NADHARIA Je, Paka kulia kama watoto wakati wa usiku inaweza kuashiria jambo baya?

NADHARIA Je, Paka kulia kama watoto wakati wa usiku inaweza kuashiria jambo baya?

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Wakuu hivi hali ya paka kulia usiku kama watoto wachanga huwa inasababishwa na nini maaana kuna muda huwa watu wanahusisha na imani potofu kamauchawi.
1790946713933.png
 
Tunachokijua
Kama ilivyo kwa viumbe vingine Paka hutumia mlio kuwasilisha hisia wanazokuwa nazo kwa wakati husika. Mbali na mlio wao wa kawaida huwa wanalia kama mtoto mdogo, mlio ambao umekuwa ukiwatisha wengi aidha uwe mmiliki wa paka huyo au paka tu wa mtaani.

Zimekuwepo imani mbalimbali zinazohusishwa na mlio huo kulingana na jamii husika. Mathalani kuna jamii zimeenda mbali na kuamini kuwa huenda Paka kufanya hivyo kunaweza kuashiria kifo.

Makala ya Petoska inaeleza kuwa, tafiti unaonyesha kuwa mlio wa paka mara nyingi huwa katika kiwango cha sauti kinachofanana na masafa ya kilio cha mtoto mchanga. Hali hii huwafanya watu kuvutiwa na sauti hiyo na kuitilia maanani bila hata kufikiria.

Paka wanaofugwa nyumbani hujifunza haraka kuwa sauti hizi huleta mwitikio kutoka kwa binadamu, kama vile kupewa chakula, kupewa uangalizi au kutulizwa. Hata paka wanaoishi mitaani hutumia milio hii kuwasiliana na binadamu wanaowazunguka.

Je, Paka kulia kama Paka inaweza kuwa ni ishara ya nini?

Paka anaweza kulia ili kutoa ishara kuwa;
  • Anakabiliwa na njaa
  • Hofu na msongo wa mawazo
  • Inaweza kuwa ni changamoto ya magonjwa kama vile maumivu.
  • Kutaka kumvutia mwenza (Kama ni wa kike anamvutia dume na kama wa kiume anamvutia jike)
  • Matatizo ya umri.
Je, unaweza kufanya nini ili kumzuia paka wako asilie kama mtoto.

Kutokana na sababu hizo inaelezwa kuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa paka wako anapata muda wa kutosha wa kulala, unazingatia afya yake na pia apate mlo kwa wakati.
Wanakua kwenye situation ya mating ndo maana wanalia hivyo na sio usiku hata mchana wakitaka kulombana tu huwa wanaanza kulia hivyo
Huwa inasemwaga ni uchuro mapaka yakaanza kulia kama yana dhulumiwa

Yakalia sana sana dirisha la JIRANI yangu yule mzee AKAFARIKI siku chache baadae
 
Duh.... ukisikia tu ng'aang'aaa....ng'aaa....
Nikuanza kuomba kimoyomoyo.

Unajua tayari wachawi wameanza... Hii mind set ndio nilikuwa nayo tangu utoto sijui ni mimi tu...
Ni kweli Mimi pia sipendii mapaka yakiwa yanalia hivyo

Mshana Jr

Tupe UZOEFU kaka mshana
 
Back
Top Bottom