- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu nimekutana na hii taarifa kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa Instagram wakieleza wawili hao wamekutana jana ikiwa ni siku mbili kuelekea uchaguzi mkuu Uganda.
Je ni kweli?
Je ni kweli?
- Tunachokijua
- Uganda inatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa Urais Januari 15, 2026 huku kukiwa na matukio mbalimbali ikiwemo kuzimwa kwa Internet kuanzia Januari 13, 2026.
Madai
Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram baadhi ya watumiaji wake wamechapisha Picha inayomuonesha Abdul Hafidh Ameir pamoja na Gen. Kainerugaba Muhozi na kuelezwa kuwa wawili hao wamekutana nchini Uganda ikiwa ni siku mbili tu zimesalia kuelekea uchaguzi mkuu Uganda. Tazama hapa na hapa.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kina kuhusu uhalisia wa picha hiyo na kubaini kuwa inapotosha uhalisia.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandai ikiwemo nyezo za kidigitali ikiwemo google reverse image search imebainika kuwa picha hiyo si ya mwaka 2026 bali ni ya 2022.
Picha hiyo ni kutoka katika video ya mwaka 2022 ambayo ilisambazwa pia katika mitandao mbalimbali ya kijamii mathalani hapa na kurushwa na Televisheni.
Video ama picha hiyo pia ilitumika katika baadhi ya taarifa ikiwemo iliyochapishwa na AP News ambapo walieleza kuwa ni katika tukio la Mei 7, 2022 ambapo Abdul pamoja na Jenerali Kainerugaba Muhoozi ambaye kwa wakati huo alikuwa Luteni Jenerali na pia kamanda wa jeshi la ardhini walihudhuria katika moja ya sherehe huko mjini Entebbe.