Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Ni kawaida kwa nchi hii, watawala wetu kutuambia wameunda Tume kuchunguza matukio mbalimbali yanayotokea ya ajali, lakini Tume hizo zinapokamilisha Kazi zake na kukabidhi kwa watawala, huwa hazisomwi kwa Umma na badala yake, zinafichwa!
Nieleze kwa kutoa mifano michache, iliundwa Tume ya kuchunguza ajali ya moto, Katika soko la Kariakoo, jijini Dar mwezi July mwaka jana na Tume hiyo ikakamilisha Kazi yake na kuikabidhi kwa Serikali, lakini hadi hivi leo, ripoti hiyo imefichwa kabatini na imekuwa SIRI, Ili wananchi tusijue nini kilitokea!
Ripoti nyingine iliyofichwa "kabatini" baada ya Tume iliyoundwa kukamilisha Kazi yake ni ya Mauaji ya mfanyibiashara wa madini huko Mtwara, Mussa Hamisi, aliyeuawa na Polisi na baadaye kumpora pesa zake zake za madini, kiasi cha shilingi milioni 70, ambapo Tume hiyo iliundwa mwezi February mwaka huu, ambapo hadi leo hii, ripoti hiyo nayo imefichwa na wananchi hatujaelezwa nini kilibainika Katika ripoti hiyo!
Kwa hiyo ndiyo maana wananchi tunakuwa na shauku, pamoja na kauli hiyo ya Serikali, kuwa ripoti hiyo ya ajali ya ndege, itakuwa tayari ndani ya siku 14, tokea ndege hiyo ilipopata ajali tarehe 6 mwezi huu, je ripoti hiyo itatolewa kwa Umma wa watanzania, au ndiyo kama kawaida ya Serikali hii ya CCM, kuamua kuificha, Ili isijulikane kwa Umma wa watanzania, kama walivyozoea?
Ifahamike kuwa Umma wa watanzania una Haki ya kujua nini kilitokea siku hiyo ya ajali, kwa kuwa wanaamini kuwa kulikuwa na uzembe wa hali ya juu, wa vikosi vya uokoaji Katika ajali hiyo ya ndege, hadi kusababisha vifo vya watu 19, na Ili dhana hiyo itoweke vichwani mwa watu, ni LAZIMA ripoti hiyo itolewe hadharani kama ilivyoahidiwa na Serikali.
Ndiyo maana wengi tumeshuhudia, yule Kijana mvuvi, Jackson Majaliwa, akipewa "promo" kubwa baada ya kubainika kuwa yeye ndiye aliyekuwa shujaa siku hiyo, baada ya kuuvunja mlango wa ndege, kwa kutumia Kasia ya mtumbwi wake na hivyo kunusuru Maisha ya watanzania 26 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Mungu ibariki Tanzania