Je ramadhan singano alirogwa na makomando wa simba?

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Nakumbuka Ajibu aliposajiliwa yanga sc makomandoo wa simba walikuwa wanapanga waende kwa mganga kumroga Ibrahim Ajib wakati wanapanga hayo jamaa mmoja ambaye namfahamu akasema na nakumbuka mpaka leo alichosema

"Msisumbuke kwenda kumroga Ajibu ,Ajibu mimi namjua ni mvivu wa mazoezi ,kipaji anacho ila ni mvivu mpeni muda ataboronga tu yanga na atakosana nao tu.


Mjadala huu wa makomando wa simba yaliniacha na maswali mengi mpaka nikamkumbuka mchezaji wa Azam Ramadhan singano aliyeondoka simba vibaya kama Ajibu hakuondoka kwa shari walitaka kumroga na sijui kama walimroga au kauli ya yule jamaa iliwafanya wasimroge

Je vipi kwa singano aliyeondoka simba kwa Shari bila ya shaka naamini makomando wa simba walimuendea kwa mganga singano na kumroga .,singano hakuachwa salama wallahi

Nb:makomando ni wale kabla ya mechi wanaenda kulinda viwanja....kwa pamoja tushirikiane kupiga vita makomando kwenye vilabu haswa simba na yanga
 
mpira wa sasa hauna uchawi ila mazingaombwe tu!watu kama akina mzee mchawi(huyu ndye aliyeleta mvua kila simba alipokuwa na mechi ngumu na tamaduni hii hadi leo ipo),mzee ali mapilau wale ndo walikuw wachawi yan timu pinzani kuna muda ilibidi wasindikizwe na jopo la waganga na wazee wa kimila vinginevyo walifia njiani!
 
MTAZAMO WANGU KUHUSU SINGANO NI KAMA IFUATAVYO:-

SINGANO ANA KIPAJI HALISI CHA MPIRA. WACHEZAJI WA AINA YAKE WAPO WACHACHE SANA HAPA BONGO MFANO MDOGO MWANGALIE JINSI KICHUYA AU MARCEL BONIVENTURE WA MAJIMAJI WANAVYOCHEZA. HAJALOGWA WALA NINI. TATIZO NI MFUMO WANAOTUMIA AZAM HAUENDANI NA AINA YAKE YA UCHEZAJI. NA SIO YEYE TU MWANGALIE FRANK DOMAYO "CHUMVI" ALIYEKUWA YANGA NA HUYU ALIYEPO SASA HIVI AZAM. KWA HIYO MCHEZAJI ANAYEWIKA TIMU FULANI AANGALIE ILE TIMU ANAYOENDA JE ATAFITI NA MFUMO WAO. NA HIVI VILABU PIA VIANGALIE VINAPOFANYA USAJILI JE MCHEZAJI WANAYEMSAJILI WANAMUHITAJI KWELI NA ANAENDANA NA MFUMO WAO AU WANASAJILI TU BASI?

NIKIRUDI KWA SINGANO KWANZA NAMPA POLE KWANI WALIOMCHOMBEZA AONDOKE SIMBA WENGINE WAZI WAZI KABISA NA NI WAANDISHI WA HABARI WAANDAMIZI WAPO KIMYA BADALA YA KUMSAIDIA MAWAZO ATOKE HAPO ALIPO . YEYE MWENYEWE NI KAMA AMEKATA TAMAA VILE. USHAURI WANGU KWAKE. KWANZA BADO UMRI UNAMRUHUSU KUCHEZA MPIRA KWA MUDA MREFU. ASIONE AIBU AENDE AKAWAOMBE RADHI VIONGOZI WA SIMBA NA HATA IKIWEZEKANA AOMBE ASAJILIWE BURE KABISA. HILI LA KUSAJILIWA BURE NAJUA WENGI MTASHANGAA LAKINI TAFUTENI KICHUYA AU MILIPILI WAMESAJILIWA KWA KIASI GANI HALAFU MUANGALIE SIGN FEE ZAO ZITAKUWA KIASI GANI BAADA YA MIKATABA YAO KUISHA MMOJA MWAKA HUU MWINGINE MWAKANI. ARUDI NYUMBANI SIMBA AANZE MOJA NA KWAKUWA NI FUNDI KURUDI KWENYE FOMU HAITACHUKUA MUDA MREFU. KWA SASA KATIKA LIGI YA TANZANIA NI WACHEZAJI WAWILI WANAOWEZA KUMSAIDIA KICHUYA ATAKAPOKUWA NA KADI AU AKIUMIA NAO NI SINGANO NA MARCEL BONIVENTURE WA MAJIMAJI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…