Je, nipo sahihi kuacha uwalimu na kwenda kuwa Technician wa moja ya mitandao ya simu?

Je, nipo sahihi kuacha uwalimu na kwenda kuwa Technician wa moja ya mitandao ya simu?

Habari wanajamii? Kama Uzi unavyojieleza, Toka 2018 nimekuwa mwalimu wa hiari WA somo la fizikia, kutokana na kukosa kazi ya taaluma niliyoisomea, nimesoma Bsc. Information systems, nilikua mnyonge sana Kwan private schools hata muda WA kwenda kwenye interview huupati.

Jana nimepigiwa simu kwenye Moja ya mitandao ya simu, wanahitaji Technician, sijui mshahara wao utakuwaje, japo mara kadhaa nimesikia Wana kiwango kidogo.

Ninawaza nifanye Nini, huku kwenye uwalimu nilifikia 900'000 kwa mwezi japo Bado ni mdogo, huku kwenye taaluma yangu naona walau nianze ukurasa mpya wa nilichokisomea kwani nilikua sioni miaka kadhaa mbele patakuwaje!

Asante.

Kijana wenu, ni katika harakati za kuyapambania maisha.
Technician gani wa bachelor's degree au ulitumia cheti cha diploma ?
 
Ulikuwa ukilipwa laki 9 hujui kufundisha wanafunzi walikuwa hawakuelewi ndio maana mwajiri akaona huwezi kupandishwa

Walimu wote wazuri mfano shule za serikali huporwa na shule binafsi mishahara yao inaanzia milioni 3 kwenda juu

Na ukienda shule hizo nzuri wanafunzi huambiwa watoe ripoti kuhusu ufundishaji wa mwalimu anaeleweka au la

Wakisema hueleweki kwa heri na somo lako wakifeli wanafunzi kwa heri

Assessment ya mwalimu ni ufaulu wa wanafunzi na ikiwa kubwa anaporwa na shule binafsi wewe bwege mleta mada huuziki soko la ualimu afadhali umeenda huko usiendelee kudhalilisha fani ya ualimu kwa kushindwa kufundisha na kufelisha wanafunzi

Kuna walimu ni hot cake hugombaniwa kama mpira wa kona wengine wanalipwa hadi milioni sita kwa mwezi shule zinazofaulisha sana anapewa nyumba na gari bure

Unafundisha kama umelewa hueleweki wanafunzi hawakuhitaji hueleweki ukifundisha na mwajiri hakuelewi kwenda zako nenda hata ukawe hata boda boda bwege wewe
Hivi stress za Nini, halafu hata hujui hizo shule za private vizuri... Huu mwaka wangu wa 6 na ni miongoni mwa walimu ninao hama hizo shule unazoziita ni kubwa wewe, Tena hakuna kitu kibaya sana kama kuzihama hama shule.

Hizo Hela unazozisema ni za kipindi Cha kikwete, kwa wasomi wengi kuwa mtaani mwajiri kwa Sasa WA shule hzi hawezi kukupa above 1.5M, Tena hapo kwa masharti tayari ulishawahi kuingiza top 10 kitaifa, top 20 ndo hio unachezea 1M or Laki tisa wakupe nyumba ya kuishi na Hela ya usafiri.

Na vijana walivyo na njaa sahv ukileta ukinzani anakuja kijana anapiga mzigo kwa laki 5 na hasumbui kaz anapiga mpaka jumapili... So huzijui private za Leo!!!

6M hata feza hawalipi hivyo,
 
Habari wanajamii? Kama Uzi unavyojieleza, Toka 2018 nimekuwa mwalimu wa hiari WA somo la fizikia, kutokana na kukosa kazi ya taaluma niliyoisomea, nimesoma Bsc. Information systems, nilikua mnyonge sana Kwan private schools hata muda WA kwenda kwenye interview huupati.

Jana nimepigiwa simu kwenye Moja ya mitandao ya simu, wanahitaji Technician, sijui mshahara wao utakuwaje, japo mara kadhaa nimesikia Wana kiwango kidogo.

Ninawaza nifanye Nini, huku kwenye uwalimu nilifikia 900'000 kwa mwezi japo Bado ni mdogo, huku kwenye taaluma yangu naona walau nianze ukurasa mpya wa nilichokisomea kwani nilikua sioni miaka kadhaa mbele patakuwaje!

Asante.

Kijana wenu, ni katika harakati za kuyapambania maisha.
Mi nakushauri uende huko kwenye mitandao ya simu maana kuna career growth baada ya kupata uzoefu unaweza kubadilisha kazi na kupata kazi nzuri zaidi. Kwenye ualimu sioni career growth
 
Nenda kwenye Minara pamoja na changamoto za Job security ila kwenye Minara utapata Career Growth ambayo itakusaidia baadae Kuongeza thamani kwanza kwa iyo professional yako ukienda kwenye Makampuni na ukawa consistency unaweza kupata Career Growth nzuri ikakufikisha kwenye Managerial Positions
 
Ulizia hiyo kazi na usiulize mshahara tu ulizia benefits nyingine pia waweza shangaa mshahara mdogo ila marupurupu kibao.... Ikiwa hivyo nenda
 
Back
Top Bottom