POTOSHI Je, picha hii ya mfungwa aliyevaa hereni kutoka gereza la UKONGA ni halisi?

POTOSHI Je, picha hii ya mfungwa aliyevaa hereni kutoka gereza la UKONGA ni halisi?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
1778570214635.png
 
Tunachokijua
Mei 09, 2026 Jeshi la Magereza lilifanya Hafla ya kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi ngazi ya juu na Uongozi Daraja la pili kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga Dar Es Salaam, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Madai

Kumekuwapo na picha inayosambazwa mtandaoni inayodaiwa kuonesha moja ya mfungwa waliokuwapo katika hafla hiyo akiwa amevaa hereni jambo lililoibua maswali mengi mtandaoni kama wafungwa wanaruhusiwa kuvaa hereni.


Je, ni upi uhalisia wa picha hiyo?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa picha hiyo si halisi bali imehaririwa kwa Akili Unde. Kupitia Google Reverse Image search imebainika picha halisi inayoonesha wafungwa wanawake wawili wakiwa na Rais Samia ambapo Ukurasa wa Ikulu unabainisha majina yao ambayo ni Bi. Grace Chiduo na Bi. Irene Mseluka waliopata ujuzi wa kushona bidhaa mbalimbali wkiwa gerezani katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) Ukonga.

Aidha picha hiyo hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo changamoto ya maandishi ya kwenye kilemba cha kichwani jambo ambalo ni kasoro za kawaida kwa picha zinazohaririwa au kutengenezwa kwa AI.

Sanjari na hilo nyenzo za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa AI zinabainisha kuwa upo uwezekano wa zaidi ya asilimia 99 ya picha hiyo kutengenezwa kwa AI.
​
screenshot-2026-05-12-093108-png.3587387
Back
Top Bottom