Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Kuwa rais mstaafu kuna dhima kubwa. Haitoshi tu kuwa mualikwa kwenye shughuli na kukaa high tables za mialiko mbalimbali basi hiyo ikawa sababu ya roho yako kuwa kwatu. La hasha kuna dhima ya kuhakikisha nchi hii inakuwa ya haki zaidi kila siku, inayostawi zaidi kila siku.
Kwa kweli mimi kila nikimuona rais mstaafu, sioni kama ni mtu ambaye anajali, anakerwa, anasikitishwa na mambo yanayoendelea nchini.
Tangu astaafu sijawahi kumsikia akiongea neno haki, sijawahi kumsikia akizungumza neno la kuwapa pole waliotekwa, au kuuawa kinyama kama mzee Kibao. Kiufupi ni kama amechagua kuwa mstaafu "poa", mstaafu wa kucheka na kutabasamu kwenye dhifa na mialiko, lakini mambo serious ya kuchagiza mabadiliko chanya ya kujenga taifa la kidemokrasia zaidi, la haki zaidi wala hana time na wala hayuko concerned.
TLS walitoa listi ya watu zaidi ya 80 waliopotea nchini, huyu Jakaya hili linamstua kweli?. Au kwa sababu keshakuwa rais, katimiza ndoto yake ya kuwa rais, na kwa kuwa yeye na mkewe na mtoto wake mambo yamewanyookea kwa hiyo HE DOESN'T GIVE A DAMN ABOUT THE REPUBLIC?
Naandika haya kwa sababu partly sababu mojawapo ya Taifa kuwa hapa ni yeye. Alishiriki kikamilifu kufukiafukia maoni ya wananchi tuliyotoa kwenye rasimu ya Warioba, tukatumia mabilioni ya jasho la mlipa kodi, lakini baada ya hapo akatuacha Solemba, na tokea wakati huo hana time na kuzungumza au kusaidia katiba mpya ipatikane.
Yeye kwenye misiba ya watu ni bingwa wa historia kuonyesha nchi hii ilitoka wapi, na aliyekufa alikuwa "big brains" kiasi gani, lakini yeye sasa yuko hai hatuonyeshi anautumiaje huo uzoefu mkubwa anatuma ujumbe kuwa anao ili kusaidia kuzuia mambo ya utekaji, wa wananchi nchini.
Nchi hii iko katika mode ya mambo ya kidhalimu ya akina Iddi Amin Dadaa, abductions, torture lakini tuna rais mstaafu ambaye uso wake hauna majonzi hata kidogo.
Ni kweli yeye siyo Nyerere ambaye alikuwa bold kusimama na kuikosoa serikali ya Mwinyi, lakini trust me laiti Nyerere angekuwa hai asingeacha mambo ya utekaji wa wananchi yanaendelea asikemee waziwazi. Hivyo ndivyo Nyerere alivyochukia umwagaji damu wa watu.
Mwalimu hakuwa perfect, Yes aliweka watu vizuizini na kufrustrate wapinzani wake lakini alikuwa anaithamini mno damu ya mtu.
Sasa sisi tunajiuliza. Mzee Jakaya unanenepaje wakati Watanzania wanatekwa, wanapotezwa, wanauawa?. Unaanzaje kuimba Iyena Iyena na kucheza wakati kuna wazazi nchi hii wanalala bila kuwaona watoto wao wanaotekwa na kupotezwa.
Mzee hebu tueleze, hii inakuwaje hii?.