Je, nini kitatokea endapo serikali itapiga marufuku uagizaji wa magari binafsi ya kutembelea?

Je, nini kitatokea endapo serikali itapiga marufuku uagizaji wa magari binafsi ya kutembelea?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
1.) Je, ni shillingi za kiTanzania trillion ngapi hutumika na waTz kwa mwaka kuagiza magari ya kutembelea? Na je, baada ya zuio hilo matrillion hayo wanaweza kuyatumia kwenye nyanja ipi kama mbadala? Ujenzi au kilimo?

2.) Je, mikangafu inayoozea gereji juu ya mawe inaweza ikapanda thamani na kupata soko ghafla baada ya zuio? Gereji zinaweza kupata wateja wengi wa ghafla wanaotaka kuboresha magari yao ya zamani kwa kutumia pesa walizotaka kutumia kuagiza gari jipya? Je, kuna ajira mpya zinaweza kujitokeza za ufundi, je ni ngapi?

3.) Je, zuio hilo linaweza kuchagiza karakana ndogo ndogo za kuunganisha magari? Mfano kuunda body zenye design nzuri na kutumia engine , gear box , diff. used toka nje (Assembly) na kuyapa magari yao brand names zao na wakapata udhibitisho wa TBS na yakasajiliwa TRA na kupewa namba mpya kabisa kama magari mapya made in Tanzania?

4.) Je, zuio hilo linaweza kuchagiza uharakishwaji wa miradi ya usafiri ya umma kama BRT phase 2 -6?

5.) Je, hili linaweza kulazimisha uanzishwaji wa viwanda kamili vya magari nchini? Nini kitatokea endapo zuio hili likaja mapema zaidi kuliko ambavyo wanaweza kuwa wamepanga?
 
Mkuu kwa wanavopiga hela hao TRA sahau kuhusu hilo suala.

Wewe gari ununue kwa usd 3,000 ushuru unalipia 4M unadhani ni mapato kidogo hayo kwa TRA?
 
Mkuu kwa wanavopiga hela hao TRA sahau kuhusu hilo suala.

Wewe gari ununue kwa usd 3,000 ushuru unalipia 4M unadhani ni mapato kidogo hayo kwa TRA?
Nadhani basi wafanye kama ‘Scientific experiment’, yaani tuchague mwaka mahsusi wa kuendesha zoezi hili kwa majaribio kwa mwaka mzima, halafu tutanye critical analysis ya madhara yatakayotokea (faida na hasara), then tupime matokea hayo ili tuoate a way forward, maana kuna kitu hakiki sawa katika hii sekta ya magari , something is not right, yaani tunashindwa kujioenyeza kwenye hii auto industry licha ya kwamba tunamahitaji makubwa ya magari, some drastic measure needs to be taken.
 
Mkuu kwa wanavopiga hela hao TRA sahau kuhusu hilo suala.

Wewe gari ununue kwa usd 3,000 ushuru unalipia 4M unadhani ni mapato kidogo hayo kwa TRA?
Well, udodosaji huu unaweza kuwa unafanywa na hao hao unaowahofia, so kuwa na amani, tuko pamoja katika kutafuta ufumbuzi wa vizingiti vya maendeleo yetu.
 
Well, udodosaji huu unaweza kuwa unafanywa na hao hao unaowahofia, so kuwa na amani, tuko pamoja katika kutafuta ufumbuzi wa vizingiti vya maendeleo yetu.
Ni mawazo mazuri hasa kama tutachuku mpango wa ku assemble humu ndani kuongeza ajira kwa garage na mafundi.
 
Ni wazo zuri sana la kuinua uchumi wa nchi sema kwa ulemavu wa bongo zetu watanzania sahau hilo kutokea
 
Litazidi kudidimiza uchumi wetu.

Ni Moja ya wazo baya zaidi kutokea nchini Tanzania.

Sekta ya usafirishaji itapata shida mno, kumbuka Sekta hii inaliingizia pesa nyingi sana serikari.

Nchi kama Malawi, Rwanda na Zambia zitafaidika pakubwa kwa Makampuni Yao ya usafirishaji kuoperate nchini.

Ajira za madereva kuwa taabani hivyo kwenda kuvuruga uchumi wa mtu mmoja mmoja na familia.

Kupanda kwa gharama za usafirishaji hivyo kupanda kwa bei za bidhaa na huduma.

N.B kabla hujafikiria hilo jambo tajwa inabidi kwanza uhakikishe hivyo viwanda vya kuasemble vinaweza kukabiliana na mahitaji bila hivyo utaathiri na kutishia uhai na usalama wa Supply chain.
 
Nimesema magari binafsi ya kutembelea, unaelewa maana ya ‘gari ya kutembelea’? Au ulijua mabasi na magari ya mizigo?
 
Back
Top Bottom