Je, nimtonye mteja kuwa amepigwa na fundi ama nikae kimya?

Je, nimtonye mteja kuwa amepigwa na fundi ama nikae kimya?

Kuna fundi kaja hapa kisha akampa Mteja nionge nae mteja akasema nimpe mahitaji anayo taka kisha nimtumie bili zote

Nondo pis 28 fundi aka chukuwa 14 tu
Binding ware 10 fundi kachukuwa tatu
Mifuko 20 Y cement fundi kachukuwa 10 tu

Nimeingiwa huruma sna kwani mteja anapigwa mno na ukizingatia kwa sasa upatikanaji wa pesa imekuwa kwa mbinde
Mno

Nataka nimueleza mteja kijanja ila nimekosa namna ya kumuazia na ripoti ya Leo , pia nina wasi wasi wenda wananitega pia wanizukumizie kesi ya uhujumu uchumi nina wasi wasi kweli kweli

Pia nawaza fundi akijuwakuwanimewauza je akinifanyia umafya itakuwaje

Naomba mnipe mbinu ya kufanya wakuu mteja atanilipa Leo ama kesho
Mkuu hongera Kwa kumiliki biashara hiyo.

Kwahiyo GUTA huendeshi tena
 
Kula nyama nyamaza mkuu ili kesho tena fundi akipata dili arudi kukuchangia ndio Bongo hii
Ndio maana hii nchi haitakuja kuendelea kamwe sababu viongozi pamoja na raia wake wote wezi, na laana hii haita isha, hata wale wasio husika nao wameshirikishwa na wamekuwa wezi pia,
 
Mkuu ww chukua Chako kinachokuhusu km vp mwambie fundi akuachie ten ya maji maishà yaendelee,,Kwan huyo afsa yy ajui hapo nondo zinatakiwa ngapi na afiki saiti kwakee kukagua...

Mwache fundi apate Hela ya kuongaa😅😅😅
Haya ndiyo madhara ya hii nchi kukuzwa katika wizi , ona sasa raia nao wamesha kuwa na roho za wizi , yan hapo huoni tatizo?
 
Ndio maana hii nchi haitakuja kuendelea kamwe sababu viongozi pamoja na raia wake wote wezi, na laana hii haita isha, hata wale wasio husika nao wameshirikishwa na wamekuwa wezi pia,
Viongoz ndiyo wamefundisha raia kuiba
Ukosefu wa maadili umeanzia juu
Potelea pote kila mtu ale urefu wa kamba yake
 
Usiwe mnoko kula vizur na mafundi upate wateja ohoo hi dunia ni ushenz ty
 
Back
Top Bottom