secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 2,998
- 4,948
Leo mchana katika pita pita nilikuta watu katika mtaa mmoja wanabishana kuhusiana namna ambavyo samaki hupata watoto au vifaranga kama watu wengine wanavyodai. Katika mjadala huo kulikuwa na baadhi ya watu waliodai kuwa samaki anazaa watoto na kulikuwa na wengine waliodai kuwa samaki ana taga mayai. Ubishi ulichukua takribani dakika 45 bila suluhu na Kwa kuwa mimi biology niliacha kuisoma tangu nilipokuwa form one nilibaki njiapanda.
Mungu si Athumani alijitokeza mwalimu mmoja wa shule ya sekondari iliyopo katika mtaa ule na Kwa bahati nzuri alikuwa mwalimu wa biology. Tukamwita huku tukidhani kuwa ana jibu lililo sahihi, tulipomwuliza swali hilo alitabasamamu kidogo na kuanza kushusha nondo, akasema.
"Samaki anatapika watoto au Kwa lugha nyepesi anatema watoto, hii ni Kwa sababu samaki haendi nje ya maji kama mamba, hivyo inamuwia vigumi kutaga majini, isitoshe samaki hana uke na wote hapa ni mashahidi katika hilo labda kama Kuna mtu amewahi kuona uke wa samaki atuambie. Ukiachilia mbali taalima yangu ya ualimu, baba yangu ni mvuvi kule Kanda ya ziwa, tulishavua samaki tukakuta midimoni mwao wana watoto wengi so samaki anatema watoto tumeelewana! "
Mi nilifikiri Kwa sekunde kadhaa nikamwambia Kwa hiyo kama samaki hawana uke wanawezaje kujamiiana hadi wakapata mimba? Mwalimu kusikia hilo swali akajifanya amepigiwa simu ya dharura, akasogea pembeni kidogo, mara huyoooo! katokomea. Kwa kweli waalimu wa TZ ni bongolala Wala tusiwaani.