SimbaMpole123
JF-Expert Member
- Apr 23, 2023
- 5,501
- 4,956
Unataka ujue ukweli, dini zote ni man made...so unauliza according to dini gani..na interpretation ipi..Kuna madhehebu zaidi ya laki tatu ndani ya ukristo pekee...nobody knows dhambi ni Nini coz kila mtu ana interpretation zake za sheria za wayahudi au waarabu Ila we fata sheria za nchi na ishi na watu vizuri ukiendelea kumwamini Mungu wako. Kutojua dhambi ni ipi sio kosa lako ni kosa la aliyekufikishia huo ujumbeNianze kwa ku kiri kuwa nimelelewa kwenye maadili ya kikristu lakini pia nimebahatika kuishi maeneo ambapo Waislam ni wengi. Tukiwa wadogo wazazi wetu walituruhusu tuhudhurie Madrasa. Watoto wengi hapo mtaani kwetu walitoka familia za Kiislam.
Katika harakati zangu za kijipanga kupambana na Dhambi ili niweze kuishi vizuri hapa duniani na hatimaye kuyarithi makao huko mbinguni, najiuliza dhambi ni nini? Je dhambi ina sifa zipi?
Kwa nini nauliza haya maswali? Ukweli ni kwamba kutokana na kusikia mahubiri tofauti tofauti kuhusu dhambi imebidi mimi nitake kufahamu dhambi ni kitu gani na Je tunaweza kuainisha sifa za dhambi ambazo zitakuwa Universal ili kuondoa mkanganyiko kwa wanadamu na hivyo kutusaidia kuziepuka?
Mfano ni swala la pombe. Hii ni HARAMU kwa baadhi ya dini, halali kwa baadhi.
Kuoa wake wengi
Kula aina fulani ya nyama kutoka kwa wanyama fulani,
Mimi nafikiri tukiweza kuainisha dhambi itatusaidia kuwa na usawaziko na kuenenda katika njia zinazompendeza Muumba wetu.