Je, online betting inaweza kuwa chanzo cha kipato?

Mkuu jibu jepesi ni betting sio chanzo cha mapato.

Mambo yasiwe mengi.
 
Mwenyekiti kwa mamlaka niliyopewa kwa muda, nimefunga mjadala....🤔🤔
 
Acha kabisa huo mchezo mamaeeee Haufai...Nimepata Posho yang leo nlikuw nawaza namna ya ku Expand ili nifanye jambo fulan la haraka jamaa yangu akanishawishi nibet nilikataa katakata mana naskiaga watu wanaliwa mpk Ada za watoto..ye akanambia ananipa timu moja tu nisiweke nyingi..hyo moja uhakika..Akanipa ..KONYASPOR vs GALATASARAY....Alama 1.81 Tukaweka Mzigo..Half Time akamaliza Kashinda 0-1..Akasema umeona sas Bado Dk 45 UnatumiwA hapo kweny Application pesa yako..Nkamchukua Tukaend Kupasha koo kidg wakat tunasubir mechi iishe Online..Baad ya kunyw kunywa nawasha data nitazame nakuta...FT. KONYASPOR 2 v 1 GALATASARAY.. Njia zima Tumerud hatuja ongeleshana..Nimekuja Hpa Nakuta we unasema inaongeza kipatoooo!!!
 
Kwanini tusitatue hizo hesabu, siku zote bet against bookies tunaambiwa ndio solution ni sahihi mkuu!?
 
Nimekuelewa sana mkuu, hii hata katika baadhi ya biashara ipo sio betting tu
 
Ulistake kiasi gani mkuu
 
We jamaa utakua wa pori, betting inafaida kwa watu wenye akili zao timamu.. tamaa ni sumu kwenye betting
 
Kwanini tusitatue hizo hesabu, siku zote bet against bookies tunaambiwa ndio solution ni sahihi mkuu!?
Betting against Bookies / Betting against the public inaleta maana sababu kama wengi wanadhani Simba itashinda na Mbao FC watafungwa basi odds za mbao zitakuwa kubwa sana na kama utapatia kutakuwa na value....

Sasa issue ni kugundua hio value; ni kweli huenda kwa bahati Mbao akamfunga Simba na kama odds zilikuwa ni 5.6 hapo return yako kwa Tshs 100 ni 560/= (ila jiulize katika game 10 mbao atashinda ngapi) sababu akishinda moja ya pili na kushindwa nyingine tisa utakuwa umeacha ku-bet baada ya game ya pili au wewe utaanzia ya tatu mpaka ya 12 hence kupoteza Tshs 1000/=; Kwahio utaona hapo to be fair atleast odds zingekuwa 10 times

Ofcourse nilishafanya research paper trading kwenye goals overs / under na mimi ku-bet zenye value kubwa tu ofcourse kuna siku nilishinda kuna siku nilishindwa kidogo n.k. ila sikufuatilia sana sababu niliona kama vile mwisho wa siku ni kama even (sipati nyingi wala kuliwa nyingi nikiweka na muda wangu ikawa waste of time)
 
KATAA BETTING KWA HERUFI KUBWA
Wewe kila siku una bet

1. Ukilala usiku una bet sababu huna hakika kesho yake utaamka
2. Ukitoka kwende kwenye shughuli zako una bet pia
3. Ukioa na kuolewa una bet
4. Maisha yako karibia 90% ni kubet Tu
 
Wewe kila siku una bet

1. Ukilala usiku una bet sababu huna hakika kesho yake utaamka
Kwahio usilale ? !!! Kifo ni inevitable....,

Yaani sababu wewe utasikia njaa haimaanishi uache kula; kulala ni chakula cha akili na inakupa refreshment yaani kulala ndio kunakufanya uamke ukiwa recharged (after all usipolala odds za kufa ni 100%)
2. Ukitoka kwende kwenye shughuli zako una bet pia
Kwahio abaki kwenye shughuli zake; akitoka kwenye shughuli akapanda bodaboda mlevi, odds za kufa au kupata kilema ni kubwa kuliko kutumia usafiri mwingine.....
3. Ukioa na kuolewa una bet
Inategemea unatafuta nini kwenye hio ndoa kama ni short term good time huenda the end justifies the means
4. Maisha yako karibia 90% ni kubet Tu
at what odds ?

Kama unaishi kwa kutugemea utashinda sportspesa jackpot the odds are stuck against you; lakini kama una-take each day at a time while enjoying the ride you are in for a Winner
 
Watanzania siku hizi ni kama wamechanganyikiwa sana; sijui ni sababu ya umaskini au vipi. Wanatumia raslimali nyingi sana kwa kucheza kamali wakitegemea kupata hela ya haraka haraka na kuishia kuwa maskini zaidi. Ndiyo maana makampuni ya kamali yamekuwa lukuki, na wamiliki wa makampuni hayo wametajiriaka sana.
 
Nimepitia Hii Trending kwa uchache
Nikutulia siku moja nitaeleza uhalisia wa betting.
Kwa uchache tu...Kuna Useen power behind this company...unseen force.
Inatumia tamaa ya Binadamu maana always Binadamu anataa...hivyo hapo Kuna mwanya wa kwanza.
Kuna nguvu isiyo onekana nyuma ya hizi kampuni Kuna mikataba msiyo ijua Nyinyi.
Sasa Kuna stage1- 5 mpaka 6 za ulimwengu wa betting.
Stage 1 una bet unaliwa unaacha..
Hapa umeshawishiwa au umejishawishi mwenyewe...kwa nguvu usiyo iju ww.
Stage 2 unabet unaliwa unaacha Kisha unarudi Tena Baada ya maumivu ya kuliwa kuisha...unarudi Tena kuja kukomboa pesa zako.
Ulkipata pesa unarudi..na matumaini ya kushida unasahau kilicho chenga Hizo mechi bado kipo unarudi Tena kuja kushinda....sio Kama unavyowaza.
Stage 3 una bet unaliwa , unaliwa, unaliwa Tena na Tena ,na Tena ukija kupata unakuwa chambo ya kuleta wengne kwenye mchezo.
Huyu mtu kuacha Ni Hadi Maombi kasha wekwa kwenye mtungi wa kubet tu.
Stage 4 huyu pesa anayopata karibu Yote Anavutiwa kubet tu huyu Ni mtumwa Hawezi Toka Tena Ni lango la kupitisha pesa kwenda kwenye hizi kampuni! Ukishinda ww Ni member wao wamekuzawadia ili kuleta wafuasi wengi.
Stage 5. Official member/Mimiliki ..huyu ni member wa betting ' ni wahusika wa hizi kampuni wenyewe tayari yuko kwenye mkataba akikenguka tu kampuni yake inapigwa hasara na Hawezi acha hiyo biashara.
Stage 6. Kampuni kwa kampuni hizi kampuni waendesheji Kuna saa wanaviziana kwa Kuangaliana yaani
Kampuni A wanachunguza weakness za kampuni B.
Kisha A anaweka mzigo wa maana kupitia watendaji wake.
Hii kimjini inaitwa mbwa kala mbwa.
Sasa kampuni iliyo weak utakuta anachukua pea zenu, anachukua pesa za wanao bet. inaenda kulipa kampuni iliyo na nguvu zaidi.
....Haya Huwezi kuyaelewa kirahisi...Ni spiritual.
Tafuta Msaada wa Maombi ukiwa kwenye Stage 2 , au 3 Tena kuazia hiyo 3 ndio mbaya zaidi maana kila pesa lazima utoe fungu la kumi kwa wakuu wanao simamia bettingDarkpower.
Kuna mengi Sana Ila kwa Leo nishie Hapa.
 
Betting ni BAHATI NASIBU.

BAHATI NASIBU INATAFUTWA.

Nimeona watu wanabet na wanaishi hivyo, wako on the winning side, katika mara 10 atakula mara 7.

Nimeona watu wakiliwa kila siku,wako on the loosing side katika mara 10 atakula mara 2.

Usibet kile huwezi poteza.

Kama inakuathiri kiuchumi,kisaikolojia,kijamaa (Level ya addiction) ACHA MARA MOJA.

MWISHO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno mengi ambayo ni pumba tupu mimi nimewashuhudia wengi tu waliopiga pesa hii Jackpot ya juzi kuna washkaji hapa kitaa wameshinda mechi 11 wakapata laki 7 na waliweka buku tu
 
Niliwahi kumshuhudia mshkaji fainali ya uefa kati ya Chelsea na Manchester city jamaa akaweka laki 5 akampa chelsea akaipiga laki 8 faida
 
Niliwahi kumshuhudia mshkaji fainali ya uefa kati ya Chelsea na Manchester city jamaa akaweka laki 5 akampa chelsea akaipiga laki 8 faida
Uliza kama anaendelea kubet?? Ndo utajua why mtu apatr faida ya laki 5 alafu aache[emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…