Je, nini kimepelekea wajasiriamali (wafanyabiashara) kuwa wengi nyakati hizi? Je, nyakati zijazo kutatokea nini kwenye hili kundi la watu?

Je, nini kimepelekea wajasiriamali (wafanyabiashara) kuwa wengi nyakati hizi? Je, nyakati zijazo kutatokea nini kwenye hili kundi la watu?

Na huu mwisho wake utakuwaje??
Fujo, vurugu, chuki baina ya watu, gap ya walionacho na wasionacho kuendelea kuongezeka, in short threat kwa civilization (na hapa siongelei Tanzania bali ulimwengu mzima) With advance in technology nguvu kazi imepunguzwa na uzalishaji umeongezeka...

Gen Z wamezoea kuagiza vitu online na sio kwenda window shopping kupoteza muda.., wewe duka lako mafichoni unashindana na watoa huduma dunia nzima (AMAZON mmoja ana uwezo wa kutoa huduma kila kona...; Hilo lisingekuwa tatizo kama kila mtu angekuwa na ujira wa kuweza kununua ; lakini wengi wao mlo tu wa kila siku ni tatizo,,,

Kwahio utaona the current system is doomed to fail na ujasiriamali sio utatuzi wa majority (sababu ujasiriamali ni tabia na way of life; sio kila mtu ana discipline hio, wala sio last resort ya watu wakikosa cha kufanya); Ujasiriamali hapo kale ulisaidia kwa wachache kuzalisha ajira kwa wengi, since manpower haiitajiki tena utaona kwamba mchango wa hawa wachache haupo tena (no more trickle down effect - it does not trickle any more)
 
Pesa za kujikimu anapata wapi mkuu, niliwahi fanya biashara ya kuuza nguo za mitumba tena kutembeza nguo barabara huku nina family inanitegemea, unajua kilitokea nini na wakati huo nimepanga na sina chanzo kingine cha kipato.

Niliuza siku kadhaa naweka mtaji kuna siku nauza na kuna siku siuzi kabisa, aisee zilifululiza weeks kadhaa sioni faida na mwisho nikala mtaji nikatafuta kazi za vibarua mtaani saidia fundi na mungu alivo kuwa fundi nikapata kazi ya muda mrefu kwa mafundi basi bhna familia na kodi ikawezekanika.

Ila ujasiriamali bila mtaji ni kelele asa pale unapo tegemea ule kupitia hapo huku mtaji ni mdogo.
Kuna watu wameajiriwa lakini akili zao zinawaza biashara, hivo kuhusu mtaji na pesa za kujikimu kwenye hili kundi sio inshu sana kwao tofauti na sisi, sasa mimi huwa najiuliza huyu kuajiriwa lakini bado anataka afanye biashara yaani aje agawane wateja na sisi ambao hatuna shughuli rasmi zaidi ya huu ujasiriamali tunaougombania huku masokoni
 
Habarini wakuu! Toka majuzi nimekuwa nikijiuliza maswali mengi hili suala la wajasiriamali kuwa wengi nyakati hizi tofauti na miaka ya zamani let say 90's.

Kipindi cha miaka ya 90's wajasiriamali na wafanyabishara walikuwa wachache sana, yaani kukuta duka la Mangi moja mtaa mzima au kijiji kizima ilikuwa ni kawaida sana. Mzee wangu anakumbuka nyakati hizo,, wateja walikuwa wanapanga foleni kwa wenye maduka, biashara zilikuwa chache, sijui hili inamaanisha nini au kipindi hicho watu walikuwa Bize na kulima?? ama walikuwa Bize na kusoma ili kuja kuajiriwa??

Katika miaka hiyo nahisi watu suala la biashara kipindi hicho haikuwa kipaumbele chao, watu walikuwa Bize na masuala ya elimu kusoma ili kuajiriwa serikalini ama sekta binafsi au pia inawezekana watu wengine walikuwa vijijini wako Bize na kilimo na pengine walishindwa kuja mjini na hivo kuliacha kundi la watu wachache kufanya biashara ama wengine huwa wajasiriamali hasa maeneo mbalimbali ya miji.

Miaka ya 90's hakukuwa na soko la kariakoo ilo mnaliona miaka hii karibuni, bali soko kubwa la jiji la Dar lilikuwepo posta na mnazi mmoja.

Sasa sijui nini kulipeleka kukuwa kwa masoko mengi ya wafanyabishara nyakati hizi ukianzia soko la kariakoo, tegeta , Manzese, Buguruni, Mbagala, ubungo (ilikuwa zamani), na hata hapa Mbezi mwisho nilipo, wajasiriamali tumejaa kila kona. Ukipita mitaa ya Mbagala kila nyumba inafremu la duka la Mangi na sio Mbagala tu hata huku mitaani maduka ni mengi. Mama ntilie ndio usiseme wemejaa kila kona, kuna wanauza chai na uji wakitembeza kwenye vijiwe na majumbani achilia mbali wale wamama wanaouza mihogo akitembea mtaa kwa mtaa, mama zangu wa mbogamboga wamejaa kila mahali.

Yaani siku hizi kila mtu ni mjasiriamali haijalishi huyu kuajiriwa ama hajaajiriwa , haijalishi huyu ni mtoto wa au ni mtu mzima yaanj naona madogo siku hizi nao wamo kwenye gemu ya ujasiriamali, achilia mbali wanasiasa, wazee , wamama nao siku wamechangamka tofauti na wamama wa miaka ya 90's waliokuwa wakishinda nyumbani, ila siku hizo wote tupo nao masokoni kila mtu ni mjasiriamali aliyesoma na asiyesoma wote tupo kwenye gemu la ujasiriamali yaani daah shiiiiidaaaa hili ni bomu soon nahisi litalipuka tu kama zilivyo kwenye ajira za wasomi.

Huwa najiuliza baada ya haya yote ya kila mtu kuwa mjasiriamali je nini kitatokea miaka ya baadaye je kutakuwa na mfumo mpya na option mpya za watu kufanya shughuli nyingine tofauti na ujasiri na kama zitakuwepo ni zipi hizo?? Watu watakuwa na mishe gani mbali na ujasiriamali???

#Natanguliza_shukurani_wakuu
Jambo la kisikitisha kwenye kilimo & ufugaji tunakula kona ndo maana recent mazao yote hayashikiki ukienda sokoni.!
 
Fujo, vurugu, chuki baina ya watu, gap ya walionacho na wasionacho kuendelea kuongezeka, in short threat kwa civilization (na hapa siongelei Tanzania bali ulimwengu mzima) With advance in technology nguvu kazi imepunguzwa na uzalishaji umeongezeka...

Gen Z wamezoea kuagiza vitu online na sio kwenda window shopping kupoteza muda.., wewe duka lako mafichoni unashindana na watoa huduma dunia nzima (AMAZON mmoja ana uwezo wa kutoa huduma kila kona...; Hilo lisingekuwa tatizo kama kila mtu angekuwa na ujira wa kuweza kununua ; lakini wengi wao mlo tu wa kila siku ni tatizo,,,

Kwahio utaona the current system is doomed to fail na ujasiriamali sio utatuzi wa majority (sababu ujasiriamali ni tabia na way of life; sio kila mtu ana discipline hio, wala sio last resort ya watu wakikosa cha kufanya); Ujasiriamali hapo kale ulisaidia kwa wachache kuzalisha ajira kwa wengi, since manpower haiitajiki tena utaona kwamba mchango wa hawa wachache haupo tena (no more trickle down effect - it does not trickle any more)
Inasikitisha sana huko tunakoelekea ni kubaya na sijui suluhisho la haya yote ni lipi?
 
Watu washahama kwenye ajira wengi tumekuwa wajasiriamali. Je! Napo pia watu watahama kwenye huu ujasiriamali? Na kama wakihama watahamia kwenye shughuli gani?? Maana kila zama na nyakati zake.
Nafikiri watu watarejea serikalini km zilivyo nchi zilizoendelea huko tuendako government itarejesha umiliki kuliko watu binafsi
 
Inasikitisha sana huko tunakoelekea ni kubaya na sijui suluhisho la haya yote ni lipi?
Clan can not defeat empires..., Ni either masikini wengi waendelee kuwachukia matajiri wachache na mwisho wa siku kuwanyangaya vilivyo vyao... AU

Masikini hao wachache waungani kwa kuunganisha nguvu zao (cooperation) na waweze kushindana kwa kuunganisha nguvu zao na kuwa kama kitu kimoja.... AU

Matajiri wachache wajue kula na vipofu wao waendelee kula vinono lakini wasisahau kuwatupia makombo masikini waliowazunguna....

Anyway it will get worse before it gets better; lakini mark my word the current system will not stay; mambo yamebadilika mahitaji ya nguvu kazi yamepungua na efficiency imeongezeka;
 
Kuna watu wameajiriwa lakini akili zao zinawaza biashara, hivo kuhusu mtaji na pesa za kujikimu kwenye hili kundi sio inshu sana kwao tofauti na sisi, sasa mimi huwa najiuliza huyu kuajiriwa lakini bado anataka afanye biashara yaani aje agawane wateja na sisi ambao hatuna shughuli rasmi zaidi ya huu ujasiriamali tunaougombania huku masokoni
Hawa sawa lakini sio ambao ni unemployed.
 
Inabidi turudi huko kwenye mifumo yetu ya zamani
Haswaa, tunapenda dezo.! Kilimo na ufugaji tumeachia wazee huko vijijini.

Leo nimetafuta maziwa ya ng'ombe mtaa mzima nimekosa, nimekaa chini nikatikisa kichwa in magufuli style nikajisemea ihiiiii, aah.!
 
Hiyo ni fursa ila ukianza kuuza wateja wakaielewa idea yako ukaanza kupata pesa watakuja watu wengine 3 kwenye mtaa huo huo mmoja na kuuza biashara kama yako
 
Kuna watu wameajiriwa lakini akili zao zinawaza biashara, hivo kuhusu mtaji na pesa za kujikimu kwenye hili kundi sio inshu sana kwao tofauti na sisi, sasa mimi huwa najiuliza huyu kuajiriwa lakini bado anataka afanye biashara yaani aje agawane wateja na sisi ambao hatuna shughuli rasmi zaidi ya huu ujasiriamali tunaougombania huku masokoni
Kwanini anataka afanye biashara ?
  • Ipo kwenye damu kwamba ndio hulka yake ?
  • Anachopata hakitoshi hence anatafuta zaidi kwa kubahatisha na huku ?
  • Anaokoteleza kwa kumpiga ganji muajiri; yaani kule kwenye kazi hafanyi kazi yake vizuri (100%) bali anatumia muda wa kule kufanya ya huku ?

In short watu wanafanya biashara ili iweje ? Ni hobby, waongeze kipato kiwe maradufu au ni kutafuta mkate wa kila siku ? Jibu la hapo utaona wengi ni kutafuta mkata ndio maana wengi stress haziwaashi na tabasamu usoni limekuwa thing of the past.. (mwendo wa kuhamisha madeni na kuongeza riba) Na kwa uhakika wa kwamba biashara ni ngumu na sio ya kila mtu angalia ni biashara ngapi zina-fail; Na shukuru Bongo hakuna ushindani zikija corporations hapa ni mwendo wa watu kufunga vibanda vyao na kuanza kulalamikia masuala ya Uzawa...
 
Hiyo ni fursa ila ukianza kuuza wateja wakaielewa idea yako ukaanza kupata pesa watakuja watu wengine 3 kwenye mtaa huo huo mmoja na kuuza biashara kama yako
Ukifanya biashara bongo yenye threat of new entrants ndogo hakikisha unafanya diversification hiyo biashara ikichochea. Biashara zina phase kuu nne ambazo ni kuanza, kukua, kustawi na ya mwisho ni kufifia. Ukiona biashara yako imefikia kwenye kustawi ujue inaelekea kufifia hasa kutokana na ushindani mpya unaodai hapa
 
Haswaa, tunapenda dezo.! Kilimo na ufugaji tumeachia wazee huko vijijini.

Leo nimetafuta maziwa ya ng'ombe mtaa mzima nimekosa, nimekaa chini nikatikisa kichwa in magufuli style nikajisemea ihiiiii, aah.!
Hao wanunuzi wa maziwa mtaani kwenu wapo kila siku au ni kama wewe kwa mwaka unatafuta mara moja ?; Na kama ni maziwa ya unga uwezo wao ni kununua kwa carton au kwa vijiko (tena sio vya chakula bali vya chai)
 
Back
Top Bottom