Je nina tatizo katika afya yangu?

Je nina tatizo katika afya yangu?

regnaldshirima

Senior Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
124
Reaction score
78
mimi ni kijana wa miaka 23,nilizaliwa nikiwa na afya nzuri na sikuwa nasumbuliwa na magonjwa

nilipoingia shule ya sekondari nilisumbuliwa na vidonda vya tumbo kuanzia 2006 mpaka 2010 ambapo ilifikia mahali nikatapika damu usiku nikiwa nimelala sikusikia maumivu yoyote,asubui kulipokucha ndipo nilijikuta nina damu sehem za mdomoni na tishet nilikua nimelala nayo,nilikwenda kutazama seheem nilipotapika nikakuta damu nyingi imeganga nilipatwa na hofu na kuwaita wazazi wangu nao hawaku amini kama hali iyo nikonayo.ifahamike kipindichote hicho nilidhohofika kiafya na kuwa mwembamba. basi wazazi walinitaka nisiwe mbali nao na shule nisiende ingawa wiki iliyokua inafuata nilikua na mtihani wa necta. basi jioni muda wa saa2 hivi nikiwa na wadogo zangu na wazazi wangu tunaongea niliaga naenda uwani sikufika hata mlangoni kwani kizunguzungu kilikua kikali niliyumbayumba na kuangua nilisikia naitwa tu kujibu siku weza nilijikaza nikanyanyuka tena niliposima wima niliendelea kwenda nilipokua naelekea kama hatua tano hizi nilianguka tena niliita mama waliposikia walitoka wote kwa kasi kutokana na kishindo cha mimi kuanguka walifika nakunikuta natapika damu si ongei nimelalala na tumbo tu. tokea hapo sikua nafahamu yoyote nilikuja shtuka nipo kwenye gari na wapo watu wengi ambao nakumbuka walikua jirani na kwetu pamoja na majirani.walisema nimefungua macho,haikupita muda nili poteza fahamu tena hadi nilipofikishwa hospital ndo nkazinduka tena ilichukua muda kkuhudumiwa nilikua nikitazama tu nisiweze kuongea toke hapo sikujua nini kiliendelea.kulingana na maelezo ya ndugu yangu aliniambia kila ulipochomwa sindano ulihangaika sana na mwili ulivimba kupita kiasi,madakta wa zamu walipata kazi kila walipojaribu labda aina hii itamsaidia kulingana dam yake. asubui saa5 ndo nilizinduka na kuamka kitandani kama roboti bila kujua ni wapi kisha nikatulia vipimo vilianza kufanyika ingawa madaktari hawakuamini nilikua natapika damu basi vipimo vililetwa na kubainisha sina maradhi yoyote zaidi ya uti,na kitu kama kidonda katika sehemu ya (katikati ya tumbo na utumbo mdogo, kidonda hicho baada ya siku ka tatu hakikuonekana tena.

siku na nguvu ya kusimama pekee yangu.

nilijitaidi kula ilinirudishe afya yangu siku fanikiwa,lakini nilipokuja kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito niliona mabadiliko kwa haraka napo acha napungua tena



naomba ushauri wenu nami napenda kuwa na afya nzuri kwani sina kimo cha kusema mimi ni mrefu zaidi ya huu wembamba

nahitaji kujua

> Njia za kurudisha afya ya mgonjwa wa muda mrefu.?
>Matatizo ya tumbo huchangia kupungua kwa absoption ya nutrient mwilini ni vipi nitabackup.?
>je mtu alie dhohofika afya kutokana na maradhi misuli,na body fat haviwezi jijenga upya?
 
Maelezo marefu sana

Kwa sasa unaumwa nini? taja uzito na urefu wako pia sema kwa sasa unaishi wapi
 
Back
Top Bottom