mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Wakati waziri wa fedha anawasilisha bajeti ya serikali kwa mwaka 2022/2023 alipendekeza kama njia ya kubana matumizi kuwa mtu akitenguliwa kwenye nafasi ya uteuzi na akarudia nafasi yake ya awali, basi na mshahara utenguliwe ili apate unaolingana na nafasi aliyokuwa nayo kabla ya uteuzi. Kwa mfano mwalimu wa sekondari aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa halmashauri fulani, basi akitenguliwa kwenye ukurugenzi {bila kufukuzwa kazi) arudie mshahara wake wa ualimu.
Sasa swali langu ni kuwa je hii itawahusu pia ambao kwa sasa walishatengfuliwa na bado wanalipwa mishahara ya nafasi ambayo kwa sasa hawaitumikii, au hili pendekezo likipitishwa na bunge litawahusu tu wale watakaotenguliwa kuanzia 01/07/2023 na wale wa awali waendelee kufaidi mishahara ambayo kwa sasa hawaifanyii kazi?
Nimeuliza hivyo kwa sababu:
1. Kama hili pendekezo haliwahusu waliotenguliwa kabla ambao kusema kweli ni wengi mno, basi hili pendekezo halitaweza kuleta unafuu wa bajeti kwa sababu kasi ya kutengua kwa sasa ni ndogo sana ukilinganisha na huko nyuma.
2. Kama hili pendekezo linawahusu pia waliotenguliwa huko nyuma, kwanza ni kweli litaleta unafuu wa bajeti, lakini pia litafanya atakayetenguliwa sasa aridhike na asione ameonewa kupunguziwa mshahara. Maana wengine wako ofisi moja aliyetenguliwa mwanzo na atakayetenguliwa sasa.