Je ninaweza kurudi chuo baada ya kuacha bila taarifa yoyote

wakusepa

Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
83
Reaction score
5
Hello wana jf.
Kwa wazoefu na waliopo vyuoni je hili linawezekana.
Imepita miaka mitatu tangu niache chuo bila kutoa taarifa yoyote.na ku deal na biashara,sasa nataka kurudi chuoni nilikukowa nasoma kutokana na busines zangu kutokaa vyema..
Wakati nasoma nilipata bum asilimia 20 kwa wakati ule,na nilikatiza mwaka wa kwanza sem. Ya 2..je nifanyeje nirud?na je taarifa zangu chuo ztakuwepo.
Msaada waungwana
 
Wewe sio muungwana. Kwa sababu uliacha bila kuaga hauna chance manake ulijifukuzisha. Na habari ya mkopo sahau. Tafuta ada ukasome upya, elimu haimtupi mtu.
 
Wewe sio muungwana. Kwa sababu uliacha bila kuaga hauna chance manake ulijifukuzisha. Na habari ya mkopo sahau. Tafuta ada ukasome upya, elimu haimtupi mtu.

mkubwa ada ilikuw n tatizo
 
umejifukuzisha na unaweza usipate tena nafasi chuoni hapo
 
Kama uliondoka bila sababu hawawezi kukuruhusu.ila unaweza kutafuta cheti cha ugonjwa then ukawaambia uliumwa sana na ndugu zako ni watu wa kijijini hawakujua hata kutoa taarifa.ila pia kusamehewa inatokana na uongozi wa chuo unachosoma.nadhani miaka mitatu ndio kikomo cha kupostpone masomo
 
Wewe sio muungwana. Kwa sababu uliacha bila kuaga hauna chance manake ulijifukuzisha. Na habari ya mkopo sahau. Tafuta ada ukasome upya, elimu haimtupi mtu.

Hahaha,

Wewe ukiwa ndo dean of admissions mbona watakukoma!

Ila inabidi tujue chuo gani, kuna vyuo vingine vimekaa kimaslahi na as long as unaongeza occupancy wanaku admit back, na mpaka credit zako wanakupatia.

Swali halijatoa details za kutosha kuwezesha jibu la maana.

Ukitoa detail unaweza kukutana na ma dean of admissions wenyewe humu (ombea wasiwe King'asti type)
 
Mkuu hebu m2mie PM huyu Dr.Kitila Mkumbo naye atakusaidia sababu ni muhusika wa mambo haya lakin hapa usitegemee jibu zuri sababu wengi hawajali tatizo la mtu.
 
Last edited by a moderator:
Hahahaha.

Mie sina mswalie mtume kwenye uzembe. Sikawii kucharaza viboko. Wenzie wameuza barafu na soda bwenini hadi wakamaliza shule analeta pozi hapa. Ukitokea familia ya kimaskini lazma uwe sharp upstairs kuliko wenye ada zao. Afu ushauri hajaomba kabla hajaacha chuo, anaomba saa hizi! Na hajajua siku hizi mkopo ni lulu!
 
Sina hakika siku hizi wanatakaje lakini walikuwaga wanataka mtu akiwa discontinued asiombe kwa miaka 3.

Jaribu bahati yako. Hunacha kupoteza zaidi. Ila ndo ukajipange bwana. Wenzio ulaya wanaosha vyombo McDonalds hadi wanamaliza shile wanatudi hapa na viwalo!
ok,shukran mkubwa,je nkiomba tcu siwez kupata chuo,ikbid na mkopo?
 
Nenda ubalozi wa Belgium au Germany waombe wakupe taratibu za kusoma undergraduate courses kwenye chuo cha Bonn au Ghent-nafasi zipo nyingi tu
 

Maisha ni tofauti kwa watu tofauti.

Huyu anaweza kuongeza ujuzi darasani kwa vile karudi na "business experience".

Ni kwa sababu elimu ya juu ni bidhaa adimu tu nchini mwetu, nchi ambazo wanaelewa elimu ni nini halafu inaendeshwa kiushindani hamna tatizo mtu kurudi shule baada ya kupiga kazi.

Watu wanaanza kukuelewa kwamba inawezekana umepata matatizo kabla hata hujawaeleza vizuri.
 
good plan,let me try.ahsante muungwana
kwa idea nzur
 

sawa sawa mkubwa,details zip unazozingumzia hapo juu,unahtaj kupew
 
Nenda ubalozi wa Belgium au Germany waombe wakupe taratibu za kusoma undergraduate courses kwenye chuo cha Bonn au Ghent-nafasi zipo nyingi tu

ni ghali muungwana,kwenda outside,naenda na hali halis
 
sawa sawa mkubwa,details zip unazozingumzia hapo juu,unahtaj kupew

Kwanza chuo gani?

Sihitaji mimi bali mtu yeyote anayetaka kukusaidia anaweza kukusaidia vizuri zaidi kama anajua unazungumzia chuo gani, maana itifaki na taratibu zinaweza kutofautiana chuo hadi chuo, au hata chuo kimoja muhula hadi muhula.

Humu mpaka ma dean of admission tunao wanaweza kuku PM kama wewe kijukuu una zali lako.

Halafu lazima unawakomalia kuwaonyesha kwamba ile ilikuwa ni detour tu umeenda kupata darasa vile vile kwenye ulimwengu wa kweli, darasa litakalokufanya uwe well rounded na makini zaidi ukirudi darasa la chuo.

Na ikibidi kama kuna mpango wa kukupa credit kutokana na biashara ulizofanya - na kudokumeti, fafa noma- wauzie mchongo vile vile.

Sio kila mtu anaweza kumaliza degree kwa mpigo, kuna wengine mitikas kibao inaweza kuibu, kuibuka katikati ya michongo ya chuo.

Hata Bill Gates alikipotezea chuo, tena Harvard, na hata hakurudi. Leo wote hapa tunatumia mi computer yenye software zake.

Itakuwa wewe bwana kijukuu.

Nenda, mguu wa safari hata mtume kauombea, huwezi kugagangamala tu bila kujaribu zali. Amazon.com ya bongo tutaipataje?

Ila kaa ukijua elimu ya juu bongo rohostoki nyingi sana.

Kukutana na dean of admission mwenye roho ya kupetesha watu ka nilivyokupa hapo juu si rahisi.

Wengi wao wamekaa kupiga watu chini ka King'asti tu.

Ndo maana tunalosti, kina Einstein kibao, wanaishia kulamba vumbi tu.
 
Mkuu hebu m2mie PM huyu Dr.Kitila Mkumbo naye atakusaidia sababu ni muhusika wa mambo haya lakin hapa usitegemee jibu zuri sababu wengi hawajali tatizo la mtu.

ahsante mkuu ntampata wapi huyu dr.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…