Je, Nitakuwa na kosa iwapo nitasajili kampuni yangu MIRINDA ?

Je, Nitakuwa na kosa iwapo nitasajili kampuni yangu MIRINDA ?

Ni vyote viwili
Nikupe mfano rahisi trademark ni ule mchoro wa maandishi ya coca cola mekundu/meupe na pia tradename ni neno coca cola

Au azam ule mchoro ni trademark na pia neno azam ni tradename
Shukhrani, kwahiyo usajili wake ni tofauti tofauti. Yaani inamaanisha walisajili neno CocaCola ( kama Tradename ) na wakasajili pia logo ya CocaCola ( Trademark )
 
Duuh, lakini mimi ninataka kulinda mzizi halisi wa jina "Mkaruka" nilitumie peke yangu, hapo itakuwaje ?
Ni ngumu kidogo kwa kampuni ndogo ila ukiwa na uwezo unazilipia zote unazizuia. Rejea mfano wangu wa ugomvi wa Azania na Bakhresa.

Au nikupe mfano wa Jamiiforums na hii domain ya dot com. Walivyoanzisha kikoa cha dot.co.tz walienda wakainunua domain ya tz ila hawaitumii. Ili kuzuia mtu mwingine asinunue na kuchanganya wateja.

Au njia rahisi ni kuifunga kwa kusajili kama brandname ili mtu hata akiita kampuni mkaruka hawezi kuingiza product kama zako kwa jina hilo
 
- Mirinda siyo kampuni bali ni Trademark ya PepsiCo, Je, nikisema nisajili kampuni yangu kwa jina Mirinda ni kosa kisheria ?

- Na je, kilichosajiliwa ni Neno MIRINDA au Logo yake au hakuna tofauti ?

Msaada wadau !!
Kampuni unayotaka kuianzisha kwa jina la MIRINDA itakuwa inajihusisha na biashara gani?
 
Ni ngumu kidogo kwa kampuni ndogo ila ukiwa na uwezo unazilipia zote unazizuia. Rejea mfano wangu wa ugomvi wa Azania na Bakhresa.

Au nikupe mfano wa Jamiiforums na hii domain ya dot com. Walivyoanzisha kikoa cha dot.co.tz walienda wakainunua domain ya tz ila hawaitumii. Ili kuzuia mtu mwingine asinunue na kuchanganya wateja.

Au njia rahisi ni kuifunga kwa kusajili kama brandname ili mtu hata akiita kampuni mkaruka hawezi kuingiza product kama zako kwa jina hilo
Hapa sasa umenifumbua macho mkuu, maana nataka kwanza niendeshe kampuni ya mfukoni mpaka angalau nifikishe mtaji wa 30M, ila nataka kulinda kwa hali na mali BRAND Name yangu maana nimehangaika sana kuibuni. Nataka iwe kama AZAM & CELLO. Kwahiyo hapa dawa yake nitasajili kama
- Brandname na
- Trademark ( Logo )

Naamini nitakuwa salama zaidi na mzizi wa Jina kwenye kulitumia kuanzia Kwenye jina la kampuni, Brandname, logo n.k
 
Back
Top Bottom