Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Watu wengi wanakimbilia kununua router za Airtel, Vodacom, Tigo au Ttcl kwa Matumizi mbalimbali bila kujua utofauti wao uliopo kuhusu hizo router.
Sasa Leo nakupa maujanja kutokana na ripoti mbalimbali za mitandaoni nakuambia router gani nzuri kwa Matumizi ya Ofisini na Nyumbani ili kuwa salama usipigwe Tena sio 😀.
Kwani Router ni kitu gani ?
kwa ufupi tu Router ni kifaa kinacho tumika kuweza kuunganisha vifaa vyako kuanzia simu, laptop, Tv pamoja na intaneti Kisha kusambaza hiyo intaneti kwenye vifaa vyote.
kumbuka router inafanya kazi ifuatayo;
- kuunganisha intaneti Toka kwenye simu au fiber (Ttcl, Zulu nk).
- kusambaza intaneti kupitia wifi ya Nyumbani kwako / ofisini.
- inasimamia Matumizi kwa kugawa intaneti kwa usawa, kuzuia watu kutumiwa intaneti
Inawezekana unahitaji kujua ni Router gani inafaa kwa Matumizi ya Nyumbani na Ofisini, Leo nakupa Elimu kuhusu hii Teknolojia ili kuwa makini unapo nunua
Router Nyumbani nchini Tanzania.
1.Tigo Tanzania (Sasa Yas)
Ukiwa na hii router utaweza kufurahia ikiwa huko maeneo ya mjini spidi inakua nzuri, iko imara kuliko Airtel, inafaa kwa Matumizi ya Streaming na Matumizi ya kawaida.
👎Ubaya wa Yas
• Router zake ni Gharama kubwa.
• Coverage yake kubwa mjini sio kila mahali haswa vijijini.
2. Airtel Router
• Router zake ni bei ni nafuu sana
watu wengi wanazipenda.
• Spidi yake nzuri sana 4G / 5G maeneo ya Mjini.
• Router zake ni nzuri kwa Matumizi ya kawaida utaweza enjoy.
👎Ubaya wa Airtel
• Spidi yake inabadilika haiko stable
• inaweza kuwa na data limits (Fupi) bila watu kujua.
• Intaneti yake inakata kata sana.
3. Vodacom Router
• Vodacom wana Coverage Eneo kubwa nchi nzima.
• spidi yake nzuri utapata 4G / 5G maeneo ya mjini.
• Router zake zinafaa kwa Matumizi ya biashara au kawaida.
👎Ubaya wake
• Bei yake iko juu haswa bando na router yenyewe.
• Mara nyingi unalipia kwa Mwezi postpaid.
• sio nzuri kama biashara yako ni kubwa (limited control).
4. TTCL Router
• Wao wanatoa option ya Fiber ni nzuri kwa biashara aiseeh.
• ina uwezo wa ku support watu wengi zaidi ya 60+ bila shida.
• Mara nyingi wanatoa Public IP ( hivyo ni nzuri kwa biashara).
👎Ubaya wa TTCL
• wabovu kutoa huduma kwa Wateja
• wako Slowly sana mpaka kuja kufungiwa intaneti kazi unayo.
• Network yao haipatikani baadhi ya maeneo unapata tabu kuunganishwa.
🚨Hizi Router ni nzuri kwa;
• Matumizi ya Nyumbani
• biashara ndogo ndogo unaweza ku enjoy kutumia.
🚨Zitakusumbua ikiwa;
• Utaifanya kwa Matumizi ya intaneti Cafe kubwa.
• Hotel / Guest / Lodge inayopokes watu Wengi.
• Biashara Yenye watu Wengi hazifai.
💡Sio mbaya ukatumia hizi Router
• 🔥 Tigo au Vodacom (kama signal ipo strong)
• 🔥 TTCL fiber (kama imefika eneo lako) utaweza ku enjoy Intaneti.
Ebu tuambie ni router gani nzuri unatumia tuachie maoni yako tujifunze sote 💭.
#router #internet #technews #bongotech255 #fahamuzaidi