Kwa Hali inavyoonekana hii Vita imeonekana kuwa un popular kwa Russia au Putin.
1. Kwanza, nchi nyingi zimeonesha huruma kwa Ukraine kuliko kuishangilia Urusi kuipiga Ukraine. Kwa mfano Poland amegoma kucheza na Urusi kwenye Qualifiers za world cup na Putin kunyanganywa mkanda mweusi kwenye Judo.
2. Pili, Wanachi wa Ukraine wameonesha kusimama na kupigania nchi yao kwa kushika silaha. Kuna wabunge na Kuna Rais mstaafu kaamua kuingia vitani kupigania nchi hii inaleta picha ngumu kwa Urusi kwamba hata tukiiteka Ukraine bado tutapingwa na wanchi wa hapa.
3. Tatu, Kitendo Cha Rais kuingia kwenye uwanja wa Vita kimechochea uzalendo kwenye nchi husika. Hivyo kwa njia Moja ana nyingine imeleta ugumu kwenye Vita.
4. Nne, Kitendo Cha Raia wa Urusi kuandamana kupinga nchi yao kuingia vitani Ni njia mojawapo ya kuonesha kwamba hiyo Vita haikuwa priority ya nchi.
Mwisho, Vita vikitulia na URUSI akashindwa kuidhibiti Ukraine, Kuna hatari akaletewa mashtaka ya uhalifu was kivita na vikwazo Mara mbili kumkomoa maana maadui zake walitaka kuona reaction itakuwaje kwenye Vita, Sasa wameona hata Raia wa Ukraine na Urusi hawaungi mkono hiyo Vita.