- Source #1
- View Source #1
Picha kutoka ukurasa wa Kenya News Flash imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa Rais William Ruto ametangaza kuwa vipimo vya DNA vya kubaini baba wa mtoto vitakuwa vya lazima nchini Kenya.
Graphic hiyo, yenye tarehe Oktoba 6, 2026, inamnukuu Ruto akidai kuwa serikali itagharamia vipimo hivyo na pia itachukua jukumu la kuwahudumia watoto waliozaliwa nje ya ndoa.
Lakini je, Rais Ruto kweli alisema hayo?
Graphic hiyo, yenye tarehe Oktoba 6, 2026, inamnukuu Ruto akidai kuwa serikali itagharamia vipimo hivyo na pia itachukua jukumu la kuwahudumia watoto waliozaliwa nje ya ndoa.
Lakini je, Rais Ruto kweli alisema hayo?
- Tunachokijua
- Mjadala kuhusu vipimo vya DNA umekuwa ukiendelea Kenya, hasa baada ya visa vya watu kudai kugundua kupitia vipimo vya ubaba kwamba watoto waliokuwa wakiwalea hawakuwa wao kibaolojia. Hata hivyo, mjadala huo haujathibitishi kuwa serikali imetangaza mpango wa vipimo vya lazima.
Baada graphic hii ya kusambaa sana mtandaoni hakuna ushahidi wowote kwamba Rais Ruto alitoa kauli hiyo. Hakuna tangazo rasmi kutoka State House au serikali linalosema kuwa vipimo vya ubaba vitakuwa lazima nchini Kenya. Africa Check
Hakuna taarifa hiyo katika vyombo vya habari vinavyoaminika, jambo ambalo lingekuwa la kawaida endapo Rais angetangaza sera kubwa ya kitaifa kama kufanya vipimo vya DNA kuwa vya lazima.
Verdict: Si ukweli
Dai kwamba Rais William Ruto ametangaza vipimo vya DNA kuwa vya lazima nchini Kenya ni bandia.
Hakuna ushahidi kwamba Ruto alisema serikali itawafanyia wanaume vipimo vya DNA bila malipo, wala kwamba serikali itajenga kituo kikubwa cha kuwahudumia watoto waliozaliwa nje ya ndoa kama graphic hiyo inavyodai.