Je, nini kimepelekea wajasiriamali (wafanyabiashara) kuwa wengi nyakati hizi? Je, nyakati zijazo kutatokea nini kwenye hili kundi la watu?

Je, nini kimepelekea wajasiriamali (wafanyabiashara) kuwa wengi nyakati hizi? Je, nyakati zijazo kutatokea nini kwenye hili kundi la watu?

Yaani hata asipo uzaa bidhaa na hata asipoona kuna faida kwenye ujasiriamali fulani ataendelea kubaki na kufanya hiyo biashara??
Yaani hivi ndivyo ilivyo tena wengi wanalenga zile biashara ambazo haziharibiki au zinakaa muda mrefu sana hadi kuharibika.

Mfano unakuta mtu anafremu nyumbani kwake anaenda kuchukua mitungi yake anipanga hapo, hata kama inatembea kidogokidogo yeye hana hasara maana halipi kodi uyupo kwake au mingine anaweka nguo.

Yaani ilimradi tu, sasa hii imefanya kuwa na biashara kila kona biashara zenyewe ni zilezile, hivyo tunagawana tu wateja.
 
Habarini wakuu! Toka majuzi nimekuwa nikijiuliza maswali mengi hili suala la wajasiriamali kuwa wengi nyakati hizi tofauti na miaka ya zamani let say 90's.

Kipindi cha miaka ya 90's wajasiriamali na wafanyabishara walikuwa wachache sana, yaani kukuta duka la Mangi moja mtaa mzima au kijiji kizima ilikuwa ni kawaida sana. Mzee wangu anakumbuka nyakati hizo,, wateja walikuwa wanapanga foleni kwa wenye maduka, biashara zilikuwa chache, sijui hili inamaanisha nini au kipindi hicho watu walikuwa Bize na kulima?? ama walikuwa Bize na kusoma ili kuja kuajiriwa??

Katika miaka hiyo nahisi watu suala la biashara kipindi hicho haikuwa kipaumbele chao, watu walikuwa Bize na masuala ya elimu kusoma ili kuajiriwa serikalini ama sekta binafsi au pia inawezekana watu wengine walikuwa vijijini wako Bize na kilimo na pengine walishindwa kuja mjini na hivo kuliacha kundi la watu wachache kufanya biashara ama wengine huwa wajasiriamali hasa maeneo mbalimbali ya miji.

Miaka ya 90's hakukuwa na soko la kariakoo ilo mnaliona miaka hii karibuni, bali soko kubwa la jiji la Dar lilikuwepo posta na mnazi mmoja.

Sasa sijui nini kulipeleka kukuwa kwa masoko mengi ya wafanyabishara nyakati hizi ukianzia soko la kariakoo, tegeta , Manzese, Buguruni, Mbagala, ubungo (ilikuwa zamani), na hata hapa Mbezi mwisho nilipo, wajasiriamali tumejaa kila kona. Ukipita mitaa ya Mbagala kila nyumba inafremu la duka la Mangi na sio Mbagala tu hata huku mitaani maduka ni mengi. Mama ntilie ndio usiseme wemejaa kila kona, kuna wanauza chai na uji wakitembeza kwenye vijiwe na majumbani achilia mbali wale wamama wanaouza mihogo akitembea mtaa kwa mtaa, mama zangu wa mbogamboga wamejaa kila mahali.

Yaani siku hizi kila mtu ni mjasiriamali haijalishi huyu kuajiriwa ama hajaajiriwa , haijalishi huyu ni mtoto wa au ni mtu mzima yaanj naona madogo siku hizi nao wamo kwenye gemu ya ujasiriamali, achilia mbali wanasiasa, wazee , wamama nao siku wamechangamka tofauti na wamama wa miaka ya 90's waliokuwa wakishinda nyumbani, ila siku hizo wote tupo nao masokoni kila mtu ni mjasiriamali aliyesoma na asiyesoma wote tupo kwenye gemu la ujasiriamali yaani daah shiiiiidaaaa hili ni bomu soon nahisi litalipuka tu kama zilivyo kwenye ajira za wasomi.

Huwa najiuliza baada ya haya yote ya kila mtu kuwa mjasiriamali je nini kitatokea miaka ya baadaye je kutakuwa na mfumo mpya na option mpya za watu kufanya shughuli nyingine tofauti na ujasiri na kama zitakuwepo ni zipi hizo?? Watu watakuwa na mishe gani mbali na ujasiriamali???

#Natanguliza_shukurani_wakuu
Naomba nikujibu Kwa ufupi kama ifuatavyo..

Baada ya miaka kadha wajasiriamali matakuwa na uwezo WA kurithisha biashara Kwa familia zao..

Je, hiyo ajira siku ukiondoka duniani ndicho kitu utarithisha wanao?
 
Watu washahama kwenye ajira wengi tumekuwa wajasiriamali. Je! Napo pia watu watahama kwenye huu ujasiriamali? Na kama wakihama watahamia kwenye shughuli gani?? Maana kila zama na nyakati zake.

Watu wataanza kujikita kwenye uzalishaji wa bidhaa za viwandani ivyo tutegemee wakati ujao kuona watu kuwa na viwanda vidogo vidogo vya kati na ongezeko la viwanda vikubwa ambapo pia itakua ni kichocheo cha biashara na kuanza kutafuta masoko nje ya nchi kama wafanyavyo mataifa yaliyoendelea na ayo ndio tunaita maendeleo
 
Yaani hivi ndivyo ilivyo tena wengi wanalenga zile biashara ambazo haziharibiki au zinakaa muda mrefu sana hadi kuharibika.

Mfano unakuta mtu anafremu nyumbani kwake anaenda kuchukua mitungi yake anipanga hapo, hata kama inatembea kidogokidogo yeye hana hasara maana halipi kodi uyupo kwake au mingine anaweka nguo.

Yaani ilimradi tu, sasa hii imefanya kuwa na biashara kila kona biashara zenyewe ni zilezile, hivyo tunagawana tu wateja.
Yaani ujasiriamali siku hizi imekuwa kama fashion kila mtu anajaribu kuwa mjasiriamali, ukipita mtaani hivi vibaraza vya majumbani wamama wamefanya sehemu ya kuuzia vitafunio wameweka hadi madeli ya vitafunwa kwenye vibaraza vya majumbani yaani imekuwa too much
 
Hii ni kweli lakini huu mrundikano wa wajasiriamali umekithiri zaidi hapa jijini Dar es salaam, huko mikoani utakuta bado hakujachanganya kihivyo.

Ila hii ya Dar kufulikia inachangiwa na mengi, ikiwemo kurahisishwa kwa njia za uchukuzi, hivyo imeweza kumfanya hata mtu anayeishi nje ya mji kuwa na biashara zake mjini huku akiishi nje ya mji au mkoa jirani.
Hapo nisikwambie wingi wa wakazi ambao nao wameamka sasa kuanza kufanya biashara, plus wale wanaotoka mikoani kuja Dar kwa lengo la kuanza maisha.

Hivyo kuna haja ya mamlaka kuongeza juhudi katika kuongeza mizunguko ya pesa mikoani pia ili kupunguza hii mirundikani ya wajasiriamali katika huu mji.
Na huu mrundikano wa jiji unachangia na watu kuhama kutoka mikoani na kuja hapa jijini, kweli serikali inahaja ya kujaribu kujenga miji mingine nje ya dar ili kupunguza huu mrundikano.
 
Na soko la ushindani litakuwa kubwa, pengine wauzaji wa bidhaa tutakuwa wengi kuliko wanunuzi (wateja). Nadhani unafahamu athari za kuwa na competition kwenye biashara wenye nguvu za hela watabaki kubwa juu huku wajasiriamali wadogowadogo wakibaki kubwa masikini.

Na endapo nchi ikaexpand kibiashara na kuifikia dubai pangine nchi zingine tunazolingana nazo kiuchumi zitafika level hio, hofu yangu ni kubwa kuhusu international trade inamaana kutakuwa na ushindani kibiashara baina nchi na nchi na mwishowe kuleta vita vya kiuchumi na solution sijui itakuwa ni nini je watu watahama kwenye huo mfumo wa biashara na ujasiriamali?? Na kama wakihama watahamia kwenye shughuli gani?? Maana naona technolojia kila inazidi kukua na sijui tunakoelekea hasa kwenye la ujasiriamali.
Ngoja tuone itakuaje ila unawaza sahihi Mkuu, Vita ya Kiuchumi ni lazima ni swala la Muda tu.
 
Hakuna wajasiriamali hapa kuna wabangaizaji, mdalali na watu kuhangaika kutafuta mkate wa kila siku, sababu hakuna ajira specific za kuweza kuweza kuwapatia ujira...

Ndio maana kila likitoka tangazo la ajira mtu mmoja wanakwenda watu elfu moja..., In short its getting worse watoa huduma wamekuwa wengi kuliko wahitaji.., hakuna systematic system kila kitu bora liende...
 
Naomba nikujibu Kwa ufupi kama ifuatavyo..

Baada ya miaka kadha wajasiriamali matakuwa na uwezo WA kurithisha biashara Kwa familia zao..

Je, hiyo ajira siku ukiondoka duniani ndicho kitu utarithisha wanao?
Ujasiriamali haurithishwi labda biashara, ila ujasiriamali si mishe ya kudumu kwanza haina makazi rasmi na anayefanya hana uhakika wa kuishi hivo ujasiriamali inategemea na uhai wa mtu, mtu anapokufa ujasiriamali nao unakufa
 
Hakuna wajasiriamali hapa kuna wabangaizaji, mdalali na watu kuhangaika kutafuta mkate wa kila siku, sababu hakuna ajira specific za kuweza kuweza kuwapatia ujira...

Ndio maana kila likitoka tangazo la ajira mtu mmoja wanakwenda watu elfu moja..., In short its getting worse watoa huduma wamekuwa wengi kuliko wahitaji.., hakuna systematic system kila kitu bora liende...
Una logic sana mkuu.
 
Usiseme ni asili ya Mwanadamu,, watu walikuwa na shughuli za kufanya kabla ya kuja kwa mfumo wa biashara, ukirudi kwenye hostori kabla ya barter trade system watu walikuwa na shughuli nyingi za kufanya.

Ingekuwa ujasiriamali ni asili ya mwanadamu pengine barter trade ingeanza pindi tu binadamu wanapoumbwa
Sorry nimemaanisha ilianza tangu enzi ya mitume na manabii.
Nadhani wewe ulitaka labda biashara ianzishwe na Adamu sasa angemuuzia nani wakati alikuwa peke yake.
Na kitu kingine kumbuka unapoenda kufanya kazi ya kuajiriwa kwenye kampuni fulani hiyo pia ni biashara ya mtu ila anakuwa amenunua muda wako ukamfanyie biashara yake.
 
Hakuna wajasiriamali hapa kuna wabangaizaji, mdalali na watu kuhangaika kutafuta mkate wa kila siku, sababu hakuna ajira specific za kuweza kuweza kuwapatia ujira...

Ndio maana kila likitoka tangazo la ajira mtu mmoja wanakwenda watu elfu moja..., In short its getting worse watoa huduma wamekuwa wengi kuliko wahitaji.., hakuna systematic system kila kitu bora liende...
Na huu mwisho wake utakuwaje??
 
Atakula nini kama hapati faida.
Unashangaa,,, kuna watu wanalazimisha kufanya biashara hata kama asipouza ilimradi nae aonekane anafanya biashara. Watu wanyakati nashindwa kuwaelewa .

Kuna mdau mmoja apo kasema wengi wanaumua kuuza bidhaa zinazokaa mda mrefu bila kuharibika kama mitungi ya gesi, mavazi nk hata kama hauzi atalazimisha tu awe na biashara hata kwenye fremu ya nyumbani kwake ilimradi alipi kodi
 
Sasa hivi huduma za mikopo zimetapakaa tu kila kona sio makazini sio mitaani imekuwa rahisi sana watu kufungua vitega uchumi
 
Unashangaa,,, kuna watu wanalazimisha kufanya biashara hata kama asipouza ilimradi nae aonekane anafanya biashara. Watu wanyakati nashindwa kuwaelewa .

Kuna mdau mmoja apo kasema wengi wanaumua kuuza bidhaa zinazokaa mda mrefu bila kuharibika kama mitungi ya gesi, mavazi nk hata kama hauzi atalazimisha tu awe na biashara hata kwenye fremu ya nyumbani kwake ilimradi alipi kodi
Pesa za kujikimu anapata wapi mkuu, niliwahi fanya biashara ya kuuza nguo za mitumba tena kutembeza nguo barabara huku nina family inanitegemea, unajua kilitokea nini na wakati huo nimepanga na sina chanzo kingine cha kipato.

Niliuza siku kadhaa naweka mtaji kuna siku nauza na kuna siku siuzi kabisa, aisee zilifululiza weeks kadhaa sioni faida na mwisho nikala mtaji nikatafuta kazi za vibarua mtaani saidia fundi na mungu alivo kuwa fundi nikapata kazi ya muda mrefu kwa mafundi basi bhna familia na kodi ikawezekanika.

Ila ujasiriamali bila mtaji ni kelele asa pale unapo tegemea ule kupitia hapo huku mtaji ni mdogo.
 
Back
Top Bottom