Je, Ole Sabaya alipewa kibali na Magufuli kuhujumu uchumi?

Kwahiyo hata mtu akioa mke halafu huyo mke akawa na tabia za ajabu, hizo tabia zitahusishwa na Mwanamme Alie muoa?
Ni tofauti! Yule alifanya kila kitu kwa jina la mtukufu! Wale enzi ya awamu iliyo pitwa, walikuwa wanajiita ma-rais wa wilaya!
 
Huyo Sabaya kiburi chote alichokuwa nacho kilikuwa na "full blessings" za mwendazake.

Yeye alidhani kuwa mwendazake ataishi milele!

Kwa hiyo hakuwasikiliza wote waliomuonya na kumwambia kuwa mwendazake hakuwa Mungu, lakini hakusikia.

Ngoja sasa jela ya Kisongo imfundishe adabu
 
Atashindishwa sio ataahinda kwa ukweli !!! Period wataifuta....kutoa ngoma juani
 
Swali: Je, Ole Sabaya alipewa kibali na Magufuli kuhujumu uchumi?
Mjasiriamali Magufuli alikuwa mwekezaji mkubwa sana...aliwekeza serikalini, kila Wilaya, kila Mkoa, kila taasisi na kila shirika la Umma na kuzimiliki kwa asilimia 100%.

Hakuridhika na hilo Mjasisiriamali Magufuli aliwekeza hadi kwenye mihimili kama Bunge na Mahakama kwa asilimia 100%

Mjasiriamali Magufuli alikuwa mbinafsi, aliwekeza na kuzibinafsisha Katiba, sheria, kanuni na taratibu na kuzimiliki kwa asilimia 100%.

Matokeo yake mjasiriamali Magufuli akajimilikisha uchumi wa Tanzania kwa asilimia 100%, akajimilikisha matumaini ya Watanzania kwa asilimia 100% na kujimilikisha uhai wa Watanzania kwa asilimia 100%.

Ili afanikiwe ikabidi aue harakati za kisiasa, aue harakati za kiuchumi, aue harakati za kibiashara na aue harakati za wananchi kudai haki, uhuru na usawa.

Lakini Mjasiriamali Magufuli alipoamua kuwekeza katika ujenzi wa mnara kama wa Babeli, hilo likawa kosa lisilovumilika...akapigwa stop na mnara ukaporomoka.
 
Sabaya ni kijana wa kazi wa mwendazake alikuwa anapiga kazi chafu ambazo lazima zilikuwa zifanywe😂🤸🐒
 
Kwahiyo hata mtu akioa mke halafu huyo mke akawa na tabia za ajabu, hizo tabia zitahusishwa na Mwanamme Alie muoa?
Kama unaambiwa mkeo anatesa watoto wa kambo,anatukana wazazi wako.ameonekana anachepuka ukakaa kimya bila kuchukua hatua.
Jibu ndio anahusika
 
Hii kesi Ole Sabaya ATASHINDA!
Labda ashindwe njaa! Umemsikiliza mkimbiza mwenge kwa like alichokiona kwenye ujenzi wa dispensary ya kijiji?
Yaani hiyo kesi imeelemezwa takukuru Tena wachunguze ni kwanini fedha za ujenzi zilizochangiwa na vyama vya ushirika zitunzwe kwenye account ya sabaya na wakusanya pesa wawe na wale mabaunsa wake wawili ambao siyo waajiriwa wa serikali? Yaani alipiga zaidi ya tshs 300m! Hachomoi !
 
Time will tell.
 
Kwa maoni yangu. Utawala wa magufuli na safu nzima ya wateule wake haikuwa kwa bahati mbaya hata kidogo tangu alipoingia madarakani tukumbuke alitumia muda kiasi kuteua baraza lake la mawaziri hiyo nayo ilikuwa na sababu zake kwa kuwa alifahamu mfumo wa utawala anaokwenda kuutumia ambao unatambulika kama no nonses type of a regime ndiyo maana alianza haraka sana na kutumbua bila kujali mahali mazingira ushauri wala kufuata utaratibu wa mifumo iliyokuwa imezoeleka ya kupelekwa kwenye kamati tume na vitu kama hivyo kwa muda mfupi sana alishafukuza watu kazi tena hakuwa na utaratibubwa kusimamisha kupisha uchunguzi kwa hivyo akawa tayari ameshawafanya watendaji wote wa umma kuwa ni watu wa ndiyo mzee wasiyotambua kesho kutatokea nini. Baada ya kulikamilisha hili ambalo kwake lilikuwa muhimu sana kwa sababu hadi hapa bado alikuwa katika maandalizi ya mfumo akaingia kupangua muhimili wa mahakama na kuufanya nao pia utende kama alivyotaka yeye kwa kuteua watendaji aliowataka na hilo alifanikiwa bado maandalizi hayakuwa yamekamilika akaingia bungeni akamleta mwanasheria mkuu, akamteua Dr tulia aingie bungeni kisha akampachika unaibu speaker na kujenga urafiki mkubwa na ndugai hakuishia hapo akamleta palamagamba kabudi bungeni na kumteua waziri wa sheria na katiba. Hapo akawa amekamilisha safu yake ya kuutawala muhimili wa bunge na ghafla sheria za kushtukiza zikaanza kutungwa kama za habari, takwimu na nyingine nyingi. Hapo akawa amemaliza uumbaji sasa akaanza utekelezaji kwa kuhamisha wizara nyeti katika ofisi yake mwenyewe hivyo kufanya baadhi ya mambo kujulikana asubuhi kuwa kuna hiki kitafanyika kuna kile kimeamuliwa hiki hakifai kukuza huyu weka ndani wale na wasababu alikuwa ameshaunda mfumonwake yote haya yakawa rahisi sana kwake mihimili yote mitatu iko mikononi mwake lakini bado hapo kulikuwa na tatizo kwa sababu kwenye msafara wa mamba kenge pia wapo kwa hivyo hakukuosekana walioanza kumpinga ikiwa ni pamoja na hata viongozi waliomtangulia hakusita kuwajibu kiurahisi tu tu kuwa walimsikia lini Obama akimshutumu au kumuingilia trump baada ya kustaaf wazee wa watu ikabidi watulize ngoma chini maana waliona kuwa kwao imeshakuwa ngoma ya watoto ambayo huwa haikeshi hapo akapavuka akaingia sehemu hatari zaidi kwa kuteua wimbi la wakuu wa mikoa na wilaya wengi wao vijana waliokuwa na sifa ya kufanya tukio fulani la kihalifu ambalo kwake aliona ndiyo kigezo na dalili ya uzalendo wengi wao walitokea kwenye umoja wa vijana wa CCM mfano Makonda aliteuliwa kwa kumshughulikia mzee warioba aliyekuwa kinara wa katiba mpya ambayo ingepatikana ingemshinda kuongoza kwa mfumo alioutaka,sabaya naye akatunukiwa u DC kwa kughushi kitambulisho akiwa diwani arumeru akijifanya ni afisa usalama wa taifa ili awapchunguze vizuri wapinzani maana kanda ya kaskazini kwake ilikuwa haimpi usingizi kabisa, kijana ally hapi nae akateuliwa kwa kufanikiwa kuwasambaratisha wapinzani katika chaguzi kinondoni, mbeya hakukuwa salama upinzani ulikuwa moto chalamila akaletwa kutoka kusikojulikana kwenda kumaliza hiyo kazi. Vikaundwa vikosi kazi visivyojulikana ambavyo vilitumika kuwapoteza waliompinga na kuwafuta kabisa katika uso wa dunia vikapewa jina la watu wasiojulikana shuhuda za miili kuokotwa fukweni ikiwa kwenye sandarusi kupotea kwa akina ben saa nane, Azory gwanda, na kunusurika kuuwawa kwa tundu lissu achilia mbali utekaji nyara na mambo kama hayo hayakuwa mageni tena kwenye mfumo ule. Sasa turudi kwenye hoja hawa wateule ambao sifa zao za kuteuliwa ilikuwa nilazima wawe wamefanya tukio fulani na wakawa wanakiri hadharani kuwa ni amri kutoka juu hawakuwa na sababu tena ya kuwa na hofu ya ubinadamu wala Mungu kwa sababu walishajipatia Mungu mtu hapa duniani wakabweteka wakapigiana simu wakati wowote na wakaambiwa chapeni kazi na wakachaka kazi kweli kilichokuja kuporomosha ukuta huu wa babeli ni kifo cha mungu mtu na hapo ndipo mawe sasa yameanza kupaza sauti.AKINA SABAYA WAMEJAAA KWENYE MFUMO ALIOUACHA MAGUFULI wapo ambao watajibanza lakini watabainika siku si nyingi na kosa kubwa la sabaya ni uropokaji kama alivyoropoka Albert chalamila juzi. Sabaya alinukuliwa katika mahojiano na kituo fulani cha luninga akisema kuwa alikuwa anawajibika kwa raisi, makamu wa rais. Waziri mkuu na mkuu wake wa mkoa sasa unaweza kuona Rais samia kumuachia tu pale angejitumbukiza katika mfumo niliouchambua hapo juu ikabidi amtoe sadaka na kazi iendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…