Habari wana JF, ndugu zangu hapa ni jukwaa la kupeana michongo na kubadilishana mawazo.
Kuna jambo naombeni tusaidiane Mimi ni mwalimu na niko nje ya system I mean sijaajiriwa serikalini nafanya private school ila nina hitaki kufanya master degree kipi kinaweza kuwa sahihi kwangu.
1. Kusoma masters ambazo zinahusisha education. In case nimeajiriwa inaweza kunisaidia.
2. Kufanya master ambazo ziko nje ya ualimu. Kuhusu hii naombeni kuuliza hivi master degree unaweza kutumika as one of direct qualification for employment serikalini?
Nipeni mawazo ndugu zangu
Pole Sana mkuu!!
Unataka kuongeza elimu hiyo uliyonayo umeshaitumia vya kutosha na kufika kilele Cha mafanikio yake!!?
Kama ni serikalini huku masters Yako haihitajiki kama criteria ya ajira Wala cheo ni uzoefu kazini!!
Hakuna sehem utaiapply masters huku hata ukiwa afisa elimu hutoshindwa kusimamia elimu mkoani.au.wilayani kiss huna masters!!
USHAURI
USIENDE KUSOMA MASTERS COZ HIYO DEGREE BADO HAIJATUMIKA KWENYE KILELE CHAKE CHA MAFANIKIO!!
WAZA NAMNA YA KUWEKEZA KIUCHUMI KWA KIZAZI CHAKO CHA KWANZA HADI CHA NNE!!ACHANA NA UJINGA WA KUWA NA VYETI WAKATI AJIRA HAMNA KABISA MKUU!!!
NIPO JOB KWA GOVERNMENT KWA MIAKA KUMI SIJAONA DEGREE YANGU IMETUMIKA KATIKA KILELE.CHAKE!
EPUKANA NA MENTAL SLAVERY,WE HUONIW MAPROFESA WANAKIMBIA UPROF WAO WANAINGIA KWENYE SIASA AMBAKO KUNA HELA NA SIO HUKO KWENYE VITENGO VYAO!?
WAMEONA ELIMU YAO NI BURE HAINA MAANA BORA WAKAE NA MUSUKUMA NA KIBAJAJI AMBAO HATA MASTERS AU DEGREES HAWANA NA WANABISHANA KWA HOJA NA HAKUNA TOFAUTI KATI YA MSOMI NA ASIE MSOMI!!!
Pole sana mkuu nasikitika sana kuona kumbe hata hiyo Elimu yako unayojivunia hata wewe haijakusaidia kabisa na hujui unachokiandika . Pole sana ni huzuni mno kuwa na wasomi kariba yako.
Any way we jamaa kasome kwa maana kila mtu na njia yake ya mafanikio. Kama performance yako Undergraduate ni nzuri unayo possibility hata ya kufundisha vyuo vya kati hata vyuo vikuu kabisa. Wakati wewe unaenda kusoma ukirudi utakuta wenzako wana maisha yale yale yaani hata hampishani. Walimu wa Msingi na Sekondari 90% ni njaa tu hata ukidanganya vipi lakini wengi wao ni kampuni moja. Walau walimu wa vyuo shavu nyingi kule. Kasome mkuuuuuu
Mkuu undergraduate hafundishi chuo!!?
Vyuo kama ndala,Butimba wanaofundisha wote Wana masters mbona wanafundisha wengi TU Tena wenye degree!!?
Au wewe umekariri lazima uwe na masters ndio ufundishe chuo!!?wakufunzi wangapi Wana degree na wanafundisha vyuo!!?
Hasta vyuo vikuu wanachukuliwa wale wenye gpa Kali yaani wanabaki ndio wanakua kwenye presha za masters degree lakin sio vyuo vya kati hivi hasta ukiwa na Bachelor unafundisha!
Mbona washkaji zangu wengi Wana fundisha na hawana masters hai wahitimu was diploma na certificate mbona wanafundishwa na Bachelor degrees!!?
Masters ninao kibao na wamebaki pale pale na hakuna chochote kinachoendelea na ninao hapa !!!
ACHA kumdanganya aje awe disappointed!!