu au kama linamchukiza; kwao hakuna matendo yasiyokuwa mema au mabaya, yakifanywa na moyo mwema, basi ni mema. Yakifanywa kwa nia mbaya , basi ni mabaya. Kwao, dhambi hukaa katika moyo.
Kwa nini nauliza haya maswali? Ukweli ni kwamba kutokana na kusikia mahubiri tofauti tofauti kuhusu dhambi imebidi mimi nitake kufahamu dhambi ni kitu gani na Je tunaweza kuainisha sifa za dhambi ambazo zitakuwa Universal ili kuondoa mkanganyiko kwa wanadamu na hivyo kutusaidia kuziepuka?
Mfano ni swala la pombe. Hii ni HARAMU kwa baadhi ya dini, halali kwa baadhi.
Haramu/halal - soma hapo juu.
Kwa Waislamu, ndoa haikukusudiwa kumletea mwanadamu taabu na dhiki; "Basi tutamrahisishia (mwanadamu) mambo kuwa mepesi (92:8).
Kwa Mkristo, ndoa ni namna ya kutimiza amri kuu ya Yesu ya kupenda
mwenzake kama anavyojipenda
mwenyewe.
Nao watakuwa mwili mmoja (Mt. 19:5-6)
Kula aina fulani ya nyama kutoka kwa wanyama fulani,
Mimi nafikiri tukiweza kuainisha dhambi itatusaidia kuwa na usawaziko na kuenenda katika njia zinazompendeza Muumba wetu.