Yohimbine
JF-Expert Member
- Jan 6, 2019
- 873
- 1,841
Wakati dirisha la usajili likikaribia kufungwa huko barani ulaya kumekuwa na habari mbalimbali zikiendelea lakini kubwa ni winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho akihusishwa na kujiunga Manchester United.Msimu uliopita ulikua ni msimu mzuri sana kwa Jadon Sancho kwani aliweza kufunga magoli 17 katika Bundesliga na kutoa assist 11 lakini ukiangalia aina ya mpira wanaocheza man united kuna wachezaji wengi wa aina yake mfano rashford na martial kwani wote wana wana kasi nzuri ya kuendana na mchezo.
Tatizo la man united naliona lipo katika namba tisa ya nguvu mfano Harry Kane mtu mwenye uchu wa kuliona goli kwani man united wanapoteza nafasi nyingi sana za kufunga hasahasa rashford na martial.Tatizo la pili ni mabeki wa pembeni ,Wan Bissaka amekua ni mzuri sana katika kukaba lakini akiwa na mpira anakosa ubunifu anashindwa kuwa beki wa kisasa kama alfonso davies au trent alexander anorld hivyo solkjaer anapaswa kuliangalia tatizo ili kwa namna tofauti.
Mwisho kabisa ni pale kwenye beki wa katikati baina ya Maghuire na Lindelof wamekuaa hawana muunganiko mzuri kiuchezaji kwa kufanya makosa mengi yanayogharimu timu ndio maana mpaka sasa katika mechi 2 wamesharuhusu mabao matano ,Eric Baily ni beki mzui sana pale united tatizo ni majeruhi tu ndo yanamsumbua kama akiwa fiti na maghuire basi safu ya ulinzi itakua bora sana .Haya ni maoni yangu tu wewe kama mwanamichezo una mawazo gani?
I stand to be corrected