SI KWELI Je, picha hii ya Rais Trump kwenye tukio la ufyatuaji risasi ni halisi?

SI KWELI Je, picha hii ya Rais Trump kwenye tukio la ufyatuaji risasi ni halisi?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
1778045626548.png
 
Tunachokijua
Baada ya tukio la kusikika kwa milio ya risasi wakati Rais wa Marekani Donald Trump akiwa kwenye Dhifa ya Waandishi wa Habari wa White House (WHCD), picha hii iliyohifadhiwa hapa ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kumuonesha Trump akiinua ngumi juu.

Je, ni upi uhalisia wa picha hiyo?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa picha hiyo si halisi bali imehaririwa kwa kutumia Akili Unde.

Uchambuzi wa picha halisi kutoka kwenye Dhifa ya Waandishi wa Habari wa White House jijini Washington siku ya Aprili 25, 2026, haujapata picha yoyote inayomwonesha Trump akitolewa nje kama inavyoonekana kwenye picha inayosambazwa mtandaoni, wala video yoyote inayothibitisha kutokea kwa shambulio la risasi ndani ya ukumbi huo.

Ishara nyingine inayothibitisha kuwa picha si halisi ni kutofautiana kwa maelezo yaliyo kwenye picha inayosambazwa na picha halisi na video zilizorekodiwa katika tukio hilo. Vyombo vya habari vilinasasa picha na video wakati Trump akiondolewa ukumbini hapo katika mazingira na mwonekano ambao ni tofauti kabisa na ule unaoonyeshwa kwenye picha inayosambazwa, jambo linaloashiria kuwa haina uhusiano wowote na tukio halisi na haina ukweli wowote wa kihabari.

Kupitia Google Reverse Image Search unabainisha matokeo yanayoonesha kuwa picha hiyo "ilitengenezwa kwa Google AI,"​

screenshot-2026-05-07-095401-png.3585094
Aidha Hive Moderation inabainisha pia kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa AI.
1778137180690-png.3585095
Back
Top Bottom