Je, nini kimepelekea wajasiriamali (wafanyabiashara) kuwa wengi nyakati hizi? Je, nyakati zijazo kutatokea nini kwenye hili kundi la watu?

Yaani hata asipo uzaa bidhaa na hata asipoona kuna faida kwenye ujasiriamali fulani ataendelea kubaki na kufanya hiyo biashara??
Yaani hivi ndivyo ilivyo tena wengi wanalenga zile biashara ambazo haziharibiki au zinakaa muda mrefu sana hadi kuharibika.

Mfano unakuta mtu anafremu nyumbani kwake anaenda kuchukua mitungi yake anipanga hapo, hata kama inatembea kidogokidogo yeye hana hasara maana halipi kodi uyupo kwake au mingine anaweka nguo.

Yaani ilimradi tu, sasa hii imefanya kuwa na biashara kila kona biashara zenyewe ni zilezile, hivyo tunagawana tu wateja.
 
Naomba nikujibu Kwa ufupi kama ifuatavyo..

Baada ya miaka kadha wajasiriamali matakuwa na uwezo WA kurithisha biashara Kwa familia zao..

Je, hiyo ajira siku ukiondoka duniani ndicho kitu utarithisha wanao?
 
Watu washahama kwenye ajira wengi tumekuwa wajasiriamali. Je! Napo pia watu watahama kwenye huu ujasiriamali? Na kama wakihama watahamia kwenye shughuli gani?? Maana kila zama na nyakati zake.

Watu wataanza kujikita kwenye uzalishaji wa bidhaa za viwandani ivyo tutegemee wakati ujao kuona watu kuwa na viwanda vidogo vidogo vya kati na ongezeko la viwanda vikubwa ambapo pia itakua ni kichocheo cha biashara na kuanza kutafuta masoko nje ya nchi kama wafanyavyo mataifa yaliyoendelea na ayo ndio tunaita maendeleo
 
Yaani ujasiriamali siku hizi imekuwa kama fashion kila mtu anajaribu kuwa mjasiriamali, ukipita mtaani hivi vibaraza vya majumbani wamama wamefanya sehemu ya kuuzia vitafunio wameweka hadi madeli ya vitafunwa kwenye vibaraza vya majumbani yaani imekuwa too much
 
Na huu mrundikano wa jiji unachangia na watu kuhama kutoka mikoani na kuja hapa jijini, kweli serikali inahaja ya kujaribu kujenga miji mingine nje ya dar ili kupunguza huu mrundikano.
 
Ngoja tuone itakuaje ila unawaza sahihi Mkuu, Vita ya Kiuchumi ni lazima ni swala la Muda tu.
 
Hakuna wajasiriamali hapa kuna wabangaizaji, mdalali na watu kuhangaika kutafuta mkate wa kila siku, sababu hakuna ajira specific za kuweza kuweza kuwapatia ujira...

Ndio maana kila likitoka tangazo la ajira mtu mmoja wanakwenda watu elfu moja..., In short its getting worse watoa huduma wamekuwa wengi kuliko wahitaji.., hakuna systematic system kila kitu bora liende...
 
Naomba nikujibu Kwa ufupi kama ifuatavyo..

Baada ya miaka kadha wajasiriamali matakuwa na uwezo WA kurithisha biashara Kwa familia zao..

Je, hiyo ajira siku ukiondoka duniani ndicho kitu utarithisha wanao?
Ujasiriamali haurithishwi labda biashara, ila ujasiriamali si mishe ya kudumu kwanza haina makazi rasmi na anayefanya hana uhakika wa kuishi hivo ujasiriamali inategemea na uhai wa mtu, mtu anapokufa ujasiriamali nao unakufa
 
Una logic sana mkuu.
 
Sorry nimemaanisha ilianza tangu enzi ya mitume na manabii.
Nadhani wewe ulitaka labda biashara ianzishwe na Adamu sasa angemuuzia nani wakati alikuwa peke yake.
Na kitu kingine kumbuka unapoenda kufanya kazi ya kuajiriwa kwenye kampuni fulani hiyo pia ni biashara ya mtu ila anakuwa amenunua muda wako ukamfanyie biashara yake.
 
Na huu mwisho wake utakuwaje??
 
Atakula nini kama hapati faida.
Unashangaa,,, kuna watu wanalazimisha kufanya biashara hata kama asipouza ilimradi nae aonekane anafanya biashara. Watu wanyakati nashindwa kuwaelewa .

Kuna mdau mmoja apo kasema wengi wanaumua kuuza bidhaa zinazokaa mda mrefu bila kuharibika kama mitungi ya gesi, mavazi nk hata kama hauzi atalazimisha tu awe na biashara hata kwenye fremu ya nyumbani kwake ilimradi alipi kodi
 
Biashara na ujasiriamali ndio mfumo wa uchumi kwa wanadamu....
 
Sasa hivi huduma za mikopo zimetapakaa tu kila kona sio makazini sio mitaani imekuwa rahisi sana watu kufungua vitega uchumi
 
Pesa za kujikimu anapata wapi mkuu, niliwahi fanya biashara ya kuuza nguo za mitumba tena kutembeza nguo barabara huku nina family inanitegemea, unajua kilitokea nini na wakati huo nimepanga na sina chanzo kingine cha kipato.

Niliuza siku kadhaa naweka mtaji kuna siku nauza na kuna siku siuzi kabisa, aisee zilifululiza weeks kadhaa sioni faida na mwisho nikala mtaji nikatafuta kazi za vibarua mtaani saidia fundi na mungu alivo kuwa fundi nikapata kazi ya muda mrefu kwa mafundi basi bhna familia na kodi ikawezekanika.

Ila ujasiriamali bila mtaji ni kelele asa pale unapo tegemea ule kupitia hapo huku mtaji ni mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…