Je, nipo sahihi kuacha uwalimu na kwenda kuwa Technician wa moja ya mitandao ya simu?

Je, nipo sahihi kuacha uwalimu na kwenda kuwa Technician wa moja ya mitandao ya simu?

kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2018
Posts
456
Reaction score
833
Habari wanajamii? Kama Uzi unavyojieleza, Toka 2018 nimekuwa mwalimu wa hiari WA somo la fizikia, kutokana na kukosa kazi ya taaluma niliyoisomea, nimesoma Bsc. Information systems, nilikua mnyonge sana Kwan private schools hata muda WA kwenda kwenye interview huupati.

Jana nimepigiwa simu kwenye Moja ya mitandao ya simu, wanahitaji Technician, sijui mshahara wao utakuwaje, japo mara kadhaa nimesikia Wana kiwango kidogo.

Ninawaza nifanye Nini, huku kwenye uwalimu nilifikia 900'000 kwa mwezi japo Bado ni mdogo, huku kwenye taaluma yangu naona walau nianze ukurasa mpya wa nilichokisomea kwani nilikua sioni miaka kadhaa mbele patakuwaje!

Asante.

Kijana wenu, ni katika harakati za kuyapambania maisha.
 
Kufanya choice ya jambo lolote ni muhim San katik kutafut mustakabali wa maisha yako.hapo ulipo unaonekan una-knowledge kubwa hvyo ningekuomb ujitathimin ww kwanz kihali,maisha na mamb mengn juu ya Hilo jambo kabla ya kufany maamuz japo kuishi nje ya matakwa yako ni saw na usiku wa kiza.nyakat za sas ningumu sana bro na pengine afadhali ya wew unakaz wengine sisi tuna elim lakin tupo tu mitaan
 
Ila walimu sijui kwa nini mna akili ndogo namna hii.
Yani unataka kuacha 900k kwa ajili ya kazi ambayo hujui unalipwa ngapi?
 
Ulikuwa ukilipwa laki 9 hujui kufundisha wanafunzi walikuwa hawakuelewi ndio maana mwajiri akaona huwezi kupandishwa

Walimu wote wazuri mfano shule za serikali huporwa na shule binafsi mishahara yao inaanzia milioni 3 kwenda juu

Na ukienda shule hizo nzuri wanafunzi huambiwa watoe ripoti kuhusu ufundishaji wa mwalimu anaeleweka au la

Wakisema hueleweki kwa heri na somo lako wakifeli wanafunzi kwa heri

Assessment ya mwalimu ni ufaulu wa wanafunzi na ikiwa kubwa anaporwa na shule binafsi wewe bwege mleta mada huuziki soko la ualimu afadhali umeenda huko usiendelee kudhalilisha fani ya ualimu kwa kushindwa kufundisha na kufelisha wanafunzi

Kuna walimu ni hot cake hugombaniwa kama mpira wa kona wengine wanalipwa hadi milioni sita kwa mwezi shule zinazofaulisha sana anapewa nyumba na gari bure

Unafundisha kama umelewa hueleweki wanafunzi hawakuhitaji hueleweki ukifundisha na mwajiri hakuelewi kwenda zako nenda hata ukawe hata boda boda bwege wewe
 
Baadhi ya watanzania hawajielewi kila kitu ni soko yaani makert ndio maana kuna job makert uwe ualimu au fani yeyote

Mwalimu ni moja ya kazi zenye soko kubwa mno ila unatakiwa kufanya kazi hasa sababu wazazi ,wenye shule huangalia matokeo ya somo unafundisha mitihani ya taifa

Watoto wamefunda D na F darasa zima nani akutake kwenye shule yake akulipe mshahara mkubwa?

Au wazazi wakupongeze kwa lipi kwa kufelisha watoto wao au?

Walimu wafaulishaji hata baadaye hufuatwa na wanafunzi waliowafundisha wakafika mbali kuwazawadia magari,nyumba nk

Lakiji kimwalimu kibwege unakuta kinasema mimi nafundisha basi tu nyoko si aache kazi aende akauze ubuyu huko hajielewi kwenye meza sokoni soko la ualimu anafanya nini hajielewi

Bidhaa yeyote ifanyayo vibaya sokoni hakuna anayeihitaji awe mwalimu au yeyote

Inategemea performance tu hata ualimu
 
Ila walimu sijui kwa nini mna akili ndogo namna hii.
Yani unataka kuacha 900k kwa ajili ya kazi ambayo hujui unalipwa ngapi?
Hujui walimu wanaishije kaka, mshahara hata wa 1M kwa shule za private Bado ni mdogo, utapigwa kazi Toka saa 11 mpka saa tatu usiku, hizo Hela zitabaki za kula tuu... Na wakati mwingine wakisikia una kitu unakifanya wanaanza kukupa zengwe kuwa kazi sahiv huithamini... Na kibaya zaidi stress za kazi muda wowote unaweza kusimamishwa kazi... Kwa mtu anaewaza sana lazima awaze 10years to come itakuwaje....

Hivyo kusema walimu wana fikra ndogo unakosea,
 
Habari wanajamii? Kama Uzi unavyojieleza, Toka 2018 nimekuwa mwalimu wa hiari WA somo la fizikia, kutokana na kukosa kazi ya taaluma niliyoisomea, nimesoma Bsc. Information systems, nilikua mnyonge sana Kwan private schools hata muda WA kwenda kwenye interview huupati.

Jana nimepigiwa simu kwenye Moja ya mitandao ya simu, wanahitaji Technician, sijui mshahara wao utakuwaje, japo mara kadhaa nimesikia Wana kiwango kidogo.

Ninawaza nifanye Nini, huku kwenye uwalimu nilifikia 900'000 kwa mwezi japo Bado ni mdogo, huku kwenye taaluma yangu naona walau nianze ukurasa mpya wa nilichokisomea kwani nilikua sioni miaka kadhaa mbele patakuwaje!

Asante.

Kijana wenu, ni katika harakati za kuyapambania maisha.
Athari za mawazo ya kijamaa hizi? Hapa watu wanaulizia vitu ambavyo walitakiwa wafanye maamuzi wao wenyewe kwani ni mambo binafsi kabisa.
 
Back
Top Bottom