Pete ya ndoa haibadilishi tabia ya mtu! Ni kiashiria kwamba huyu mtu ameoa/olewa hasa kwa utamaduni wa kimangaribi...kuna wenzetu ambao nadhani wao kuvaa pete sio lazima....na actually sidhani kama ni lazima kuvaa pete ya ndoa kuthibitisha mapenzi yako kwa mkeo/mumeo
kinachotokea sasa hivi kama walivosema wengine, ni tabia ya baadhi ya watu siku hizi kupenda kuiba na kuendelea kuonekana wako single....hasa akina dada ambao utawakuta wapo mjini, wanamaisha ya juu, usafiri, nyumba nzuri ya kuishi na pesa lakini ukimuuliza kazi gani hasa anafanya huwezi pata jibu..mara afisa uhusiano wa kikampuni uchwara, mara secretary etc....akina dada wa hivi unakuta wanatunzwa na ATM za walio kwenye ndoa....!
Ndo kanakuja kale kautaratibu ketu ka utambulisho,.....kwenye pombe tec.."huyu ni shemeji yenu" hata kama inajulikana ana mke halali wa ndoa.
kwa upande wa wanaume wanaokubali kuwa ATM, sababu ni nyingi na tumeshazijadili sana hapa,
All in all it boils down to an individual, tabia yake ikoje, haiwezi kamwe kubadilishwa kwa kuvaa pete ya ndoa....nikisema hivyo simaanishi watu mkazitupe mmliozivaa!
ZD na Chris mnavishana lini? tupeni progress mi na Mrs hapa tujiandae...