Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Hii ndio inadhihirisha ni vipi Hesabu zinakupiga chenga..., Wengi ni wangapi ? Unajua ni wangapi wanacheza na wangapi mpaka leo wameshashinda ile top prize ?Maneno mengi ambayo ni pumba tupu mimi nimewashuhudia wengi tu waliopiga pesa hii Jackpot ya juzi kuna washkaji hapa kitaa wameshinda mechi 11 wakapata laki 7 na waliweka buku tu
Unajua inaweza ikawa rahisi kwa wewe kupigwa na radi mara mbili kuliko kushinda Jackpot top prize hao washikaji zako kitaa walishacheza mara ngapi na wameshinda mara ngapi na una washikaji wangapi ambao huenda wakacheza maisha yao yote na wasipate ? Unajua kwanini yule Mkenya aliyeshinda top prize alitangazwa kila Kona ? (ili wewe uone kwamba ni rahisi)
Kama kuna zawadi moja wakacheza watu trillioni moja akapata mmoja haimaanishi kwamba hakuna anayepata ila uwezekano wa huyo mmoja kuwa wewe ndio hapo tunapoongelea the odds being stack against you; By the way sidhani kama hao washikaji wako wanatumia jackpot kama njia ya kipato chao