Kifo ni spiritual experience. Shifting of dimension tu, huwezi shift kwenda dimension ingine pasipo roho itawalayo au iishie kwenye ile dimension. Kwani huwa huoti ndoto au ku fall into trance?Natamani sana kuna watu ambao ilishawahi kuwatokea hii waje wathibitishe.
Mkuu umesoma vizuri lakini?Wewe na huyo ChatGPT wote ni waongo, huyo mtu atalipoti vipi alivyojisikia kufa wakati amesha kufa? Ukweli ni kwamba utamuona tu Isirael mtoa roho akija na panga lake kwa mbwe nyinyi na mwikwala kibao mwisho utahisi tu shwaaaaaaaa umeshaenda kama ng'ombe machinjoni.
Hakuna vitu kama hivyo, hizi stories zimeletwa na watu wa dini kabla ya hapo hakukuwai kuwa na hizi stories za kusadikika.Inategemeana na mtu alikuwa anaamini nini, kama alikuwa anaamini malaika atawaona na kama alikuwa anaabudu mashetani basi ataona mashetani, tena mashetani ya kutisha
Hao hawakufa na hawakupitia kitendo cha kufa bali sehemu ya akili ambayo haihusiani na matendo ya hiari huamka the same way akili inavyoamshwa na wale wafanya meditation mwili unakuwa ktk paralyse lkn akili kupitia milango ya fahamu ya ndani(Nafsi) ambayo haiutegemei mwili kuhisi, huwa active na kuona kila litendekalo ktk mazingira yanayouzunguka mwili.Mkuu umesoma vizuri lakini?
Siyo kwamba mtu alikufa yaani alikaribia kufa mfano kupata ajali mbaya pia kuhusu kusimulia...baada ya kupata fahamu huwa wanaeleza matukio yaliyokuwa yakiendelea mfano wanasimulia madaktari walivyokuwa wanafanya.
Huo ukweli wewe umeujuaje ?Wewe na huyo ChatGPT wote ni waongo, huyo mtu atalipoti vipi alivyojisikia kufa wakati amesha kufa? Ukweli ni kwamba utamuona tu Isirael mtoa roho akija na panga lake kwa mbwe nyinyi na mwikwala kibao mwisho utahisi tu shwaaaaaaaa umeshaenda kama ng'ombe machinjoni.
Hata wewe hapa ukijaribu kufanya meditation utayapitia hayo aliyoyapitia huyo ndugu yako.N.D.E aliipata Shangazi yangu baada ya kupata Ajali .. (Aligongwa na Baiskeli) alikuw afe.
Baada ya fahamu kumrudia (akiwa ICU) alisimulia same scenario ya watu wengine wanayopitia N.D.E
Yeye yake ilikuwa tofauti kdg sana, aliitwa sehemu aende.. akaangalia nyuma.. akagoma kwenda na kurudi nyuma. (Inavyosemekana, kama angekubali kwenda basi alikuwa Afe).
Ni siku nyingi sana.. ntamtafuta nimuulize zaidi...
Je hata hao watu wa mediation na wao hupata maumivu makali wakati wa kurudi katika mwili wao?Hata wewe hapa ukijaribu kufanya meditation utayapitia hayo aliyoyapitia huyo ndugu yako.
Kifo kinapotokea huwa hakuna excuse ni lazima ufe either unataka au hutaki maana hiyo huwa ni nguvu ya asili ambayo inatambua uwepo wako duniani kwa siku na saa ambazo lazima uzikamilishe na zinapokamilika ni lazima tu ufe iwe kwa ajali au hata mafua lazima yakuondoshe,
Hayo mambo ya kuitwa na kuona watu sijui mambo gani ni yakawaida na mara nyingi ni viumbe wa sanaa(pepo wa giza) ambao ndio hawa hawa huwapa maono wale wanaojiita wachungaji au wale wanaosema walipelekwa kuzimu na mbinguni kumbe ni michezo ya hawa viumbe wenye uwezo wa kuteka akili na kuionesha maono yoyote ili mtu huyu baada ya akili Yake ya kimwili kuamka akayasimulie haya mambo ambayo kiuhalisia ni uongo na uzishi.
Nikazie tena, mtu yoyote anayefanya meditation anaelewa hili jambo unapofungua mlango wa fahamu wa mwili wako na nafsi yako automatic unakuwa ktk ulimwengu wa mwili na nafsi kwa wakati mmoja ambapo lazima utakuwa na uwezo wa kuona/kuhisi uwepo wa viumbe wengine ambao ndio hao huishawishi nafsi yako kubaki ktk makazi hayo ili ziutawale mwili wako kama vile wanavyotawaliwa watu wenye pepo,
Zoezi hili likifanikiwa mtu huyu anakuwa kapagawa na pepo lakini hafi bali anapoamka huamka akiwa tayari anamilikiwa na pepo, na zoezi hili halihusiani na kifo wala pepo hao hawana uwezo wa kukutoa uhai.
Mambo haya hamuwezi kufundishwa ktk hizo dini zenu maana yako BEYOND ufahamu wa watu waliofungwa na mafundisho ya kidini.
subiri lissu akirudi tumuulizeHakuna vitu kama hivyo, hizi stories zimeletwa na watu wa dini kabla ya hapo hakukuwai kuwa na hizi stories za kusadikika.
Mtu yeyote anapokufa anapitia hatua ambayo angepitia muovu au mtenda mema, hizo habari zenu za kuona malaika na mashetani ni uzushi umeletwa ambao hauna ushahidi, vile vile huwezi kuleta masimulizi ya mahala ambapo hakuna mtu amewai kwenda akarudi, hivyo stories zenu zinabaki kama ngonjera za kusimulia watoto muda uende.
Dini zimeleta hofu kwa watu kuofia hata kwa kitu ambacho ni asili hakihusiani na mambo ya kutishana wala hizo hukumu zenu na Mbingu za mchongo.
Anayesema ukifa unaenda mbinguni sijui jehanamu muulize anaushahidi upi? Kama hajaanza kusema kasikia kwa fulani au kaona imeandikwa mahala fulani, why asilete ushahidi aliouna yeye kama yeye?.
Hakuna aliyewai kufa akarudi, hayupo na hatowai kuwepo, kiuhalisia hata hawa mnaowaona wamezinduka mkidai walikufa, kiuhalisia walipitia tu kitendo cha baiolojia ambapo Ubongo unakuwa active lakini mapigo ya moyo yanasimama kwa zaidi ya saa72,
Madactari wanaelewa hili, ndiomana kuna mashine za kushitua mapigo ya moyo ili mtu huyu aamke, ikishindikana kama akili(ubongo) bado uko active mtu huyu lazima ataamka tu hata zipite siku5, kwa maana hakufa bali alikuwa ktk DEEP SLEEP PARALYZE.
Tutafute maarifa tuache kuupa uongo kipaumbele hata kwa mambo mepesi
Nilimsindikiza babu yangu nikamuacha getini.Huo ukweli wewe umeujuaje ?
Sasa hizo ni ndoto za kuzimia siyo kufa.Mkuu umesoma vizuri lakini?
Siyo kwamba mtu alikufa yaani alikaribia kufa mfano kupata ajali mbaya pia kuhusu kusimulia...baada ya kupata fahamu huwa wanaeleza matukio yaliyokuwa yakiendelea mfano wanasimulia madaktari walivyokuwa wanafanya.