Je, Noah hakuwakusanya Wanyama kwenye Safina wakati wa gharika bali Enki ndiye aliyemkusanyia DNA za wanyama hao?

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,187
Kupitia Utafiti wa Zecharia Sitchin mwaka 1976 "The Earth Chronicles" juu ya maandishi ya 14 tablets yaliyoandikwa na Mfalme wa Sumeria (Mesopotamia), Enki (miungu ya Annunaki); unaonyesha kuwa, baada ya miungu ya Annunaki waliotoka Sayari ya Nibiru kuzaa na wanadamu waliowaumba purposely kuchimba dhahabu ya kuijenga Nibiru, ilipelekea ongezeko kubwa la wanadamu kuliko idadi ya miungu ya Annunaki iliyohamia duniani, hali iliyowaudhi Annunaki na hivyo Mfalme wao aishie Nibiru, Ani aliamuru kuletwa gharika ili kufutilia mbali uso wa wanadamu na Annunaki waliotamani kubaki duniani.
Hata hivyo, Enki, Ali muamuru kwa siri Noah atengeneze Safina kwa kuwa, gharika ilikuwa njiani. Enki alimuandalia DNAs za wanyama na viumbe wote ndani ya kibox na kumpelekea Noah. Gharika ilipokuja iliteketeza viumbe karibia vyote (but siyo vyote) duniani. Baada ya gharika Kamanda wa Duniani alikasirika sana hadi kutaka kumuua Enki, alipogundua kuwa Enki ndiye aliyeokoa uzao wa mwanadamu (Noah) usiangamie kwa gharika. Hata hivyo alieleweshwa na Enki so akaridhia.

 
Last edited:
Mkuu nilifikiri utnapishtim sio noah ndie aliyetonywa kuhusu mpango wa dunia kuletewa gharika tena hyo siri alivujishiwa na mmoja wa hao miungu mwisho wa siku utnapishtim alipona yye na familia yake kinachonishangaza ukisikia story hii inafanana kila kitu na Nuhu maana huyu naye walipona 8 tu hata ukubwa wa boti,muda iliotumika kujengwa na muda wa gharika vinafanana sana alafu kinachoshangaza tablet hizi ziliandikwa miaka zaidi ya 2000 kabla ya Nuhu kuzaliwa sasa najiuliza huu mfanano vipi au kuna copy and paste zinahusika kati ya mmoja wao

Cc Malcom Lumumba Wick Elungata Kipanga boy
 
 
ndugu yangu hiko kitabu bora uachane nacho maana hata kuelewaka hakieleweki na muelezeaji nae kujenga hoja sijui ni bado?
Basi tu-assume kitabu hicho kinanipotosha. Hebu na wewe na akili yako, niambie hivi leo hii tukiamua kujenga Safina ya kutosha wanyama wote dunia ni wawili wawili, itakuwa na ukubwa gani? Una uhakika kuwa, wanyama wote waishio duniani kwa sasa walikuwa wakiishi Middle East? Je, Noah angekuwa na uwezo wa kuwakusanya kwa urais wanyama hao? Je, Chombo hicho kilikuwa really strong na chenye uwezo wa kuwahifadhi wanyama wote na ndege wote tuwajuao duniani?
Linganisha Safina iliyokuwa na urefu wa mita zipatazo 150 dhidi ya Meli kubwa duniani zinazofikia hadi mita 400.

 
Ukuu angali mavitabu mengine yana mikosi mikosi,eti mungu Mani kazaa na mwanadamu,Punda mwenyewe hawezi kuzaa na mwanadamu iweje miungu?
 
Hizo ni story tu. Bible ni kitabu cha Mungu. Hizo tablets sijui ziliandikwa miaka 2000 ni mapotoshaji. Ukiitaja miungu maana yake kuna mungu na Mungu.
Wote tuseme ameen!!
 
Enki kamshauri Noah ajenge Booonge la jahazi halafu kampa DNA za wanyama kwenye kibox! akili gani hizi? Halafu baada ya hapo Noah aliumba wanyama kupitia hizo DNA?au Enki alikifata kibox chake cha DNA ili aumbe wanyama?
 
Last edited:
Mbona me huyu jamaa namuelewa sana....ila wote hatuwezi kua sawa
 
Enki kamshauri Noah ajenge Booonge la jahazi halafu kampa DNA za wanyama kwenye kibox! akili gani hizi? Halafu baada ya hapo Noah aliumba wanyama kupitia hizo DNA?au Enki alikifata kibox chake cha DNA ili aumbe wanyama?
[emoji23] [emoji23] haya mambo haya
 
Ukuu angali mavitabu mengine yana mikosi mikosi,eti mungu Mani kazaa na mwanadamu,Punda mwenyewe hawezi kuzaa na mwanadamu iweje miungu?
Je, mchawi anaingiaje ndani ya nyumba wakati umefunga mlango? Hapa Dar es Salaam inadaiwa licha ya joto lililopo ni kosa kubwa kwa mwanamke kulala uchi. In fact hata mwanaume naye hatakiwi kulala uchi, Y?
Uwezo wetu wanadamu wa kufikiri unapoishia, ndipo ukweli wa jambo hilo pia unapoishia although the reality of it is not affected by our intuition coz reality is always free of our merely imaginations.
So, jambo ambalo leo hii ni uongo kesho linaweza kuwa kweli kwa malimwengu. Hata hivyo, mawazo haya complex huwa yanaanzishwa na vichwa ngumu na ma-genius tu na sometimes huchukua muda mrefu watu kukubaliana na ukweli huo.
Wakati Theory za Geography kama: Continental Drift, Isostacy na Plate Tectonics, zinaanza kuongelewa Karne za nyuma zilipingwa sana mpaka zilipokubaliwa hasa Karne ya 20. Fikiria wazo la Dunia kuizunguka Jua lilikataliwa na Viongozi wa Dini walikuwa wakidai sisi wanadamu Mungu ametuumba na kutupa mwanga wa kutuangazia kwa hiyo Mwezi, Jua na Nyota, vinamtumikia mwanadamu. Leo hii ukifuatilia ukubwa wa Milk Way Galaxy ambamo ndo Solar System yetu ilimo, kamwe huwezi ukadai tena we are all alone in the Universe. Ajabu ni kuwa licha ya Galaxy yetu hiyo kuwa na mabilioni ya Nyota (jua), bado hiyo Galaxy ni ndogo kwa Universe kuliko hata tone la maji ndani ya maji yote ya bahari duniani, kwani Universe ina matilioni ya Galaxies (nimesema galaxies, sijasema nyota hapo, wala sijagusia sayari kama zetu) - think, think, think... Probably we are not alone... time!!!
 
Last edited:
Hizi habari nyingine zina ajenda gani??
 
Hizi habari nyingine zina ajenda gani??
Ndugu usiwe skeptical bila sababu, tujadili ajenda iliyo mezani. Elimu haina mwisho. Mi nakwambia leo hii haya mambo yanaweza yakaonekana upuuzi but kesho tunaweza kuongelea stori nyingine.
Zamani kidogo, tuliaminishwa kuwa, kanuni za masomo ya sayansi, hazibadiliki kama masomo ya Arts. Hata hivyo, baadaye ikaonekana hata kwenye Biolojia, baadhi ya Kanuni zake zimekuwa zikibadilika badilika. Leo hii kuna watu wanahoji Theory mama ya Physics - Gravity. Fikiria jinsi itakavyoathiri elimu endapo itaonekana kuwa theories nyingi za Sayansi hasa zilizoko Physics na Geography, zilikuwa ni hoax.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…