Je pesa ndiyo mtaji pekee katika mafanikio yetu?

Je pesa ndiyo mtaji pekee katika mafanikio yetu?

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
1,941
Reaction score
2,044
Hivi ni kweli pesa ndiyo mtaji pekee kwenye mafanikio yetu ya kibiashara.? Jibu ni HAPANA. Kama hauniamini acha kusoma nilichoandika huku chini maana utakuwa unapoteza tu muda wako. Kwa sababu kila jambo linaanza na imani. Kama unaamini tuendelee sasa.

Nianze kwa kusema kabla Mungu hajamuumba mwanadamu alianza kwa kutengeneza miundombinu itayomuwezesha mwanadamu kuishi kwa amani na furaha. Miundombinu hiyo ni pamoja na maji, wanyama wa kila aina, mimea na matunda yake ya kila aina, ardhi yenye madini na viumbe wa kila aina baharini. Bado Mungu hakuchoka, alipomaliza kumuumba mwanadamu kwa sura yake alimpa akili na uwezo wa kufikiri kuliko kiumbe yeyote duniani. Alimpa nguvu na mwili, alimpa ufanisi na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati muafaka. Hizo zote ni rasilimali za kumsaidia mwanadamu.

Dhambi ilipoingia duniani ndiyo ilisababisha rasilimali hizo kupoteza uwezo na nguvu zake za asili. Miundombinu mingine imekuwa adimu sana na kufanya watu waanza kudanganyana, kuuana na kuanza kuzurumiana. Kwa mantiki hiyo, pesa haikuumbwa peke yake lakini leo ndiyo kigezo cha mafanikio ya mahitaji pekee.

Ni makosa sana kuamini pesa ni kila kitu katika maisha yetu. Sikatai pesa sio muhimu, hapana. Ninachosema ni kuwa tutafute pesa lakini tusiabudu fedha kiasi cha kusahau kuwa kuna kufa. Tusifikiri pesa ndiyo mtaji pekee wa biashara au mafanikio! Hapana. Tumepewa vyanzo vingi ambavyo tunaweza kuvitumia kama mtaji baadala ya fedha. Siwezi kutaja vyote kwa sababu ni vingi na havina ukomo, ila nitajitahidi nitaje vichache.

> Una uzoefu na kazi gani: Kama kuna jambo ambalo umekuwa ukishughulika nalo kwa muda mrefu, basi unaweza kulitumia kama mtaji. Unaweza kuwa mshauri au mwalimu wa jambo hilo na kutoza gharama kidogo tu na utatengeneza kipato. Kwa mfano kama una uzoefu wa kutunza bustani ndogo ndogo za maua, basi unaweza kutumia uzoefu huo kukupatia kipato kwa kuelimisha wengine. Jambo la kuzingatia ni kuwa lazima uwe mahili kweli kweli katika jambo hilo.

> Wazo la mradi: Unajua kuna watu wana mkwanja lakini hawana wazo lolote la mradi na hawajui namna ya kuanzisha na kutengeneza mradi? Hiyo ni fursa na mtaji tosha kwako. Kama unao uwezo wa kuweka kumbukumbu sahihi na kuziweka katika maandishi kwa kufanya rejea za kutosha, unaweza kuandika pendekezo la mradi na kuliuza kwa wadau ili utengeneze kipato. Huhitaji pesa kuandika wazo la mradi bali ni akili na uwezo wa kufikiri tu katika kazi.

> Kuwa wakala wa shirika, kampuni au taasisi fulani: Unaweza kujua bidhaa za kampuni f'lani na kubeba huo wasifu na kuzitangaza. Beba bidhaa hizo na kutafuta wateja kupitia mitandao ya kijamii au mtandao wa watu ulionao na utalipwa pesa na mwenye bidhaa. Unajua kwenye nyakati hizi, mtu unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, whatsapp nakadhalika kutangaza bidhaa yako bila kutumia gharama kubwa. Hauhitaji mtaji wa fedha hapa ili ufanye kazi hii bali unahitaji hamasa na utayari tu.

> Nguvu ya afya ya mwili na roho: Kila mtu amepewa nguvu ya akili na mwili pamoja na afya njema ambayo anaweza kuitumia kufanya kazi ambayo haihitaji elimu na utaalam mkubwa sana, bali maamuzi ya kinafsi tu. Mfano kilimo cha jembe la mkono, kuponda kokoto na kazi za kubeba mizigo viwandani hazihitaji elimu kubwa, bali nguvu na utayari wako. Unaweza kufanya kazi hizi kwa muda kwa lengo la kupata pesa kidogo uendelee na shughuli zingine. Usifanye kazi hizo kwa sababu umekosa kazi za kufanya bali ufanye kwa malengo.

> Taaluma yako: Kama umejaliwa kusoma na kuelimika kufika ngazi za juu ni matumaini yangu utakuwa umebobea katika huduma f'lani. Kama ni sheria, ualimu, utalii, uhasibu, uongozi nakadhalika. Tambua kuwa una chanzo cha mtaji. Buni na kuanzisha hata mradi mdogo unaoendana na taaluma yako.

Mfano kama wewe ni mtaalamu wa mifugo na kilimo haihitaji kukaa na kusubiria ajira serikalini. Rudi kijijini na utumie taaluma uliyopata kuanzisha kilimo cha biashara. Anza na shamba dogo kadri ya uwezo wako, jinsi unavyokazana ndivyo unavyokuwa kibiashara na kupata mafanikio. Hauhitaji mtaji mkubwa wa fedha kufanikisha hili, bali ni ubunifu tu na utayari wa kuanza.

> Mungu amekupa kipaji gani: Kuna wengine wamepewa vipaji vya uimbaji, uchekeshaji, uongeaji mzuri wa kuvutia katika biashara, uchoraji, na mambo mengine mazuri. Hebu tumia kipaji chako kutengeneza hela huku ukimtanguliza M/Mungu. Mimi binafsi naamini tulipewa vipaji kwa madhumuni matatu. Moja ni kumtukuza yeye aliyetupa kama muumba wa vyote. Pili ni kuwasaidia wengine hasa wasiojiweza na jamii kwa ujumla. Na mwisho ni kutusaidia sisi wenyewe kwenye maisha yetu ya duniani. Anza kuonesha kupaji chako ili watu wakuone uanze kuingiza pesa. Uzuri ni kwamba hauhitaji pesa yetote kuonesha kipaji chako.

> Mtandao wako wa watu ukoje: Wataalamu wa idadi ya watu (population) wanasema ongezeko la watu Afrika ni mtaji sahihi wa mafanikio. Nataka kukuuliza wewe unaesoma, umezungukwa na watu aina ipi?

Ukweli mchungu ni kuwa watu wengi tumezungukwa na marafiki wasiokuwa na msaada kwetu. Wakati mwingine sisi ndiyo hao marafiki tusiokuwa na msaada kwa wenzetu. Acha nikupe zoezi: Angalia namba za watu waliopo kwenye simu yako ni watu wangapi? Unaweza kuwapigia na wakakupa msaada? Wengi wetu tumejaza majina ya watu ambao tunapoteza nao muda na sio wa kusaidiana. Hebu jitahidi utengeneze Mtandao wa watu ambao ni sahihi kwako wewe. Hawa baadae watakuwa nguzo imara ya kukunyanyua wewe. Tatizo ni kwamba tunaishi maisha ya ujanja ujanja mwingi na utapeli ndiyo maana hatuna marafiki wa kweli. Nikuambie tu, watu ni mtaji tosha kabisa wa mafanikio. Ukitaka kuamini hilo waulize wanasiasa watakuambia. Na uzuri wa hapa ni kwamba hauhitaji pesa nyingi kutengeneza mtandao sahihi wa watu, bali uaminifu na nidhamu tu.

> Kujitolea kwenye taasisi, Kampuni au Shirika: Moja kati ya jambo ambalo vijana wengi wanajisahau, haswa waliomaliza chuo, ni kujitolea kwanza bila malipo. Hii ni njia moja wapo inayofungua milango ya fedha na mafanikio. Unapojitolea kufanya kazi katika shirika unatengeneza nafasi ya kusaidiwa kuliko kukaa nyumbani au vijiweni.

Huwa najiuliza moyo walionao wenzetu wa ulaya kuja Afrika na kuamua kujitolea katika serikali zetu. Lakini ni mara chache sana kuona waTanzania wakijitolea kwenye taasisi. Hebu leo tafuta taasisi na shirika na anza kujitolea bila malipo uone fursa na mafanikio zitakavyokufuata kwa muda mfupi.

> Mikopo yenye masharti nafuu: Njia nyingine inayoweza kukusaidia kupata pesa ya kuanzia ni kwa njia ya mkopo. Tatizo ni kwamba mikopo huwa ina sura mbili. Kwanza ni chanzo cha madeni. Pili husaidia kuinuka kimafanikio kama utatumika ipasavyo. Hata hivyo, kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kabla haujachukua mkopo. Kwanza pata elimu ya kutosha kabla ya kuchukua mikopo ili ujue faida na hasara zake. Pili tafuta taasisi au benki zenye riba nafuu kwenye mikopo yake. Tatu epuka kukopa kutoka kwa watu binafsi au taasisi ambazo hazijasajiliwa maana hawa watakufirisi bila huruma. Nne kopa fedha ambayo utaweza kuiendesha na kuzalisha faida. Ni muhimu sana kutotumia fedha ya mkopo kwa matumizi yasiyokusudiwa. Tano na mwisho, fanya utafiti wa kutosha kwa biashara unayotaka kuifanya kwa kutumia mkopo wako.


Hitimisho: Nina imani ukitumia njia hizo hapo juu unaweza kupata kipato cha kufikia malengo yako. Ni matumaini yangu pia kuwa hautolala ndani na kukata taama eti hauna mtaji. Una malengo ya kufanya biashara? Inuka, buni na anza kutembea kwani uwezo wako ni mkubwa mno.

Kumbuka pia, Kiwango cha mafanikio yako kinategemeana na ukubwa matatizo unayoyatatua ambayo wengine wameyakimbia.
 
Theory za PDF hizi.

‘Minding my business’ is Only Business on the earth you can start without funding apart from that business NEVER.

Theory za kwenye PDF hizi.

Portfolio | 2020
 
Theory za PDF hizi.

‘Minding my business’ is Only Business on the earth you can start without finding apart from that business NEVER.

Theory za kwenye PDF hizi.

Portfolio | 2020
Haha! Ni suala la mindset tu, kaka.
 
Back
Top Bottom