POTOSHI Je, picha hizi zinazoonesha matukio ya mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini 2026?

POTOSHI Je, picha hizi zinazoonesha matukio ya mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini 2026?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Siku za hivi karibuni, taifa la Afrika Kusini limeendelea kukumbwa na changamoto ya kuongezeka kwa mashambulizi na vurugu za chuki dhidi ya wageni (xenophobia). Maandamano hayo yanadaiwa kulenga kuwaondoa raia wa kigeni nchini humo.

Pamoja na kuendelea kwa matukio hayo, kumekuwa pia na ongezeko la matumizi ya picha za zamani na picha zilizohaririwa kwa teknolojia ya akili unde (AI) katika kuelezea matukio ya sasa yanayoendelea nchini humo.

Moja ya chapisho lililosambaa kupitia chombo cha habari cha Mwananchi lilikuwa na kichwa kisemacho, “Ukaburu unarejea Afrika Kusini”, kikitumia picha ambayo kwa uhalisia ilipigwa mwaka 2015 wakati wa machafuko yaliyolenga raia wa kigeni katika eneo la Johannesburg Central Business District (CBD).

PICHA UKABURU.webp


Uhalisia wa Picha hiyo inaonyesha dereva wa teksi akishambuliwa na kundi la watu wakati wa mashambulizi dhidi ya wageni yaliyotokea Aprili 2015, hivyo si picha ya matukio ya mwaka 2026 kama ilivyowasilishwa kuelezea matukio yanayoendelea nchini afrika kusin.

Vilevile, baadhi ya machapisho kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo Facebook, yametumia picha hizo za mwaka 2015 kuelezea hali ya sasa nchini Afrika Kusini, jambo ambalo linaweza kuwapotosha wasomaji kwa kuamini kuwa picha hizo ni za matukio ya hivi karibuni.

Sambamba na hilo, ukurasa wa DW Afrika umetumia picha ya mwaka 2019 katika chapisho lililosema kuwa Ghana ilikuwa imewasilisha malalamiko kwa Umoja wa Afrika (AU) dhidi ya Afrika Kusini kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara ya chuki dhidi ya wageni,

FIMBO.jpg

uhalisia wa picha ni unaonesha kuwa picha hiyo ilitokana na vurugu za mwaka 2019 na si matukio ya sasa ya mwaka 2026.

PICHA DW.jpg

uhalisia wa picha unabainisha kuwa Wakazi kutoka eneo la Hosteli ya Jeppe Men walionekana wakipiga kelele kupinga matumizi ya virungu katika eneo la CBD mnamo Septemba 3, 2019, baada ya mji mkuu wa kifedha wa Afrika Kusini kukumbwa na wimbi jipya la ghasia dhidi ya wageni.

Aidha, chombo cha habari cha First Daily nacho kilitumia picha ya zamani katika habari iliyosema kuwa The Nigerians in Diaspora Organisation Africa (NIDO Africa) imewataka Wanigeria wanaoishi Afrika Kusini kuwa waangalifu kutokana na kuongezeka kwa taharuki ya mashambulizi ya xenophobia katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Picha hiyo haikuwa ya matukio ya sasa bali ilitumiwa tena kuhusisha na hali inayoendelea mwaka 2026.

Mbali na matumizi ya picha za zamani, pia kumekuwa na kusambaa kwa picha kadhaa zilizohaririwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde ili kuonyesha vurugu na uharibifu unaodaiwa kuendelea nchini Afrika Kusini. Uchunguzi unaonyesha kuwa baadhi ya picha hizo si halisi wala hazihusiani na matukio ya sasa.

PICHA AKILI MNEMBA.jpg

Kwa mfano, moja ya picha hizo kwa uhalisia ilichapishwa na vyombo mbalimbali vya habari vya Afrika Kusini mwezi Septemba mwaka 2020. Wakati huo, vyombo hivyo vilikuwa vikiripoti kuhusu uharibifu wa barabara uliofanywa na wakazi wa Umzinyathi, wilaya iliyopo katika jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini. Hivyo, picha hiyo haina uhusiano wowote na vurugu za xenophobia zinazoendelea mwaka 2026.

UHALISIA WA PICHA.jpg
 
Tunachokijua
Siku za hivi karibuni, taifa la Afrika Kusini limeendelea kukumbwa na changamoto ya kuongezeka kwa mashambulizi na vurugu za chuki dhidi ya wageni (xenophobia). Maandamano hayo yanadaiwa kulenga kuwaondoa raia wa kigeni nchini humo.

Miongoni mwa picha iliyochapishwa na tovuti ya Mwananchi ikiwa na kichwa kisemacho, “Ukaburu unarejea Afrika Kusini”,ambapo halisia ni kwamba picha hiyo imekuwepo mtandaoni tangu mwaka 2015.​
picha-ukaburu-webp.3586262

Vilivile picha hii ambayo iliwahi kuchapishwa na DW mwaka 2019 na 2020 imekuwa ikisambazwa mtandaoni na kudai kuonesha matukio ya 2026 nchini humo jambo lisilo la kweli.

Mfano tovuti ya First Daily ilitumia picha hiyo na kichwa cha habari na kudai Shirika la Wanigeria Wanaoishi Ughaibuni Barani Afrika. (NIDO Africa) limewataka Wanigeria wanaoishi Afrika Kusini kuwa waangalifu kutokana na kuongezeka kwa taharuki ya mashambulizi hayo katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.​
678812528_945942994811316_5991792586339711054_n.jpg


Aidha picha hii inayoonesha watu wakichimba barabara pia haihusiani na matukio ya 2026. Picha hiyo kutoka Afrika kusini, ilichapishwa mtandaoni mwezi Septemba mwaka 2020.

Aidha taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya News24, chombo cha habari cha Afrika Kusini, inaeleza kuwa wakazi walikuwa wakiandamana kutokana na ukosefu wa maji na umeme katika jamii yao.​

EihOiw0XgAcD3D2
Back
Top Bottom