Je, nipo sahihi kuacha uwalimu na kwenda kuwa Technician wa moja ya mitandao ya simu?

Technician gani wa bachelor's degree au ulitumia cheti cha diploma ?
 
Hivi stress za Nini, halafu hata hujui hizo shule za private vizuri... Huu mwaka wangu wa 6 na ni miongoni mwa walimu ninao hama hizo shule unazoziita ni kubwa wewe, Tena hakuna kitu kibaya sana kama kuzihama hama shule.

Hizo Hela unazozisema ni za kipindi Cha kikwete, kwa wasomi wengi kuwa mtaani mwajiri kwa Sasa WA shule hzi hawezi kukupa above 1.5M, Tena hapo kwa masharti tayari ulishawahi kuingiza top 10 kitaifa, top 20 ndo hio unachezea 1M or Laki tisa wakupe nyumba ya kuishi na Hela ya usafiri.

Na vijana walivyo na njaa sahv ukileta ukinzani anakuja kijana anapiga mzigo kwa laki 5 na hasumbui kaz anapiga mpaka jumapili... So huzijui private za Leo!!!

6M hata feza hawalipi hivyo,
 
Mi nakushauri uende huko kwenye mitandao ya simu maana kuna career growth baada ya kupata uzoefu unaweza kubadilisha kazi na kupata kazi nzuri zaidi. Kwenye ualimu sioni career growth
 
Nenda kwenye Minara pamoja na changamoto za Job security ila kwenye Minara utapata Career Growth ambayo itakusaidia baadae Kuongeza thamani kwanza kwa iyo professional yako ukienda kwenye Makampuni na ukawa consistency unaweza kupata Career Growth nzuri ikakufikisha kwenye Managerial Positions
 
Ulizia hiyo kazi na usiulize mshahara tu ulizia benefits nyingine pia waweza shangaa mshahara mdogo ila marupurupu kibao.... Ikiwa hivyo nenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…