Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Baada ya tetemeko kuikumba mikoa kadhaa ya kanda ziwa,nimeanza kujiuliza kama kumilki nyumba bado ni asset ya kuaminika kama tulivyozoea.
Ni kawaida kusikia mtu anasema ukitaka kuwekeza na hela yako isipotee kirahisi,wekeza katika majengo na wala si vyombo vya moto au kitu kingine chochote.
Sometimes ni bora hata chombo cha moto unaweza kukikarabati kwa gharama ndogo na kikatengamaa kuliko hekalu lililoporomoka kutokana na tetemeko.
Baada ya tukio hili la tetemeko, nimeamini asset ni ile tu iliyowekewa bima na hata kama una jumba lako lakini halina bima, basi ujue unajidanganya tu maana moto nao hauwezi kukuacha salama.
Nasema hivi kwasababu naamini inawezekana zaidi ya asilimia 97 ya nyumba zilizobomoka hazikuwa na bima yoyote ikiwemo bima ya moto na wengi wao waliamini wameshajikomboa kimaisha kwa kumiliki nyumba bila kujali ni ya ukubwa gani ili mradi tu ana nyumba.
Tukio hili liwe funzo kwa watu kuwekea bima mali zao zikiwemo nyumba zao.
===========
Maoni ya WanaJF kuhusu mjadala huu yamesomwa pia kwenye kipindi cha JAMII LEO