Je pengo la samatta linazibika ?

RUKUKU BOY

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
1,516
Reaction score
1,775
Wakuu pole na stress za Korosho, kesho timu yetu ya taifa(Taifa stars) inashuka dimbani kukipiga na Lesotho. Lakini habari mbaya tutamkosa naodha mbwana Samatta.

Je pengo lake linazibika ? Tuangalie Takwimu.

Tanzania vs Lesotho(Dar es Salam) matokeo ilikuwa 1-1. goli là TZ lilifungwa na Samatta Kwa direct freeck.

Tanzania vs Uganda(kampala) matokeo 0-0.

Cape verde vs Tanzania matokeo 3-0

Tanzania vs cape verde(Dar) matokeo 2-0 . Samatta alifunga goli moja na kutoa bonge la assist.

Tanzania imefunga julma ya goli 3 uku 2 zikifungwa na Samatta.

Je kukosekana kwa samatta hakutaigalimu timu ?

Karibu tujadili.
 
Mechi kama hizi lazima mumtengeneze hero. Mtu kama Chilunda anapewa jukumu la kuibeba taifa, ndio ni team work lakini mtu mmoja anabebeshwa jukumu la mauaji kwa kila gharama. Hata akiwa uwanjani anajua jukumu lake na nchi yote ipo mgongoni kwake. Acheze kama vile ndio mechi yake ya mwisho! Hata asipofunga yeye lakini pressure yake itasaidia mengi.
 
Sasa ni kipindi ambacho wachezaji wa star wanatakiwa kuonesha kwamba kumbe bila hata samata wanaweza cheza mpira na kupata matokeo safi.Wakishindwa fanya hivyo nikuvunja team yote na kuanza ,hakuna maana ya kutegemea mchezaji mmoja tu
 
Chilunda ni mzuri kwenye kufunga, ila Bocco atapewa jukumu la kuongoza safu ya ushambuliaji. Ni mpiganaji na kiongozi mzuri.
Wakicheza pamoja kutakuwa na matokeo bora bila shaka
 
Duu sijakuelewa mkuu
 
Sasa ni kipindi ambacho wachezaji wa star wanatakiwa kuonesha kwamba kumbe bila hata samata wanaweza cheza mpira na kupata matokeo safi.Wakishindwa fanya hivyo nikuvunja team yote na kuanza ,hakuna maana ya kutegemea mchezaji mmoja tu
Ila Samata ni hatari huwezi mlinganisha na kina Chilunda au Boko
 
Mm uwa nashindwa kuelewa unaita mchezaji mzuri tena bwana mdogo kabisa kama chiluda afu unaishia kumpiga benchi kweli? hiv kocha anashindwa kumpa ata dakika thelathini tu? nasubili kesho hasimpange aone.
 
Anachezaga namba ngapi uyo dogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…