Je, salamu ya kwenye simu inajitosheleza?

Je, salamu ya kwenye simu inajitosheleza?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Wakuu,

Hebu tupeane uzoefu .

Mfano imetokea ukaongea na mzazi wako kwenye simu pengine hamjaonana tangu asubuhi, mkasalimiana salamu ya shikamoo na kujuliana hali. Je baada ya muda mfupi mkikutana kuna haja ya kusalimia tena au mtaendelea na maongezi mengine tu?

Au tuchukulie hujaonana na mpenzi wako kwa siku nzima, lakini muda mfupi kabla ya kuonana naye uliongea naye kwenye simu. Je, ukionana naye kuna haja ya kuanza na salamu tena au utaendelea na stories zingine tu?

Je, wewe mtu akikufanyia hivyo utachukulia kawaida au ni muhimu kusalimia tena uso kwa uso?

images.jpg
 
Mkuu salamu ni kila wakati, kwan kwenye salaam watu hujiliana hali ambayo kikawaida hubadilika kila wakati.
Kama ulimsalimia shikamoo mtu mzima dk 20 zilizopita kwenye simu ukikutana nae utamsalimia tena?
 
Kumbuka tunaishi katika mfumo wa Softcopy and hardcopy

Ukimtumia mtu laki moja kwenye simu (softcopy) unafikiri unaweza kutegemea kujibiwa kua huna adabu kwasababu hujampa mzazi pesa mkononi (hardcopy)

Zaidi zaidi utasikia mbona hujaweka yakutolea

Sasa kwanini isitumike sheria hiyo hadi kwenye salamu?

Sikufichi huu undezi wa shikamoo tunao sisi waafrika na inferior zetu zilizochangiwa na utumwa
 
Unasalimia tuu hamna tatizo.
Kwani ye akiuchuna bila kudai shikamoo kuna tatizo?

Katika vitu nisivyovipenda ni kusalimia salimia mtu shikamoo. Ndo maana sometimes nikipita around nikakuta nyomi ya wazee najibipu kujifanya niko busy na simu ili kuua soo
 
Mimi hiyo salamu ya Shikamoo huwa siielewi kabisa.

Napendelea>

Habari za asubuhi, umeamkaje, habari za mida, habari za siku n.k.
 
Mkuu salamu ni kila wakati, kwan kwenye salaam watu hujiliana hali ambayo kikawaida hubadilika kila wakati.
Salamu ni kila wakati hatukatai, ila salamu ya shikamoo imekaa ki-wack sana

Halafu sijui kwanini waafrika tumejijengea imani kua salamu ndio heshima?

Especially shikamoo, ukimsalimia mzee "habari yako" kesho unasikia kengele ya kijiji imelia baraza la wazee limekuwekea kikao kwamba kijana huna heshima
 
Mimi hiyo salamu ya Shikamoo huwa siielewi kabisa.

Napendelea>

Habari za asubuhi, umeamkaje, habari za mida, habari za siku n.k.
Yes hizo ndio salamu ambazo zinatambulika kidunia, shikamoo ni salamu inayotumika katika muktadha wa kitumwa

Yani "niko chini ya miguu yako" Aaah mzee mi pia ni mkubwa kwa wengine lakini hunikuti nikikomalia kuwaambia madogo wanipe shikamoo
 
Salamu ni kila wakati hatukatai, ila salamu ya shikamoo imekaa ki-wack sana

Halafu sijui kwanini waafrika tumejijengea imani kua salamu ndio heshima?

Especially shikamoo, ukimsalimia mzee "habari yako" kesho unasikia kengele ya kijiji imelia baraza la wazee limekuwekea kikao kwamba kijana huna heshima
Ni kweli aisee,hii salamu ya shikamoo inakuzwa sana,wakati ukimwambia mtu umeamkaje au habari ya jioni ndio ina maana zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hiyo salamu ya Shikamoo huwa siielewi kabisa.

Napendelea>

Habari za asubuhi, umeamkaje, habari za mida, habari za siku n.k.

Kwahiyo bro hata kwa aliyekuzidi umri parefu, unamsalimu kwa namna hiyo?
 
Back
Top Bottom