Je, Raia tunaruhusiwa kutembea na ushahidi wa kesi za jinai, kama ugaidi na mauaji?

Je, Raia tunaruhusiwa kutembea na ushahidi wa kesi za jinai, kama ugaidi na mauaji?

masanjasb

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
2,364
Reaction score
867
Kumekucha wanajamvi?

maana kulala uraiani na kuamka jela limekuwa jambo la kawaida sana hapa kwetu ndo maana nauliza kama kumekucha na makucha yetu salama?

Leo nina swali moja kuu la msingi na kama raia wa Tanzania ninao uhuru wa kuhoji as long as sivunji katiba na sheria za nchi yangu.

Swali kuu nimeuliza hapo juu kabisa kuwa ni kwa nini bwana Lameck alikuwa na ushahidi wa kesi ya Lwakatare na hata kuuonyesha bungeni katika bunge hili linaloendelea sasa tena mbele ya waziri wa wizara husika na wala hakuchukuliwa hatua yoyote.

Je kwa raia wa kawaida naweza kaa na ushahidi wa kesi kubwa kama ya ugaidi mfukoni mwangu na hata kuonyesha rafiki zangu huku mtaani kuwa nina ushahidi wa kesi ya mtu fulani nasubr kuitwa tu ili nikautoe huu ushahidi,naniko tayari kuutoa hapa duniani na hata Mwigulu?<mbinguni kwa lugha za kabila moja maarufa hapa nchini ni Mwigulu.

Kwa faida ya wengi naomba nijibiwa na wanasheria na sio pro-cdm wala pro-ccm
 
Swali lako inategema limeulizwa wakati gani au nchi gani, kwa Tanzania na hasa katika kipindi hiki cha wamu ya 4 kila kitu kinawezekana, kwa nchi nyingine au hata hapa Bongo wakati wa utawala mwingine hili halikuwezekana. Tumeshuhudia jinsi ambavyo sheria ilivyowekwa kapuni kipindi hiki kuliko muda wowote, angalia jinsi mafisadi wa EPA walivyo pewa muda wa kushitakiwa tena Bungeni na muheshiwa rais wa nchi n.k
 
Mazindu Msambule una maana ningeuliza kipindi cha mkapa jibu lingekuwa zuri zaidi kuliko kipindi hiki cha Rais pendwa?
 
labda kabla ya kuuliza hilo swali naomba ujiulize hivi ushahidi ni nini? sidhani kama ni kosa mtu kutembea na ushahidi mpaka atakapo hitajiwa ( kwa hiyari yake). Ila katika kuutafuta ushahidi kuna mbinu nyingi sana huwa zinatumika au kutumiwa na wanoutafuta wakiwemo polisi. Bbadhi yake ni kuteswa au kuminywa hadi useme ukweli inapobidi. kuna mambo mengi sana yanayofanyika kinyume cha sheria lakini kwa kuwa hakuna aliyeshitaki au kushitakiwa basi hata ushahidi dhahiri kabisa huwa hauna maana! Mfano mdogo tu.... wakati uko secondari ulikuwa unawajua wanafunzi wenzako wangapi wanavuta bangi au wana wapenzi na hukuwahi kuwashitaki panapo husika? nimalizie kwa kukuuliza pia kwa nini ulkuwa unatembea na ushahidi?ilikuwa ni kosa?......au hiii ya Rwakatale tu?..eeh?
 
Back
Top Bottom