Je, online betting inaweza kuwa chanzo cha kipato?

daxy Jr

Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
88
Reaction score
307
Kubashiri mtandaoni kwenye tovuti au Apps kama vile Sokabet kunaweza kuwa chanzo cha mapato, lakini ni muhimu kutambua kwamba si njia ya uhakika ya kupata pesa. Ingawa baadhi ya watu wamefanikiwa kupata faida mara kwa mara kwa kubashiri mtandaoni, wengine wanaweza kuishia kupoteza pesa kwa muda mrefu.

Ili kuongeza nafasi zako za kupata pesa kwa kubashiri mtandaoni, ni muhimu kuichukulia kama shughuli nzito na kuwekeza muda katika kujifunza mikakati na mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wabetiji waliofanikiwa. Hii ni pamoja na kuelewa michezo na mechi unazobetia!

Ni muhimu pia kubashiri kwa wajibu na epuka kubetia pesa nyingi kuliko unayoweza kumudu kupoteza.

Kumbuka, betting inapaswa kutazamwa kama aina ya burudani na sio chanzo cha uhakika cha mapato.

beeeeet.jpg
 
Long term hakuna anayeweza kutengeneza pesa kwa Kubashiri sababu kimahesabu odds zipo against you...

Unaweza kutengeneza pesa ukiwa Bookies au kwa kuuza odds tofauti na hapo The House Always Wins...

Hata leo ukigundua system fulani ya kula pesa baada ya muda bookies wataziba hio loophole

Nikupe mfano kama Timu yenye kawaida ya kushinda mechi tuseme kwa bookies kwa kulijua hili huwa inaipa hii timu odds ndogo tuseme 1.2 au chini ya hapo; tuseme unaweka tshs 100 kwenye kila game ya hii timu yaani kwenye Tshs 100 yako faida Tshs 20/= Na hapo Sijaweka Kodi....., Sasa basi ukiweka mara kumi utakuwa na faida ya Tshs 200/= (hapo bookies wanajua hilo na kwa kulijua hilo huenda wanajua hii timu kwenye kila mechi 10 wanashinda 9 kwahio mechi ya 11 utapoteza hio Tshs 100/=) kwahio badala ya kukupa odds fair kutokana na probability wanaweza wakakupa odds za 1.05 average ili kwenye hizo mechi kumi utakuwa umeshinda Tshs 50/= na ukipoteza hio moja kutokana na probability na law of average na previous happenstances unajikuta not back to square one, but you are on the red....

Moral of the Story you have a Raw Deal......
 
Ni biashara kwa wengine
Kwa wengine ni mchezo, ila mchezo gani wa kupoteza pesa?
Si kupoteza tu, na kupata pia. Hapa unasema tu itatokea penati katika mechi. Isipotokea unapoteza afu tano yako, ikitokea unapata afu ishirini na tano. Hiyo afu ishirini na tano, tano nazirudisha pembeni, ishirini zinatumika kwenye mikeka mingine, tunaita kumkaanga papa kwa mafuta yake, yaani natumia faida iliyopatikana kutafutia faida nyingine

1678624422764.png
 
Long term hakuna anayeweza kutengeneza pesa kwa Kubashiri sababu kimahesabu odds zipo against you...

Unaweza kutengeneza pesa ukiwa Bookies au kwa kuuza odds tofauti na hapo In the House Always Wins...

Hata leo ukigundua system fulani ya kula pesa baada ya muda bookies wataziba hio loophole

Nikupe mfano kama Timu yenye kawaida ya kushinda mechi tuseme kwa bookies kwa kulijua hili huwa inaipa hii timu odds ndogo tuseme 1.2 au chini ya hapo; tuseme unaweka tshs 100 kwenye kila game ya hii timu yaani kwenye Tshs 100 yako faida Tshs 20/= Na hapo Sijaweka Kodi....., Sasa basi ukiweka mara kumi utakuwa na faida ya Tshs 200/= (hapo bookies wanajua hilo na kwa kulijua hilo huenda wanajua hii timu kwenye kila mechi 10 wanashinda 9 kwahio mechi ya 11 utapoteza hio Tshs 100/=) kwahio badala ya kukupa odds fair kutokana na probability wanaweza wakakupa odds za 1.05 average ili kwenye hizo mechi kumi utakuwa umeshinda Tshs 50/= na ukipoteza hio moja kutokana na probability na law of average na previous happenstances unajikuta not back to square one, but you are on the red....

Moral of the Story you have a Raw Deal......
Najua tumekuelewa sisi wachache, Bookies ni noma
 
Si kupoteza tu, na kupata pia. Hapa unasema tu itatokea penati katika mechi. Isipotokea unapoteza afu tano yako, ikitokea unapata afu ishirini na tano. Hiyo afu ishirini na tano, tano nazirudisha pembeni, ishirini zinatumika kwenye mikeka mingine, tunaita kumkaanga papa kwa mafuta yake, yaani natumia faida iliyopatikana kutafutia faida nyingine
Tuje hapo kwenye kutokea; kwahio ukipatia unapata mara nne faida yaani elfu tano yako uliyoweka na ishirini uliyopewa....

Sasa ukifanya mahesabu na kuangalia happenstances na probability unaweza kuona uwezekano wa kutokea penati (hapa nafanya assumptions) inaweza ikawa penati moja kila baada ya mechi kumi au zaidi...., kwahio katika kila michezo kumi ambayo utakuwa umeweka kama elfu hamsini uwezekano mkubwa ni kupata 25k hence kupoteza na ukisema uchague game ambalo uwezekano ni mkubwa zaidi wa penalty odds zitapungua zaidi....

In short wewe unajua game mchezeshaji anajua pia game ila yeye hesabu zinamlinda.....
 
... inaweza ikawa penati moja kila baada ya mechi kumi au zaidi...., kwahio katika kila michezo kumi ambayo utakuwa umeweka kama elfu hamsini uwezekano mkubwa ni kupata 25k
Jana pekee zilitokea penati kibao. Sema niliingia tamaa mechi ya Liverpool, nikasema penalti plus Mo Salah kufunga, ikawa penati lakini Mo Salah hakufunga, nikapoteza. Lakini mechi za penati huwa nazijua, hata za red card. Ukitaka tips nitakupa, ila kwa kuanzia PSG ikicheza it's likely kuwepo kwa penati, na ligi ya serie A it's likely kuwepo kwa red card. Tulishausoma mchezo usifikiri tunaweka kila mechi

1678611749874.png
 
Aisee kwahio wewe peke yako ndio unajua mechi za penalty na red cards ?!!!!

Ndio maana nikakwambia odds zinaendana na probability lakini pamoja na hayo wewe ukishinda unapewa kidogo kuliko wewe ukipoteza unachowapa kwahio in the long run everything being equal lazima utapoteza tu..., Its nature of the game..., Hata ukishinda trilioni leo unless uache ila baada ya miaka kadhaa utajikuta umewapa trillioni na nusu; unless unafanya kama leisure na sio biashara au unauza odds hence ukishinda au kushindwa bado unashinda
 
Uzuri ni kwamba hakuna anayemlazimisha mwingine
 
Kiukweli mie niipinga San hyo betting mie ni mmoja wa waasilika walio bet Kwa muda mrefu ila nimekua wa kumchangia mhindi t ambpo sometime nakula lakini nikija kuliwa naliwa zaidi ya ile pesa niliyokula Mimi Kwa hyo niwizi mkubwa bila kujua
 
hapa unaongea kinyume
Ngoja nikupe mfano wa kueleweka kidogo ukirusha shilingi outcome ya kutokea head or tail mara nyingi sana uwezekano ni nusu kwa nusu..., sasa hapo ukienda kwa bokies badala ya kukupa odds za even money (2) atakupa hata 1.95 au 1.81 hivyo kwa wewe utaalamu wako wa kusoma michezo na wao utalaamu pamoja na kwamba hii kitu ni unpredictable in the long run you will be found wanting....

Kwahio hata hizo penalty siongelei kwamba hazitokei kila siku duniani zinatokea ila issue zinatokea wapi ? chukua timu inayopata penalty nyingi zaidi kwa mwaka alafu imagine ulikuwa unaifuatilia hio timu unaweza kuona kwa kuifuatilia hio moja na zile odds ambazo ungekuwa unapewa kila game hata ukipatia mara tatu unaweza ukajikuta bado kwenye red....
 
Odds za penati sio kama hizo za 1.24 nk. Odds za penati ni 4.00, 5.00 hadi 6.00. Mfano mzuri ni huo niliouweka, ilikuwa 5. Mimi naenda kwenye odds kubwa kubwa zenye probability ndogo hivyo hivyo. Baadae nataka niweke mechi moja ya correct score yenye odds 67
 
Twende kwenye penalty hapo hapo na concentrate kwenye timu moja msimu huu imepata penalty ngapi unaweza ukakuta msimu mzima timu imepata penalty kama 7 sasa na sababu hii inapata sana unaweza ukakuta average odds zilikuwa 4 (tuseme una bahati umeopata zote saba hio ni 28 units) kwenye game 38 ukicheza zote ni 38 units ukicheza tuseme 20 ni 20 units sasa hapo room ya kufanya makosa ni kupatia zote saba ziwe within hizo 20 yaani 18 zote zisiondoke na uliyopatia....

Utasema kwamba huchagui timu moja unachagua huku na kule ila hapo ndio utaona probability ya kupatia inazidi kuwa ngumu.....

Utaona hapo in the long run lazima utapoteza tu hata kama leo upo vizuri jua soon or later kipigo ni inevitable (na makosa sio yako ni kwamba value unayopewa ni raw deal)
 
Mimi sideal na timu moja, sio kwamba leo nikiiwekea Madrid na kesho hivyo hivyo, no

1678624289842.png
 
Mimi sideal na timu moja, sio kwamba leo nikiiwekea Madrid na kesho hivyo hivyo, no
Naona bado hujanielewa anyway conversion rate yako ipoje katika penalties yaani ukichagua mara games kumi unashinda ngapi au ishirini unashinga ngapi wala sisemi kwamba unaweka accumulator yaani moja moja leo kesho wiki jana mwezi jana mpaka leo umeshagua penalties ngapi na umeshinda ngapi tuanzie hapo....

Na hapo nimeona unacheki zile games ambazo penalties ni kubwa hence kupewa odds mpaka za 3.6
 
Hamuwezi kuelewana kwasababu moja tu. Betting ni mchezo wa kubahatisha na katika maisha kuna watu wana asili ya bahati. Ni ngumu sana kukaa na kuwaza kuwa mechi ya Juventus na Sampdoria itakuwa na penati au kadi nyekundu hakuna namna unaweza kupiga hesabu kujua zaidi ya kubahatisha na anayeweza kupatia ni mwenye bahati.
 
Bahati sio 100 percent ukitabiri matokeo yenye uwezekano wa asilimia 90 kutokea ukapatia mara 8 kati ya kumi hio sio bahati ni trend ila ukifanya hivyo mara 1000 lazima utakosea hata mara moja....

Ukitabiri vitu vyenye uwezo wa kutokea asilimia 50 ukapatia nusu yake au mara nane katika kumi ndio unaweza ukawa na bahati kwa wakati huo (ila sababu zile nane unazopata hata ukikosea mbili bado hesabu zinakufunga wewe) sababu hata odds unazopewa sio fair (unapunjwa) ndio maana nikasema hata kwenye 50 chance games bookies anakupa pungufu ya odds ndio maana hata wachezeshaji Walikuwa wanaitwa bookmakers sababu walikuwa wanakula pesa inayobaki watu wakishaweka pesa zao kwenye matukio yaani hawa wanaoshinda huku wakishawalipa wale walioshindwa yeye bado anabakia na margins....

Ila kwa sasa wanakwenda tu na trend ambapo kila kitu kimekuwa accounted for (uwezekano, wangapi wame-bet, na ufahamu fika hata wakikupa leo umeshinda kesho utawarudishia na chenji) sababu huwezi ukawa na bahati kila siku.... (hata wao pia wana bahati)
 
Back
Top Bottom